China yachochoea utalii wa Afrika kwa kutoa jukwaa la kutangaza biashara, kutafuta uwekezaji na kuvutia Wachina kutalii Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1730857431318.png

Maonesho ya biashara ya Utalii (COTTM) yamemalizika hivi karibuni mjini Beijing, China.

Maonesho haya yaliyofunguliwa tarehe 16 na kuendelea hadi tarehe 18 mwezi wa 10, yalitoa jukwaa muhimu la kufanya biashara ya utalii nje ya China kwa kutoa fursa za uwezekezaji na soko la watalii wa China.

Maonesho ya mwaka huu yamekuwa na mwitikio mkubwa kwani yamevutia wadau wa sekta ya utalii ya China na nje ya China wapatao 3,000 kutoka nchi zaidi ya 200 zikiwemo za Afrika.

Pia yameleta pamoja makampuni yanayoongoza ya utalii, mawakala wa usafiri na mahoteli, yakiwa na lengo moja tu la kutangaza biashara zao, kutafuta fursa za uwekezaji na kuvutia zaidi Wachina kwenda kutalii kwenye nchi zao.

Maonesho haya yaliyoendelea kwa siku tatu, yalifanyika wakati China ikiwa inaendelea na juhudi zake za kuchukua hatua kabambe za kukuza sekta za utalii za nchi za Afrika kwa njia ya kuunga mkono mashirika yake ya ndege kudumisha ushirikiano na mashirika ya ndege ya nchi za Afrika na kuunga mkono makampuni yake binafsi kuwekeza katika sekta ya utalii ya nchi za Afrika.

Kupitia maonesho haya, wafanyabiashara wa nchi nyingi za Afrika wamefaidika kwani wamepokea Wachina waliokuwa wanataka kujulishwa kuhusu bidhaa za Afrika na ambao hawajui watafika vipi Afrika kwenda kutalii, na kuwapatia taarifa sahihi na za kutosha kuhusu utalii wa Afrika.

Kwa nchi za Afrika hili ni jukwaa lenye thamani kubwa sana la kupata kutangaza vivuto vilivyopo na kubadilishana mawazo na Wachina juu ya namna ya kuboresha biashara zao za utalii, ambapo kwa sasa ongezeko la watalii katika nchi hizi limekuwa kubwa sana.

Dkt. Miraji Ussi, Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini China, ambaye alihudhuria maonesho ya COTTOM anasema kwamba maonesho haya makubwa ya utalii ya China yamekuwa na faida kubwa kwasasabu watu wanapata fursa ya kushauriana kibiashara, pia Tanzania inatumai kulikamata zaidi soko la China.

“Maonesho haya yamechangia pakubwa kukua kwa watalii wa China wanaokwenda Tanzania, kwa mfano mwaka 2023 Tanzania ilipokea wageni takriban 45,000, na mwaka huu hadi kufikia mwezi wa 8, Tanzania tayari ilikuwa imeshafikia malengo ya mwaka jana”. Anasema Dkt. Miraji Ussi

Kwa mujibu wa Mpango wa Utekelezaji wa (2025-2027) wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika lililofanyika Beijing mwaka huu, China na nchi za Afrika zimekubaliana kuhudhuria maonesho makubwa ya utalii ya kila upande yakiwemo maonesho haya ya Biashara ya Utalii ya China (COTTOM), ili kukuza zaidi shughuli za utalii za China na Afrika. Wakati huohuo katika kutoa wepesi na urahisi wa watalii wa China kwenda kutalii katika nchi za Afrika bila bugudha, serikali ya China na za nchi za Afrika zimekuwa zikirekebisha sera zake za utoaji viza.

“Serikali za Kenya na China zimejaribu kushirikiana kwa kuwaondolea viza Wachina wanaokwenda kutalii nchini Kenya. Wanapatiwa viza wanapofika uwanja wa ndege bila kufuata taratibu za zamani za kuomba kupitia ubalozini. Njia hii imetoa urahisi kwa Wachina kuja Kenya kutalii.” Anasema Nancy Wangoi Munderu mfanyabiashara mwenye kampuni ya Travel Shore Africa

Wachina waliotembelea maonesho ya COTTOM wameonesha azma kubwa ya kutaka kutalii katika nchi za Afrika, kwani wengi wao walimiminika kwenye mabanda ya nchi za Afrika wakitafuta taarifa husika za mambo ya utalii. Wachina hawa walijawa na hamasa kubwa ya kujionea wanyama pori wa kuvutia wa Afrika pamoja na mlima maarufu wa Kilimanjaro.

“Nimetembelea mabanda kadhaa, nimepata taarifa nyingi kutoka kwa wafanyakazi kuhusu mambo ya utalii barani Afrika. Na nimevutiwa na uhamiaji wa wanyama pale Afrika Mashariki. Natumai nitapata fursa kwenda kujionea.” Anasema mmoja wa Wachina aliyetembelea maonesho hayo

Katika miaka ya hivi karibuni, nchi za Afrika hasa Kenya na Tanzania zimekuwa maeneo pendwa zaidi kwa watalii wa China. Idadi ya watalii wa China wanaoenda kutalii katika Afrika Mashariki inaendelea kuongezeka, ikionesha uwezo mkubwa wa ushirikiano wa utalii kati ya pande mbili.

“Afrika ina rasilimali tele za utalii ambazo zinavutia watalii wengi wa China, wakati huohuo sekta za utalii huko Afrika zimevutia wawekezaji kutoka China. Soko la China ni kubwa, ambalo linathamani kwa marafiki wa Afrika kuja kuangalia. Tunatarajia uhusiano kati ya China na Afrika utaendelezwa siku hadi siku.” Anasema Jane, mfanyabiashara wa utalii

Kwa mujibu wa ripoti ya Maendeleo ya China na Afrika juu ya Ujenzi wa pamoja wa Ukanda Mmoja Njia Moja, China imesaini nyaraka za ushirikiano wa utalii na nchi 31 za Afrika, na kuorodhesha nchi 34 za Afrika kama maeneo ya vikundi vya utalii vya China kwenda kutalii. Katika miaka ya hivi karibuni mahitaji ya China ya kutalii katika Afrika yameendelea kuongezeka na ushirikiano wa mambo ya utalii kati ya pande hizi umezidi kuimarika.
 
View attachment 3144756

Wajapan,wakorea sawa ila sio wachina dhiki waliyonayo kuwaona kwenye mbuga za wanyama ni kama tesla kuikuta Yombo.
 
Back
Top Bottom