Chini ya utawala wa Magufuli, Taifa limepata hasara ya mabilioni na pia upotevu mkubwa wa fedha uliozua utata

Ni bora hii hasara lakini watoto wetu wanasoma bure, barabara zimejengwa, tuna umeme hadi vijijini, madaraja yamejengwa, kuliko kipindi kile cha mzee wa msoga
Kumbe so called mtetezi wa wanyonge alikuwa mpigaji pia???
 
We Kenge..umesahau EPA, ESCROW, IPTL, TWIGA, GAS ILIOUZWA WA WACHINA, WATUMISH HEWA, DAWA ZA KULEVYA, RICHMOND.
Kaa kimya..leo tunaona madaraja, flyover, meli zilizonunuliwa, ukarabati wa shule kongwe, viwanja vya ndege, ndege 11..watoto wamasoma buree..
Wakat hizo pesa za escrow zilipopigwaa hayo yote hayakuwepo.
Kaa kimyaa nyau kabisaa ww..

Hizo hela zote zilizopigwa huko nyuma zinafika 1.5t?
 
Hizo ndege ulizzotaja kwenye orodha yako unajua zimesababisha hasara ya sh ngapi mpaka sasa?. Au unaropoka tu
Hivi ww uko dunia ya wapi? Mbona watz ni washamba hiv..au tatizo ni kutokujua kingereza kusoma jinsi mashirika ya ndege yanavyoendeshwa duniani..aisee..mbona tuko nyuma sana kuwa na watu kama nyie..south africa tu mwaka jana..nusu walifunge shirika lao kwa sabab ya hasara lakin kwa sabab ya unyeti wa hiyo biashara serikal ikaingilia katu na kulinusuru..ethiopia the same..kenya hapo tu kwa majiran huwaoni wanavyosurfocate..lakin stil they operate it
.mashirika ya ndege kwa nchi zote huwa kuna hasara wanazopata tena kubwa tu..acha kuwa kilaza brother tafuta hata dictionary usome report za mashirika mengine ya ndege mana kule wanaandika kingereza sio za huyo CAG uchwara na mnafik.
 
Ni bora hii hasara lakini watoto wetu wanasoma bure, barabara zimejengwa, tuna umeme hadi vijijini, madaraja yamejengwa, kuliko kipindi kile cha mzee wa msoga
Kwani kipindi Cha jk mambo hayakufanyika ?

Barabara zilijengwa

Mikopo ilitolewa kwa wanafunzi wengi kuliko kipindi hiki

Mishahara iliongezeka

Hela ilionekana mitaani

Hakukuwa na kufirisi matajiri
Nk
Nk
Nk
 
Hivi ww uko dunia ya wapi? Mbona watz ni washamba hiv..au tatizo ni kutokujua kingereza kusoma jinsi mashirika ya ndege yanavyoendeshwa duniani..aisee..mbona tuko nyuma sana kuwa na watu kama nyie..south africa tu mwaka jana..nusu walifunge shirika lao kwa sabab ya hasara lakin kwa sabab ya unyeti wa hiyo biashara serikal ikaingilia katu na kulinusuru..ethiopia the same..kenya hapo tu kwa majiran huwaoni wanavyosurfocate..lakin stil they operate it
.mashirika ya ndege kwa nchi zote huwa kuna hasara wanazopata tena kubwa tu..acha kuwa kilaza brother tafuta hata dictionary usome report za mashirika mengine ya ndege mana kule wanaandika kingereza sio za huyo CAG uchwara na mnafik.

Usipanick Mkuu, ndege ni hasara.
 
Ni bora hii hasara lakini watoto wetu wanasoma bure, barabara zimejengwa, tuna umeme hadi vijijini, madaraja yamejengwa, kuliko kipindi kile cha mzee wa msoga
Elimu bure mtoto anamaliza kidato cha nne lkn hawezi kuandika hata barua ya kawaida tu ya kuwasalimia wazazi wake, mtoto hawezi kuandika 920,000 au 1,010,000 kama unabisha mtafte hapo ulipo mtaani mwambie akuandikie hizo tarakimu akipatia kunywa soda kwa mangi.
 
Hasara na upotevu huu unaotokana na taarifa za CAG ambapo wanasiasa waliochambua report ya CAG aliepita,Prof. Assad, waliibua utata wa matumizi ya shilling ya shilling trilioni 1.5 na hii ya hivi karibuni inatueleza hasara ya billion 150 katika uendeshaji wa ATCL.

Hasara na upotevu huu uliotokea chini ya utawala wa Magufuli, ni mbali na mamilion na mabilioni mengine yaliyopotea katika sekta za utalii, n.k kama inyoonyeshwa katika report ya CAG ya mwaka huu.

