China Yazindua Samaki wa Roboti wa Kibioniki kwa Uhifadhi wa Mito na Mazingira

China Yazindua Samaki wa Roboti wa Kibioniki kwa Uhifadhi wa Mito na Mazingira

Fbn

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
15,749
Reaction score
37,420
China imetengeneza samaki wa roboti wa kibioniki kusaidia katika uhifadhi wa mito na ufuatiliaji wa mazingira.
Samaki huyu wa kisasa umetengenezwa na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Wuhan na unatumia akili bandia (AI) kuiga mienendo ya samaki halisi huku ukikusanya taarifa kuhusu ubora wa maji, kugundua vichafuzi, na kutathmini afya ya mazingira ya maji.

Kwa sasa, roboti huyo ameshatumwa katika Mto Yangtze, ambako anatumia vichunguzi vya hali ya juu kuchambua uchafuzi wa maji na kusaidia watafiti kufuatilia mabadiliko ya kimazingira. Aidha, ana uwezo wa kujiepusha na vikwazo na kujifunza kupitia AI, jambo linalomuwezesha kuzunguka katika maeneo ya maji yenye changamoto kwa ufanisi mkubwa.

Uvumbuzi huu katika uhifadhi wa mazingira unaonyesha jinsi teknolojia ya roboti na AI inavyoweza kutumika kulinda rasilimali za maji. Kwa kufuatilia uchafuzi na kusaidia katika kulinda afya ya mito, samaki huyu wa roboti wa China ni hatua muhimu kuelekea usimamizi endelevu wa mazingira.
IMG_1632.jpeg
 
Ni deni la mama wala sio la taifa maana kila kitu ni mama.
Hili tatizo la halina mwisho
Ataondoka atakuja mwingine na Deni litazidi tu.

Deni halitapungua hata baada ya miaka 100.
Kwa sababu Riba ndio inalipwa
Imefika mpaka vyoo tunasaidiwa, ujue hali ni mbaya
 
Hili tatizo la halina mwisho
Ataondoka atakuja mwingine na Deni litazidi tu.

Deni halitapungua hata baada ya miaka 100.
Kwa sababu Riba ndio inalipwa
Imefika mpaka vyoo tunasaidiwa, ujue hali ni mbaya
Alafu wanasema ni fedha za ndani wananchi walio wengi hawajiulizi fedha za ndani zinatumika huku deni linazidi mara elfu
 
Hili ni kama tishio kwa nchi zingine sasa
Au watakuwepo wengine wamemwagwa kwenye bahari kuchunguza mienendo ya majeshi

Sisi acha tujadili madeni ya Taifa
Wakimwagwa watatu wanne pale Feri, wengine wakimwagwa Bagamoyo wakimalizia ununio na kunduchi Kwisha kazi 😃
 
Noma sana mkuu

Wachina wapo mbele ya muda
Hawana utani na ni wavumbuzi kweli kweli
Unaweza kuamini wanafyatua sio kutengeneza tena, magari ya Umeme tu 2025 wameuza 9.7m duniani

Hawa ndio wasomi sasa
Sisi PhD zetu za kunywa juice ya Madagascar itibu COVID
 
Hili ni kama tishio kwa nchi zingine sasa
Au watakuwepo wengine wamemwagwa kwenye bahari kuchunguza mienendo ya majeshi

Sisi acha tujadili madeni ya Taifa
Tumewaza sawa sawa mkuu nafikiri neno mazingira yalio chafuliwa ni kigezo tu kwaajili ya kukinga lengo lao la kiusalama.
 
Tumewaza sawa sawa mkuu nafikiri neno mazingira yalio chafuliwa ni kigezo tu kwaajili ya kukinga lengo lao la kiusalama.
Kweli kabisa Mkuu
Sasa ni vita ya kiuchumi watu wanachunguzana sana
 
Back
Top Bottom