China yaiwekea bidhaa zote za Marekani zinazoingia China ushuru wa asilimia 34 kama

China yaiwekea bidhaa zote za Marekani zinazoingia China ushuru wa asilimia 34 kama

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Wakuu,

China imetangaza ushuru wa asilimia 34 kwa bidhaa zote kutoka Marekani, ikiwa nchi ya kwanza kujibu hatua ya Rais wa Marekani, Donald Trump, ya kutoza ushuru mpya kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ya Marekani.

China imesema ushuru huo utaanza kutekelezwa Aprili 10 na baada ya hapo itapeleka malalamiko rasmi kwa Shirika la Biashara Duniani (WTO).

China pia, imetangaza kuzuia na kudhibiti kuiuzia Marekani madini adimu yanayotumiwa katika teknolojia ya matibabu na vifaa vya kielektroniki.

Kufuatia Ushauru wa Trump masoko ya hisa barani Asia na Ulaya yameendelea kuyumba, huku soko la hisa la New York (S&P 500) likishuka kwa asilimia 4.8, anguko lake kubwa zaidi tangu janga la Covid-19 mwaka 2020.

Barani Ulaya, Frankfurt imeshuka kwa asilimia 5, Paris kwa zaidi ya asilimia 4, na London kwa asilimia 3.8. Huko Asia, soko la hisa la Tokyo lilifunga kwa asilimia 2.8 chini, huku Waziri Mkuu wa Japan, Shigeru Ishiba, akitaja ushuru wa Trump kama "janga la kitaifa".

Trump, hata hivyo, amepuuza hali hiyo, akisisitiza kuwa masoko "yataimarika" huku akielekea kwenye mapumziko yake ya mwishoni mwa wiki huko Florida.

ship.png

================================================

China announced 34 percent tariffs on US imports on Friday, the first major economy to fire back against US President Donald Trump's sweeping new levies in an escalating global trade war that sent markets deep into the red.

Countries and companies alike weighed their options and the EU readied for talks with US officials. Potential responses could include retaliatory tariffs or other measures that could escalate a trade war that has raised fears of recession.

China – one of the United States' top trading partners – was first, announcing that tariffs of 34 percent on all American imports would come into effect from April 10 and saying it would file a suit against the World Trade Organization (WTO) over the tariffs.

It also said it would impose export controls on a number of rare earth elements used in medical technology and consumer electronics.

Asian and European stock markets added to their losses after a bloodbath on Thursday that sent New York's broad-based S&P 500 index down 4.8 percent, its biggest drop since the Covid pandemic in 2020.

In Europe, Frankfurt sank by five percent after midday on Friday while Paris shed more than four percent and London was down almost 3.8 percent.

Tokyo's Nikkei index closed 2.8 percent lower, with Prime Minister Shigeru Ishiba describing Trump's tariffs as a "national crisis".

Trump dismissed the turmoil on Thursday, insisting to reporters as he left for a weekend at his Florida golf resort that stocks will "boom".

Source: France24, Financial Times
 
Serikali ya China inashirikiana na Makampuni binafsi kwa kuwapa Funds zote za muhimu kuhakikisha wanateka masoko Duniani.
Funds hizo ni kama hela, ardhi na mengine huku serikali ikishikilia Umiliki wa asilimia Chache kwa baadhi ya makampuni hayo.

Mfano.
Seikali ya China imetoa eneo la Hekari elfu 32 (32,000) huko Zhengzhou, kwa ajili ya kiwanda cha kampuni ya BYD cha kuzalishia magari 😂🙆‍♂️
Hilo Eneo ni kubwa kuliko hata Nchi ya Rwanda ambayo ina hekari 26,000.

Ambapo Kampuni hiyo ya BYD ina malengo ya kuzalisha magari zaidi ya Milioni kila mwaka.

Na China lazma itauza sasa nchi za nje na kuleta Compitition katika Soko since,

Thamani ya hela yao iko chini...
Na wanatengeneza bidhaa ambazo zina Quality.

So wakipeleka bidhaa masokoni, mtu atakuwa radhi achague gari la BYD ambalo lenye teknolojia kubwa kuliko gari la Tesla ambalo lipo bei kubwa na teknolojia Kidogo.

Na magari yakishakuwa mengi yanakuwa Trend kila mmoja atalitaka.
 
Hivo hivo twenzetu

Narekani bila shaka anajiandaa kuhama hii sayari na kwenda sayari nyingine

Hatoi msaada wowote kwa sasa
Kaitoa nchi hiyo NATO na mashirika yote Duniani

Maana yake anahitaji kukusanya fedha nyingi zaidi ili kama vipi ahame hii sayari na kuhakikisha ameivuruga vya kutosha?

Bado mtasikia katoa mtaji wake wooote kwenye bank ya Dunia na mabank yote alikowekeza, Africa na hata Asia!

Ndo mtajua hamuijui vizuri USA baby
 
Back
Top Bottom