China yaweka lengo la asilimia 5 la ukuaji wa uchumi, wakati Marekani inajaribu kuvuruga utaratibu wa uchumi dunia

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1741830747599.png

Kwenye ufunguzi wa mkutano wa bunge la umma uliofanyika hapa Beijing, Waziri Mkuu wa China Bw. Li Qiang amewasilisha ripoti ya serikali inayokadiria ongezeko la uchumi wa China kwa mwaka huu kuwa asilimia 5. Makadirio hayo yamefikiwa kwa kuzingatia utulivu wa ndani, na maendeleo ya hali ya uchumi duniani. Hata hivyo makadirio hayo yametolewa wakati hali ya sintofahamu kwenye uchumi wa dunia ikizidi kutanda, kutokana na sera zenye uhasama kwenye upande wa biashara zinazotekelezwa na serikali ya Marekani.

Kuingia madarakani mwanzoni mwa mwaka huu kwa Rais Donald Trump wa Marekani na amri alizotoa, kumefanya hali ya uchumi wa Marekani kuwa kwenye hatihati, lakini pia uamuzi wake wa kuongeza ushuru wa bidhaa zinazotoka katika nchi nyingine duniani kunaleta hatihati kati nchi hizo.

Kila mtu anajua kuwa uchumi wa Marekani ndio uchumi mkubwa zaidi duniani na ni moja ya mihimili muhimu duniani, kama mhimili huo ukiyumbishwa kutokana na maamuzi yasiyo na msingi, ni wazi kuwa uchumi wa dunia unaweza kutetereka.

Mwezi Machi Rais Trump alitangaza kuongeza ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa zinazoingia Marekani kutoka Mexico na Canada, na asilimia 10 kwa bidhaa zinazoingia kutoka China. Uamuzi huo wa Rais Trump umetajwa na wataalam wa uchumi kuwa sio tu utasababisha mfumuko wa bei nchini Marekani, bali pia utaleta changamoto kwenye mfumo wa biashara duniani.

Brian Bethune, Profesa wa uchumi katika Chuo cha Boston cha Marekani, amesema hatua zinazochukuliwa na Trump zinaleta mshituko mkubwa kwenye uchumi wa Marekani na wa dunia hakujawa na mshtuko mkubwa kama ule wa mwaka 1930 kutokana na sheria ya kodi, iliyopewa jina la Smoot-Hawley. Profesa Bethune amesema kodi hiyo itavuruga minyororo ya ugavi na kuwafanya wazalishaji wa bidhaa wa Marekani kuwa katika hali ngumu. Wanachoweza kufanya wazalishaji hao wa Marekani ni kuwekeza katika nchi nyingine ambako hakuna ushuru na kodi ya kulipiza kisasi, jambo ambalo hata Trump mwenyewe hatapenda.

Hata hivyo tukumbuke kuwa China ni nchi ya pili kwa nguvu ya uchumi duniani, na ni moja wa waagizaji wakubwa wa bidhaa duniani. Ripoti ya serikali iliyowasilishwa kwenye bunge la umma la China na waziri mkuu Li Qiang, inaleta matumaini kuwa uchumi wa China utaendelea kuwa na utulivu na sera zake kwa nchi nyingine zitaendelea kuwa imara. Profesa Cui Hongjian, wa Akademia ya Mambo ya usimamizi wa Kikanda na Dunia ya Chuo Kikuu cha Mambo ya Kigeni cha Beijing amesema katika siku zijazo, China ina uwezekano wa kusisitiza jukumu lake la kuwa nchi inayoleta utulivu, na kuleta hali tofauti kabisa kinyume na sintofahamu inayoletwa na Rais Trump. Amesema kuwa kutetea umoja wa pande nyingi, China inaweza kujiweka tofauti na mtazamo wa Marekani wa maamuzi ya upande mmoja, na hivyo kuimarisha uwezo wake wa mazungumzo na nguvu laini kimataifa.

Umuhimu wa China utazidi kuonekana kupitia miundo mbalimbali ya uchumi kama vile BRICS-Plus na mchango inaotoa kwenye kundi la nchi za kusini. Kwa uwezo wake wa kujiimarisha kama njia mbadala inayoaminika kwenye utaratibu wa dunia unaodhibitiwa na Marekani, China inaweza kuleta matumaini kupitia mipango inayozingatia biashara huria, ushirikiano wa kikanda na maendeleo endelevu. Juhudi kama hizo zinaweza kuimarisha ukuaji wa uchumi na kushughulikia changamoto kubwa za kimataifa kama vile mabadiliko ya tabia nchi, na changamoto nyingine zinazoikabili dunia.
 
View attachment 3268626

Wazayuni wao wanafanya kila liwezekano kulinda nchi yao hata kama usa itacolapse kwao sio issue kubwa sana
 
Back
Top Bottom