Imeripotiwa na gazeti la Mwananchi la leo, januari 6;
Chato. Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya China, Wang Yi anatarajiwa kutua nchini Tanzania kesho Januari 7, ambapo pamoja na mambo mengine atashuhudia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa awamu ya tano ya reli ya kisasa (SGR) inayotoka Mwanza hadi Isaka yenye urefu wa kilometa 341.
Kwa sasa ujenzi wa reli hiyo kutoka Dares Salaam hadi Mwanza unatekelezwa na kampuni ya Yapi Merkezi.
Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Chato leo Januari 6, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi amesema awamu hiyo ya ujenzi itagharimiwa na Serikali ya Tanzania kwa jumla ya Sh3.0617trillion na itajengwa na kampuni mbili kutoka nchini China.
Pia, Profesa Kabudi amesema Waziri huyo atakayetua katika uwanja wa ndege wa Chato Januari 7 jioni, atafanya mazungumzo na Rais John Magufuli na kuzindua chuo cha ufundi wilayani Chato na kutembelea mwalo wa ziwa Victoria wilayani humo kuangalia shughuli za uvuvi.
Amesema Waziri Wang Yi yupo kwenye ziara ya siku tano katika bara la Afrika ambapo kwa Tanzania atakuwepo kwa siku mbili akishiriki mazungumzo binafsi na Rais John Magufuli kisha kufanya mazungumzo rasmi ya kiserikali ya yeye na ujumbe wake.