China ya leo ni nchi yenye uhusiano wa karibu na dunia

China ya leo ni nchi yenye uhusiano wa karibu na dunia

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
2022123121152880521.jpg


Katika mkesha wa sikukuu ya mwaka mpya, rais Xi Jinping wa China alitoa salamu za mwaka mpya wa 2023, akibainisha kuwa, China ya leo ni nchi yenye uhusiano wa karibu na dunia, na inachangia busara na mipango ya China kwa ajili ya amani na maendeleo ya binadamu wote.

Mafanikio ya China kutokana na mshikamano na juhudi kubwa za wananchi wote yamekuza maendeleo na kutia moyo duniani. Katika mwaka uliopita, China ilishinda changamoto zilizosababishwa na janga la UVIKO-19 na hali ya utatanishi duniani, na kuandaa Michezo ya ya kushangaza ya Olimpiki ya Majira ya Baridi. China ilifanikiwa kurusha vyombo vya anga ya juu vya Shenzhou NO. 13, No. 14, na NO. 15 kwa nyakati tofauti, na kukamilisha kituo chake cha anga ya juu. China ilitengeneza manowari ya tatu ya kubeba ndege za kivita ya “Fujian”, ambayo iliimarisha zaidi nguvu ya China ya kudumisha amani na utulivu. Ndege ya kwanza ya C919 ilikabidhiwa kwa shirika la ndege, na kupita hatua ya kwanza katika soko la ndege kubwa za abiria... Kama Rais Xi alivyosema katika salamu zake za mwaka mpya, mafanikio hayo yote yanatokana na bidii na jasho la watu wote, na mshikamano ndio nguvu kuu ya China. Mafanikio ya China yameonesha kwamba mshikamano na juhudi kubwa ni chanzo cha nguvu, kama nchi zote duniani zikishirikiana na kushikamana, dunia itakuwa na mustakabali mzuri zaidi.

Kuwajibika kwa China kumeleta imani kwa dunia katika kukabiliana na changamoto na kufikia malengo ya maendeleo. Mwezi Aprili mwaka jana, Rais Xi alitoa Pendekezo la Usalama Duniani kwa mara ya kwanza kwenye Mkutano wa Boao, akifafanua msimamo wa China wa kuhimiza ushirikiano katika masuala ya usalama duniani. Pendekezo hilo limetoa mpango wa China katika kukabiliana na changamoto za usalama na kufikia amani na utulivu wa muda mrefu duniani. Katika mkutano wa 17 wa viongozi wa G20 uliofanyika mwaka jana, rais Xi kwa mara nyingine tena alisisitiza Pendekezo la Maendeleo Duniani, akihimiza nchi kubwa zibebe majukumu ya kuchangia maendeleo ya kimataifa.

Kufungua mlango zaidi kwa China kumechangia ushirikiano wa kunufaishana duniani. Katika mwaka uliopita, China imeendelea kuhimiza ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na miradi husika imefanywa kwa utaratibu. Wakati huo huo, maonesho mbalimbali ya kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara yakiwemo Maonesho ya Canton, Maonesho ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika, na Maonesho ya Kimataifa ya Uagizaji wa bidhaa wa China kutoka nchi za nje yaliendelea kufanyika nchini China. Licha ya hayo, mwaka jana China iliandaa mazungumzo ya ngazi ya juu kuhusu maendeleo ya dunia, na kupendekeza “Hatua Nane Kuu za Pamoja” kwa ajili ya ushirikiano wa kivitendo kati ya China na nchi za Kiarabu, na sekta tano muhimu za ushirikiano kati ya China na nchi za Ghuba...

Uhai wa uchumi wa China umehimiza kufufuka kwa uchumi wa dunia. Katika mwaka uliopita, China ilishinda changamoto zilizotokana na janga la UVIKO-19 na mazingira ya kutatanisha ya kimataifa. Pato la Taifa la mwaka jana lilitarajiwa kuzidi renminbi Yuan trilioni 120, sawa na dola za kimarekani trilioni 17.14. Uchumi wa China una ustahimilivu na uhai mkubwa, na hali yake ya kimsingi ya kuwa na mwelekeo mzuri kwa muda mrefu bado haijabadilika. Mwishoni mwa mwaka jana, China ilirekebisha hatua zake za kukabiliana na janga la UVIKO-19, na uchumi ulianza kuonyesha uhai zaidi. Mwaka huu, uchumi wa China unatarajiwa kuimarika zaidi, jambo ambalo limeleta matarajio zaidi kwa dunia.

Kama Rais Xi alivyosema katika salamu zake, China ya leo ina uhusiano wa karibu na dunia. Katika mwaka mpya, China itaendelea kusonga mbele kwa ujasiri, na kuchangia zaidi busara na mipango ya China kwa ajili ya amani na maendeleo ya binadamu.
 
China Wanajitahdi aisee they’re doing the great, Wanauza bidhaa katibu za kila aina
 
Back
Top Bottom