Bado hasara zinazotokana na serikali kufunguliwa makesi katika mahakama za usuluhishi za kimataifa bila kusahau hasara zilizotokana na siasa za hovyo za watu kujiuzulu kwa hoja ya kuunga mkono juhudi na kuliingiza Taifa gharama kubwa za mamilion kugharamia chaguzi ndogo.

Kwa kifupi, katika awamu ya Magufuli, Taifa limepata hasara kubwa Katika baadhi ya maeneo na pia kuna fedha nyingi zimetumika na kuacha utata mtupu kama hayo matumizi ya shilingi trilioni moja yaliyohojiwa na wabunge wa upinzani baada ya kuichambu report ya CAG aliepita(Prof.Assad).

Itakuwa ni jambo jema Bunge kuunda kamati teule kuchunguza utata wa matumizi haya ya shilingi trilioni 1.5 ili umma ujue ukweli ni upi na si hizi kelele za MATAGA kutaka kutuaminisha kuwa ufisadi ulidhibitiwa enzi za Hayati Magufuli tofauti na awamu zilizopita.

Kama hamtaki kuchunguza tuhuma hizi, acheni kumlinganisha Magufuli na watangulizi wake, hasa Kikwete, ambae wakati wake Bunge liliweze kuunda kamati teule na kuchunguza tuhuma zinazoihusu serikali, na pia vyombo vya habari viliweza kuanika kashifa mbalimbali za serikali bila kusahau Whistleblowers (kina Tumbili) waliweza kuanika madudu yaliyokuwa yanaendelea serikalini tofauti kabisa na ilivyokuwa wakati wa Magufuli .
Tumeibiwa sna hawamu ya tano ndo maana vyombo vya habari havikuwa huru na iliminya sana demokarasia lengo lilikuwa kutuhujumu nadhani ndo awamu iliyolisababishia taifa hasara kubwa lazima serikali ichukue hatua kali sana kwa wahusika
 
MWAMBIENI CAG, SISI TUMERIDHIKA!!

1. Mwambieni CAG kwamba sisi wenyewe tumeridhika, tumezoea kuibiwa. Mwambieni tofauti ya wizi wa zamani na huu ni kwamba wizi wa sasa unafaida kwa Wananchi wala asiumize kichwa. Mwambieni sisi Wananchi hatuna tatizo na hasara au wizi uliofanyika wakati wa JPM. Sisi tumeridhika hivyohivyo kwa sababu tuna macho ya kuona!!

2. Mwambieni CAG kwamba tuliibiwa hapa kupitia EPA. Pesa bilioni 135 zikaliwa na watu wachache, wakati huo elimu bure ilikua bado kuja. Mikopo ya elimu ya juu ilikua ni songombingo kwa hiyo hatuoni hatari kuibiwa sasa huku elimu bure ikiwa imeanzishwa na mikopo ikitoka kwa wakati. Sisi tumeridhika kabisa na hasara au wizi wa JPM!!

3. Mwambieni CAG kwamba tuliibiwa hapa bilioni 300 Serikali ikilipa Makampuni hewa katika kashfa ya MEREMETA. Mwambieni hapakua na tatizo lolote na wakati huo bajeti ya Dawa ilikua chini ya bilioni 30 lakini sasa na wizi wa JPM umepandisha bajeti ya DAWA zaidi ya mara tisa; yaani bilioni 270. Mwambieni kwa wizi huu Mungu atupe nini? Tumeridhika sana na wizi wa JPM.

4. Mwambieni CAG kwamba tulishaibiwa sisi kwenye mauzauza ya uwekezaji wa Bulyanhulu na Buzwagi na hata leo hakuna maelezo ya yanayoeleweka. Kodi hazikulipwa na pesa zikapigwa na wajanja wachache. Wakati huo wote madini na migodi yote ilikua ni mali ya wawekezaji wasiolipa kodi, Wananchi ilikua ni marufuku kukaribia migodi katika nchi yao. Kama JPM ameiba halafu wananchi wanachimba madini wenyewe kwa uhuru, ninaumia kwamba atakua ameiba kidogo sana. Wizi wenye manufaa kwa umma una maana zaidi kuliko wizi usio na manufaa. Sisi tumezoea kuibiwa, lakini kwa huu wa JPM tumeridhika.

