China wazindua meli kubwa inayotumia umeme kujiendesha

Kaka yake shetani

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2023
Posts
5,771
Reaction score
14,732
Kampuni ya COSCO Shipping, ambayo ni mali ya serikali ya China, imeanzisha meli kubwa zaidi inayoitwa Green Water 01.

Meli hii kubwa, yenye uzito wa zaidi ya tani 10,000, inafanya kazi kwa kutumia umeme pekee. Ina urefu wa mita 119.8, upana wa mita 23.6, na kina cha mita 9. Inaweza kutembe kilomita 19.4 kwa saa (maili 12 kwa saa).

Meli hii inaweka rekodi mbalimbali katika sekta ya bahari, ikiwa ni pamoja na urefu wake, upana, uwezo kubeba tani za mzigo (zaidi ya tani 10,000),

Meli inaendeshwa na betri kubwa yenye nguvu zaidi ya kWh 50,000.

Teknolojia ya umeme kwenye vyombo vya usafiri inazidi kukuwa kasi.

 
Kwani inalingana na ya kwetu ya MV mwanza anao enda kuanza kazi hivi karibuni.
 
Sisi bado tunapambana na Bwawa letu la Mwl Nyerere
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…