China yazindua Global Digital Payment System na kuikacha Swift ya USA

Kiukweli hakuna anayeweza kushindana na china ...hakuna ...wamejipanga kuliko neno kujipanga lenyewe ..huyo usa saivi ni mchicha tu kabaki kupandisha tariffs kiholela ita back fire na tumeanza kuona matokeo ya kukurupuka ya trump mwendawazimu
 
Hongera zake mchina ingawa western world still wako mbele ya muda kuna mfumo mpya wa cross borders payment system tena basi ni cryptos ambao very soon utatawala dunia nzima jisomee mwenyewe mtandaoni kampuni ya US inaitwa Ripple Labs, Inc na nyingine inaitwa Stellar Lumens. Mfumo wa Ripple Labs na huo wa Stellar Lumens inatumia sekunde 3-5 kutuma pesa ambayo ni chini ya huo mfumo wa mchina wa sekunde 7!.
Ila narudia tena hongera kwa mchina na huo mfumo wake!
 
Safi sana big up to 🇨🇳
 
Hiyo ni kama unafanya biashara na China tu ila kama unafanya biashara na mataifa kama ya magharibi bado huwezi kukwepa SWIFT.

Na hata China mwenyewe kwenye biashara yake na mataifa mengine kama Marekani ambapo ndipo soko lake kuu lilipo lazima atumie tu SWIFT hana namna.

Na hata Russia moja ya masharti aliyoweka ili kusitisha vita vyake na Ukraine ni kurejeshwa kwenye mfumo wa SWFT kwani wanajua ina faida nyingi ikiwamo kumwezesha kufanya biashara na Marekani na marafiki zake.

Mambo mengi yanayofanyika kuhusiana na biashara duniani yana uongo mwingi sana ambayo hayawezi kubadilisha ukweli ulivyo na ni kitu ambacho wengi humu hawawezi kuelewa kwa sababu za kishabiki.

China kwenye biashara yake na Marekani lazima atumie tu dola na SWIFT hana namna nyingine yoyote ya kukwepa na isitoshe ana hifadhi kubwa sana ya dola za kimarekani kwenye benki kuu yao.
 
Ndo wale pro west wanaabudu dollar
 
Na mataifa mengi si yanafanya biashara na china
 
Na mataifa mengi si yanafanya biashara na china
Nafikiri wewe hata hujui kinachoendelea. Angalia volume ya biashara kati ya Marekani na China halafu linganisha na China na mataifa hayo mengine labda unaweza ukapata cha kuongea.
 
Nafikiri wewe hata hujui kinachoendelea. Angalia volume ya biashara kati ya Marekani na China halafu linganisha na China na mataifa hayo mengine labda unaweza ukapata cha kuongea.
Sicho alichomaanisha,alichomaanisha ni china kutumia huo mfumo wao kufanya biashara na mataifa mengine,jambo ambalo ni dhahiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…