5. Mwambieni CAG kwamba sisi tumezoea kuibiwa. Tumeshaibiwa haswa, ilikuja hapa tukaibiwa katika Mkataba wa kijinga wa DOWANS. Nchi ikalipa bilioni 111 kwa sababu ya maslahi ya watu wachache. Wakati tunaibiwa kupitia DOWANS, Mv. Victoria ilikua inalaza watu siku mbili ziwani kwa ubovu wake. Maisha yao yalikua hatarini kila safari, leo JPM akiiba au akitutia hasara ya bilioni 60 huku Mv. Victoria ikiwa MPYA kuna tatizo gani? Meli mpya tele kuanzia ziwa Nyasa, Tanganyika na Bahari ya Hindi Kilwa. Tunapenda wizi wa namna hii, angeiba kabisa za kutosha akajenga nyumba nzuri kama wenzake, akamiliki magari za mizigo meupe kukuki na sheli za kumwaga. Au akamilika supermakert za Da'slam kama wenzake. Sisi kuibiwa tumezoea, wizi wa JPM una manufaa, tumeridhika.

6. Mwambieni CAG kuwa sisi tumezoea kuibiwa asijiumize bure na ma-press ya kutangaza vi-wizi vya kitoto hivyo. Tulipigwa hapa pesa TAKATIFU katika Mkataba maarufu wa RICHMOND ulioondoka na Serikali ya mwaka 2008 hadi sasa hakuna kilichofanyika. Wakati tukipigwa pesa za Richmond daraja la Mfugale lilikua halipo, Daraja la Ubungo (Kijazi Interchange) haikuwahi kufikiriwa, Daraja la Tanzanite (Salender) lilikua katika ndoto, lile la Busisi halikufikiriwa kabisa. Kama tumeibiwa leo na mambo yote haya yamefanyika mwambieni CAG sisi roho kwatu, tumeridhika riport zake tupa kule hatusikii la mwazini wala mnadi swala. Tumefunga masikio!!

7. Mwambieni CAG sio hata siku nyingi zilichotwa BOT bilioni 306 kwa kilichoitwa kashfa ya TEGETA ESCROW. Nchi ikaibiwa tena na wajanja wachache, wakabeba pesa kwenye masandarusi. Wakati tukiibiana bilioni 306 za Escrow umeme vijijini ulikua unaunganishwa kwa Tsh. 454,000 ila kwa wizi wa JPM umeme vijijini unaunganishwa kwa Tsh. 27,000; asilimia zaidi ya 70 umeme umefika vijijini. Wizi mzuri kiasi gani huu!? Sasa tunajenga megawati 2400 kutoka Bwawa la Nyerere ili umeme ushuke zaidi. Ingalikua uwezo ni wangu ningalimrudisha mtu huyu aendelee kuiba na kutia hasara zaidi kwa sababu wizi na hasara zake zina manufaa kwa watu. Mwambieni CAG sisi tumeridhika hivyohivyo, atuwache!!

8. Mwambieni CAG sisi tumewahi kuibiwa Twiga mzima akabebwa na shingo yake akaondoka zake. Hii nchi tunaibiana na Wanyama yeye anahangaika na vipesa vidogo vidogo vya matengenezo ya ATCL. Mwambieni wakati tukiibiana TWIGA upatikanaji wa maji Vijijini ulikua ni asilimia 47 na sasa kwa wizi na hasara za JPM upatikanaji wa Maji vijijini umefikia asilimia 70.1 huku mijini upatikanaji ukitoka asilimia 74 hadi 84. Ni mtu mjinga pekee anaweza kuchukizwa na wizi wa JPM, mwambieni CAG sisi tumeridhika tunatamani angekuwepo aibe tena. Hatutakagi ujinga!!

9. Mwambieni CAG kuwa tumeibiwa sana nchi hii. Wakati wote tuliibiwa huku Nchi ikiwa haina Ndege hai hata moja. Mwambieni leo tuna Ndege 11 za kwetu wenyewe. Hizo hasara za ATCL zisimuumize kichwa, hakuna biashara isiyo na hasara, JPM keshawawekea mtaji na heshima ni wajibu wao kutafuta akili za kupata faida sio kuua mtaji. Mwambieni CAG, sisi tunampenda mwizi anayeiba halafu akanunua Ndege kwa ajili ya Nchi nzima, akajenga reli ya kasi, stend kibao za kisasa, masoko kwa ajili ya biashara nk. Kwakweli sisi tumeridhika sana na wizi huu!! Mungu amlaze mahala pema JPM, ametutoa tongotongo!!

10. Mwambieni CAG asipoteze nguvu zake bure kwa sababu hata hao wezi huwa hawafanywi kitu. Mwambieni tumezoea na zaidi tumeridhika na wizi au hasara za JPM. Mwambieni CAG nchi hii imeongozwa na wezi wengi lakini huyu alikua ni mwizi wa heshima. Tunampenda, tutammiss hivyohivyo na yeyote mwenye kumchafua atachafuka kwanza yeye. Tutakua Taifa la kijimga sana kuacha ALAMA za mtu huyu zifutwe na watu wajinga, wavivu
wasio na lolote walioachiwa Nchi wasiongoze wakihangaika na umbea, udaku na ushambenga.
Kwa taarifa yenu #SISI TUMERIDHIKA HATA ANGEIBA NCHI YOTE AIUZE!! Tuna macho ya kuona, tusichoshane.
#TutakukumbukaDaimaJPM.
MenukaJr,
Da'slam-Tanzania.
 
