China yataka usawa katika usimamizi wa Dunia

China yataka usawa katika usimamizi wa Dunia

Shadow7

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
24,606
Reaction score
39,289
Rais Xi Jinping wa China amesema mfumo wa utawala wa kilimwengu lazima ufanywe uwe wa usawa na uadilifu zaidi, na kwamba kanuni zinazowekwa na nchi moja ama baadhi ya mataifa haziwezi kulazimishwa kufuatwa na wengine.

55687942_303.jpg

Akizungumza kwenye Jukwaa la Boao, ambalo ni mbadala na Jukwaa la Kiuchumi la Davos na lililo maalum kwa mataifa ya Asia, rais huyo wa taifa la pili kwa nguvu ulimwenguni amesema dunia inahitaji zaidi haki na sio utawala wa kundi ama nchi moja.

Xi amewaambia washiriki wa jukwaa hilo kwamba kujenga vizuizi na kulazimisha mgawanyiko kutawaumiza watu wote na kamwe hakufaidishi hata mmoja.

Bila ya kulitaja taifa lolote kwa jina, Rais Xi amesema kuwa dunia ya sasa inapaswa kukataa kurejea kwenye zama za vita baridi, huku akisema China itaendelea kupunguza orodha aliyoiita ‘hasi’ kwa ajili ya uwekezaji wa kigeni.

Kwa muda mrefu sasa, China imekuwa ikitaka kuweka mageuzi makubwa kwenye namna ulimwengu unavyosimamiwa, ikipigania mitazamo na maadili ya nchi nyingi nyengine kuakisika, yakiwemo ya China yenyewe, na sio mataifa machache yenye nguvu duniani.

Mara kadhaa, Beijing imepambana na wadau wakubwa wa usimamizi wa ulimwengu, hasa Marekani, juu ya masuala kadhaa kuanzia ya haki za binaadamu hadi ushawishi wa kiuchumi wa China kwa mataifa mengine.

“Nchi kubwa ionekana kubwa kwa kuonesha kubeba wajibu mkubwa zaidi, na sio kuwalazimisha wengine waifuate.” Alisema Rais Xi.

Marekani yaitenga China

Kombobild Biden und Jinping

Ijumaa iliyopita, Rais Joe Biden wa Marekani aliitisha mkutano wa kwanza wa kilele wa ana kwa ana na Waziri Mkuu wa Japan Yoshine Suga, ambapo China ilikuwa kwenye ajenda ya mwanzo kabisa.

Katika taarifa yao ya pamoja, viongozi hao wawili walisema wana wasiwasi mkubwa juu ya uvunjwaji wa haki za binaadamu katika jimbo Xinjiang la China na pia Hong Kong.

Serikali ya Marekani inaishutumu China kwa kuendesha mauaji ya maangamizo dhidi ya Waislamu wa jamii ya Uighur kwenye jimbo la kaskazini la Xinjiang, madai ambayo China imekuwa ikiyakanusha.

Kama ishara ya wazi wa ushirikiano wa kiuchumi wa Marekani na Japan na katika kuitenga China, Biden alisema Marekani na Japan zitawekeza kwa pamoja kwenye miradi kama vile teknolojia ya mawasiliano ya 5G, maarifa ya kompyuta na biashara ya mitandaoni, maeneo ambayo China imeyahodhi vya kutosha.

Mbali ya ushindani wa kijeshi kwenye Bahari ya Kusini ya China, Marekani inaikosowa China pia kwenye uzalishaji wa gesi zinachofua tabaka hewa na kutokuwa kwake tayari kushirikiana na mataifa mengine katika udhibiti wa athari za mabadiliko ya tabianchi yanayochochewa pakubwa na shughuli za viwandani za China.
 
China alipaswa kuonyesha njia bora ya kufuata sio na yeye analia lia kama nchi masikini za kiafrika.

China kama anasema Marekani ni wanyonyaji basi yeye angekuja na mpango mzuri wa kutoa mikopo ya bei nafuu na misaada ili nchi nyingi zifuate mtazamo wake lakini yeye ndie mnyonyaji mkubwa kuliko hao anaowalalamikia.

China badala ya kuzisaidia nchi yeye anazitumbukiza kwenye mademi makubwa ambayo hayalipiki halafu inatumia hiyo leverage kunyang'anya hizo nchi rasilimali zao kwa sababu ya kushindwa kulipa madeni.

Naamini kama Bandari ya Bagamoyo ingeombwa na nchi za Ulaya isingekua na masharti ya kizezeta kama waliyotuletea China. Hakuna nchi ambayo itaegemea china ikatoboa, haipo, zote zilizoegemea China kama Tanzania ni fukara wa kutupwa.
 
Kabisa
 
China bila Xi hamna kitu

China bila CCP inaanguka fasta

Moja ya kuwa na stable economy na kuwa super power ni lazima uwe na strong administrative system inayoweza kusimamia Maono ama Vision zako hata kama haytokuwepo ziendelee kutelekezwa, wachinese Hawana hii wanamtegemea kila kitu Xi na Chama chao CCP
 
China alipaswa kuonyesha njia bora ya kufuata sio na yeye analia lia kama nchi masikini za kiafrika.

China kama anasema Marekani ni wanyonyaji basi yeye angekuja na mpango mzuri wa kutoa mikopo ya bei nafuu na misaada ili nchi nyingi zifuate mtazamo wake lakini yeye ndie mnyonyaji mkubwa kuliko hao anaowalalamikia.

China badala ya kuzisaidia nchi yeye anazitumbukiza kwenye mademi makubwa ambayo hayalipiki halafu inatumia hiyo leverage kunyang'anya hizo nchi rasilimali zao kwa sababu ya kushindwa kulipa madeni.

Naamini kama Bandari ya Bagamoyo ingeombwa na nchi za Ulaya isingekua na masharti ya kizezeta kama waliyotuletea China. Hakuna nchi ambayo itaegemea china ikatoboa, haipo, zote zilizoegemea China kama Tanzania ni fukara wa kutupwa

Jamaa wana tabia za kimasikini sana we angalia hata katika miradiyao hapa nchini utakuta wafanyakazi wao wapo dhofli hali yani hata nguo za kazi hawana.

Mishahara ndio usiseme wanapewa ela ya kulatu iliwafanye kazi.
 
Back
Top Bottom