China yapiga hatua kubwa katika kuwapa fursa wanawake kufanya uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1714626809156.png

Dunia ni nzuri kwa sababu ya sayansi, na sayansi ni nzuri kwa sababu ya wanawake. Hivi karibuni ulifanyika Mkutano wa Baraza la Kimataifa la Uvumbuzi wa Sayansi na Teknolojia la Wanawake wa mwaka 2024. Mkutano huu uliofanyika Aprili 27 mjini Beijing, ulikuwa na kauli mbiu ya "Kuchochea Uhai na Msukumo wa Wanawake". Kihistoria, uwepo wa wanawake katika nyanja za teknolojia na sayansi umekuwa mdogo sana ukilinganishwa na ule wa wenzao wanaume. Hata wakati wanawake wanapochangia katika nyanja hizi, machapisho yanayoelezea kazi zao yanakuwa machache pia.

Kwa kuwa Nyanja ya sayansi na teknolojia imekuwa ikitawaliwa zaidi na wanaume, hamu ya kuandika juu ya michango ya wanawake katika nyanja hizi pia ilikuwa ndogo. Hata hivyo katika miaka ya hivi karibuni muelekeo huu umekuwa ukibadilika kwa kasi hapa nchini China. Wanawake wengi zaidi siku hizi wanaingia katika nyanja za sayansi na uhandisi, pamoja na sayansi na teknolojia, na pia vyuo vikuu vya China vinajitahidi kuvutia wanawake zaidi katika sayansi na uhandisi.

Wakati akihutubia kwenye mkutano wa baraza hilo, Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanawake la China Bibi Shen Yiqin, amesema China inatilia maanani sana nafasi muhimu ya wanawake katika uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia na daima imekuwa ikijali na kuunga mkono ukuaji wa sayansi na teknolojia wa wafanyakazi wanawake. Wafanyakazi hawa wengi wao wamejitolea katika kufanya tafiti na uvumbuzi mbalimbali, na kuleta mafanikio makubwa ya kisayansi na kiteknolojia ambayo yana jukumu muhimu la kusaidia na kuongoza.

Hivi sasa dunia kila siku inashuhudia mapinduzi mapya ya sayansi na teknolojia na mabadiliko ya kiviwanda, hivyo wanawake hawapaswi kuwa nyuma na kushika mkia tu, bali wanatakiwa kuwa vinara katika kufanya tafiti muhimu za sayansi na teknolojia, kuwaandaa wataalamu wanawake, kujenga jumuiya ya pamoja ya sayansi na teknolojia duniani, ili kutumika vizuri kwa ajili ya maendeleo ya sayansi na teknolojia, maendeleo ya wanawake na maendeleo ya binadamu wote.

Kwa sasa nchini China kuna wanawake wapatao milioni 40 wanaofanyakazi katika masuala ya sayansi na teknolojia, idadi ambayo inachukua 45% ya jumla ya idadi ya wafanyakazi wa sayansi na teknolojia. Katika safari ya maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia, wafanyakazi hawa wa kike wamechangia maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa moyo wote na uvumilivu wa hali ya juu. Uvumbuzi wao wa kiteknolojia umekuwa kigezo muhimu katika kuujenga upya ulimwengu na kuweka mustakabali wa binadamu.

Yau Chengtong, mshindi wa kwanza wa Medali ya Fields, tuzo ya juu zaidi katika sekta ya hisabati duniani, ambaye ana asili ya China amesema kuwa matokeo mapya ya sayansi kamwe hayapatikani kwa urahisi, hivyo amesisitiza kwamba kuna haja ya kuanzisha mfumo ambao unawawezesha wanasayansi wanawake wajihisi kuwa wanaheshimiwa sio kwa sababu ya jinsia yao, bali kutokana na matokeo ya kazi zao za utafiti wa sayansi ambazo wametumia juhudi kubwa na kuvuja jasho hadi kupata matokeo hayo.

Katika miaka ya hivi karibuni, Shirikisho la Wanawake wa China na taasisi nyingine wamezindua kwa pamoja Mpango wa Uvumbuzi wa Wanawake katika Sayansi na Teknolojia, ukihimiza kikamilifu utangazaji mashirikisho ya sayansi na teknolojia ya wanawake katika mikoa yote 31, mikoa inayojiendesha na manispaa zote nchini, pamoja na kuuweka mazingira mazuri kwa wafanyakazi wa kike wa sayansi na teknolojia. Taasisi ya Kitaifa ya Sayansi ya Asili ya China na Wizara ya Sayansi na Teknolojia pia zimepitisha sera ya kuwapa kipaumbele wanawake chini ya mazingira mazuri kama hayo.

Lakini cha kusikitisha ni kwamba kwa baadhi ya nchi, hasa nchi za Afrika wanawake na wasichana wengi bado wanakabiliwa na aina hii mpya ya umasikini wa kidijitali, ambao unawatenga na kuwa mbali sana na dunia ya kidijitali. Mgawanyiko huu wa kidijitali umekuwa ni changamoto nyingine ya ukosefu wa usawa wa kijinsia, ambao umesababisha wanawake na wasichana kuachwa nyuma kwenye masuala ya sayansi na teknolojia.

Ndio maana kwa kuzingatia hilo, Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa UNESCO Irina Bokova, alisema kuwa katika dunia ya leo, wasichana na wanawake wengi wana uwezo mkubwa wa ugunduzi wa kisayansi na wana ujasiri wa kukabilaiana na kuyatafutia ufumbuzi yale yasiyojulikana. Kwa vipaji vyao na udadisi wao, wanaweza kuifanya dunia kuwa mahali pazuri zaidi. Hivyo ili kufikia ndoto zao, dunia inahitaji kuwapa msaada kamili na fursa.

Bi. Irina Bokova alisema mwaka 2016 Umoja wa Mataifa ulitangaza Februari 11 kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Wanawake, Wasichana na Sayansi, lengo likiwa ni kuhamasisha wasichana na wanawake wengi kushiriki katika fani za sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati ambayo leo hii inajulikana kama STEM.
 
Nice

...,.............................. character 50 tosha.............
 
These are the Chinese motherfvkers you have been glorifying you slaves?

View: https://twitter.com/bxieus/status/1785979359884460391
 
Wanawake wa China wana akili kuliko wanawake wa kiafrika kwenye mambo ya Teknolojia
 
Wanaume hawapewi ?
 
Back
Top Bottom