Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Katika starehe ninazopenda hapa duniani ni kula na kulala, huwa ninapenda kujifunza kupika vyakula tofauti, ninapenda kujaribu kula vyakula tofauti na vile nilivyozoea. Katika marafiki niliyowapata nimeweza kumudu kula vyakula vya nchi wanazotoka.
Kitanda changu ninahakikisha ni kisafi mahali ninapoweza kupata usingizi mzuri kwani hii ni starehe unayopata bila malipo.
Katika vyakula nimejaribu kula Chinese nimeshindwa kabisa, siku ya kwanza nilikuwa na wenzangu safarini, group lote waliamua kwenda Chinese restarant, niliingia chakula chote nilichokula nilirudisha change pale, ilibidi niweke tissue mdomoni nikikimbila bafuni. Mara ya pili binamu yangu alinipeleka buffet ya wa-China, nilishindwa kumwambia hiki hakipandi, tumefika nilijikaza, tumerudi nyumbani yaliyonitokea sina haja ya kusema mengi.
Hivi ni mimi tu au kuna ambao chakula cha wa-China hakipandi?