China vs USA: Infrastructure, Technology and Development

Kwani hayo majengo n.k Marekani kwanini hajajenga mkuu?
Marekani hizo skyscrapers alishakuwa nazo kitambo sana, china bado ilikuwa hata haijachipua.

Kuna majengo kama empire state building au WTC haya yalijengwa zamani ingawa sasa hv yamepitwa na wakati.

Hakuna chochote China aweze fanya marekani asiweze mkuu.

Unaweza ongozea hapo

American cities like New York City or Chicago, most land in the cities is already being occupied by existing buildings, to find a flat land (like a parking lot) for a new skyscraper is not easy, available flat land like Hudson Yards is in the minority, in most cases developers must first purchase the old buildings .
 
Mambo yanabadilika mzee. Usiishi kwenye past.
 
Bila ya teknolojia ya kutengeneza baruti ya wachina kusingekuwa na bunduki wala mizinga ambayo ndiyo iliyowezesha Uingereza kuja kuitawala dunia na kuweza kutajirika. Kwa kutumia mizinga ya Royal Navy waliweza kulazimisha biashara haramu ya madawa ya kulevya kufanyika China na wakaunda Benki ya HSBC ili kutorosha pesa.

Teknolojia ya kutengeneza nyuzi za harriri ilitoka China na biashara ya nguo ndiyo iliyoleta mapinduzi ya viwanda Uingereza na kuwafanya wawe mabepari wa kuu karne ya 17 na kuja kuwa na koloni kubwa la Marekani.
 
Mambo yanabadilika mzee. Usiishi kwenye past.
Past kivipi wakati empire state qbuilding au golden gate bridge zinajengwa china alikuwa wapi?

Mambo ambayo mchina anafanya sasa hivi Marekani keshafanya kitambo sana mkuu
 
Past kivipi wakati empire state qbuilding au golden gate bridge zinajengwa china alikuwa wapi?

Mambo ambayo mchina anafanya sasa hivi Marekani keshafanya kitambo sana mkuu
Hakuna High-Speed Train huko USA. Mzee utaachwa USA ndiyo basi tena ndugu yangu.
 
Uko sahihi!

Asichokijua mleta uzi ni kwamba, hata hizo skyscrapers zenye urefu mkubwa zaidi nchini China zimekuwa designed na Wamarekani.

Ulinganisho wa mleta uzi unakosa mashiko kwa sababu hiyo. Aliyefanya architectural design ya majengo yaliyopo Marekani kwenye jiji kama New York ndiye huyohuyo amehusika kwenye majiji yaliyoko China.

Cha kushangaza zaidi na pengine mleta uzi hafahamu ni kwamba, hata jengo refu zaidi duniani (Burj Khalifa) lililopo Dubai limebuniwa na Mmarekani.

Mmojawapo wa designers wa majengo marefu yaliyopo China ni kampuni ya ujenzi inayoitwa Kohn Pedersen Fox ya New York nchini Marekani. Hawa wamehusika kwenye majengo mengi ya kibiashara yaliyopo China likiwemo Shanghai World Financial Center.

Link:
 
Nadhani ukweli anaujua ila basi tu anajitutumua. Afike haraka hapa ajibu hapo.
 
Mleta uzi, ulinganisho wako wa kimiundombinu kati ya China na Marekani una makosa mengi ya kisomi.

Ulinganisho unapaswa kuzingatia zaidi yule aliyehusika kwenye ubunifu ama usanifu wa miundombinu, siyo yule ambaye ni mtumiaji wa mwisho wa miundombinu husika au yule ambaye miundombinu hiyo ipo nchini kwake.

Miundombinu unazoziona nchini China hususani majengo marefu (skyscrapers), asilimia kubwa ni miradi iliyobuniwa na kampuni na mashirika ya kigeni tena hasa kutoka Marekani ambaye mara nyingi ndiye mshirika mkuu wa kibiashara wa China.

Umetaja jengo refu zaidi nchini China la Shanghai (Shanghai Tower). Aliyehusika katika usanifu wa jengo hilo ni kampuni ya usanifu wa majengo ya Gensler iliyopo San Francisco nchini Marekani.

Website yao hii hapa. Wameweka mpaka PDF document inayoeleza jinsi design process ya jengo zima ilivyofanyika:

Achilia mbali Gensler, nenda kafanye utafiti kuhusiana na hizi kampuni zingine mbili za hiyo USA unayojaribu kuilinganisha na China:

1) Kohn Pedersen Fox
2) Skidmore, Owings & Merrill

Hao wawili pekee wamehusika katika usanifu wa majengo matano yaliyoko kwenye orodha ya majengo 10 marefu zaidi duniani.
 
