Ikiwa ni taarifa ya kwanza ya kisera kutolewa na serikali kuu ya China kila mwaka, waraka huu unachukuliwa kama kiashiria cha vipaumbele vya sera. Kazi kuhusu kilimo na maeneo ya vijijini zimepewa mkazo kwenye ajenda hii kwa miaka 19 mfululizo tangu mwaka 2004.
Waraka huu unatoa wito wa juhudi zaidi kufanyika ili kudumisha na kuongeza uzalishaji wa kilimo, kuongeza hatua kwa hatua mapato ya wakulima, na kuhakikisha utulivu kwenye maeneo ya vijiji kwa ajili ya kukabiliana na janga la Uviko-19 na mabadiliko mengine ambayo hayajawahi kushuhudiwa katika karne iliyopita na kuhimiza mazingira mazuri ya kiuchumi na kijamii.