Mzee China kuna mamilion ya skyscrapers. Unaona tu skyscrapers tu wili tu unakuja kubweka. Kwanini huko USA wasijenga?
 
Reference Wikipedia!!!! Mzee are yo serious?
 
Mzee China kuna mamilion ya skyscrapers. Unaona tu skyscrapers tu wili tu unakuja kubweka. Kwanini huko USA wasijenga?
Nilidhani umetuletea uzi ili tuujadili kisomi, kumbe umeleta uzi kwaajili ya ushabiki tu, ndugu?!

Kati ya majengo 10 marefu zaidi nchini China, majengo 9 yamebuniwa na Wamarekani. Nimetaja kampuni kadhaa za Kimarekani ambazo zimehusika kwenye usanifu wa baadhi ya majengo marefu zaidi duniani. Fanya utafiti!
 
Kwenye field ya construction hii ni kawaida.
 
Past kivipi wakati empire state qbuilding au golden gate bridge zinajengwa china alikuwa wapi?

Mambo ambayo mchina anafanya sasa hivi Marekani keshafanya kitambo sana mkuu
Ulinganisho unapaswa kuzingatia zaidi yule aliyehusika kwenye ubunifu ama usanifu wa miundombinu, siyo yule ambaye ni mtumiaji wa mwisho wa miundombinu husika au yule ambaye miundombinu hiyo ipo nchini kwake.

Mnaijuwa Panama canal na maajabu yake ya kiuhandishi (iliyojengwa na wamarekani zaidi ya miaka 100 iliyopita) na impact yake kiuchumi? Pound locks zinazotumika kwenye Panama canal ili kuipitisha meli usawa wa juu au chini, in invention ya wachina, zaidi ya miaka 1000 iliyopita lakini hata huwezi sikia ikitajwa.

I'm not pro anything but this notion of burying contibutions of other civilizations makes me sick. You guys mentioned about the Golden gate bridge but forgetting (not knowing) that the chinese were the first to come up the the idea of suspension bridge, during the Han Dynasty.

Marekani imejengwa kwa steel industry (reli, madaraja na skyscraper structures), hawa wakina Andrew Carnegie walitajirika sana na biashara hiyo. Msichokijuwa ni kwamba uwezo wa kutengeneza steel kwa wingi ulitokana na teknolojia ya blast furnace ambayo kwa mara ya kwanza ilitumika China.

Ukiangalia juu juu unaweza kuona wachina wanakopi kila kitu ila kiundani utaona wao ndiyo waliokuwa wa kwanza kugundua mambo mengi kama karatasi, uchapishaji wa vitabu, navigation, baruti, utengenezaji wa nguo, na hata mbinu za kivita n.k. Huwezi kuwa na population kubwa vile kwa bahati mbaya, hapo inaonesha kulikuwa na mifumo mzuri wa chakula, madawa, afya na ulinzi.
 
China ipo na majiji zaidi ya 200.
Usiichukulie China kama Malawi mzee. Huna exposure ya kuijua dunia mzee. China kwa sasa is a talk of earth.

Pitia uone big construction co. in the world

China inaongoza.
 
Kwani kinacho zungumziwa hapa ni yupi mbunifu wa majengo kati ya hizo nchi mbili au ipi nchi imemzidi mwenzie kwenye miundombinu ?
 
Also mchina amejenga Great Wall zaidi ya miaka 2000 iliyopita. Leo uje useme USA.

Soma geopolitics na Historia ya dunia mzee.
 
Nani ameichukulia China kama Malawi? Hoja zako ziko kishabiki zaidi kuliko kisomi!

Wewe unazungumzia construction wakati mimi nazungumzia architecture. Hapo ndipo tatizo lilipo. Hakuna construction bila architecture.
 
Kwani kinacho zungumziwa hapa ni yupi mbunifu wa majengo kati ya hizo nchi mbili au ipi nchi imemzidi mwenzie kwenye miundombinu ?
Demographics kati ya hizo nchi mbili ni tofauti sana hivyo kipimo cha idadi ya miundombinu hakiko sahihi. Kila nchi hapo inajenga miundombinu kwa kuzingatia masuala mbalimbali ikiwemo idadi ya watu.

Hoja zangu zimejikita katika suala la usanifu (architecture). Architecture ndiyo msingi wa miundombinu zilizopo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…