We Kenge..umesahau EPA, ESCROW, IPTL, TWIGA, GAS ILIOUZWA WA WACHINA, WATUMISH HEWA, DAWA ZA KULEVYA, RICHMOND.
Kaa kimya..leo tunaona madaraja, flyover, meli zilizonunuliwa, ukarabati wa shule kongwe, viwanja vya ndege, ndege 11..watoto wamasoma buree..
Wakat hizo pesa za escrow zilipopigwaa hayo yote hayakuwepo.
Kaa kimyaa nyau kabisaa ww..
Acha uongo.

Ukarabatu wa viwanja vya ndege ni project iliyoachwa na Kikwete.
 
Hiyo mirad inaoperate au haioperate? Meli zinasafirisha watu hazisafirishi? Viwanja vya ndege havijakarabitiwa? Shule watoto hawasomi bure?? Vituo vya afya havipo? Acha ushamba mzee..heri utuibie wakat huo huo tunaona tunapata huduma za kijamii hata kama sio bora lakin ni heri kuliko kuzikosa kabisa..awamu zilizopita hela zilikuwa zinapigwa na bado watu wanalia huduma mbovu za serikal..ww ni mmoja kati ya watz wajinga ambao mwalimu asisitiza tuuondoe huo ujinga ila ww bado uko nao mwingi mno.
I am very dissappointed by your views. I gues if you are a graduate probably you are from Yohana University. You are completely incompatible with the current trend especially in the economic percel.

Hapa ndio ninapozipendea K-Vant, ni kiingereza tu, japo haziondoi ukweli.
 
Hivi ww uko dunia ya wapi? Mbona watz ni washamba hiv..au tatizo ni kutokujua kingereza kusoma jinsi mashirika ya ndege yanavyoendeshwa duniani..aisee..mbona tuko nyuma sana kuwa na watu kama nyie..south africa tu mwaka jana..nusu walifunge shirika lao kwa sabab ya hasara lakin kwa sabab ya unyeti wa hiyo biashara serikal ikaingilia katu na kulinusuru..ethiopia the same..kenya hapo tu kwa majiran huwaoni wanavyosurfocate..lakin stil they operate it
.mashirika ya ndege kwa nchi zote huwa kuna hasara wanazopata tena kubwa tu..acha kuwa kilaza brother tafuta hata dictionary usome report za mashirika mengine ya ndege mana kule wanaandika kingereza sio za huyo CAG uchwara na mnafik.
Mkuu tatizo siyo hasara. Tatizo ni kwamba wakati wa Utawala wa Jiwe hatujawahi kusikia hasara bali faida. Je nikweli kulikuwa hakana hasara?? Walikuwa wanaficha kwa faida ya nani?? Je ndege ndiyo iliyokuwa kipaumbele cha Watz??

Nyimbo zilikuwa zinaimbwa za kuabudu na kusifu. Hakuna kukosoa wala kurekebisha. Na yeyote aliyejaribu kufanya hivyo aliishia kushambuliwa kwa matusi ya kila namna.
Sasa tatizo linakuja hao hao waliokuwa waimbaji wakubwa wa nyimbo zile ndio hivi sasa ni wakosoaji wakubwa wa utawala wa Jiwe. Je kwako wewe ni sahihi??
 
Hasara na upotevu huu unaotokana na taarifa za CAG ambapo wanasiasa waliochambua report ya CAG aliepita,Prof. Assad, waliibua utata wa matumizi ya shilling ya shilling trilioni 1.5 na hii ya hivi karibuni inatueleza hasara ya billion 150 katika uendeshaji wa ATCL.

Hasara na upotevu huu uliotokea chini ya utawala wa Magufuli, ni mbali na mamilion na mabilioni mengine yaliyopotea katika sekta za utalii, n.k kama inyoonyeshwa katika report ya CAG ya mwaka huu.

Bado hasara zinazotokana na serikali kufunguliwa makesi katika mahakama za usuluhishi za kimataifa bila kusahau hasara zilizotokana na siasa za hovyo za watu kujiuzulu kwa hoja ya kuunga mkono juhudi na kuliingiza Taifa gharama kubwa za mamilion kugharamia chaguzi ndogo.

Kwa kifupi, katika awamu ya Magufuli, Taifa limepata hasara kubwa Katika baadhi ya maeneo na pia kuna fedha nyingi zimetumika na kuacha utata mtupu kama hayo matumizi ya shilingi trilioni moja yaliyohojiwa na wabunge wa upinzani baada ya kuichambu report ya CAG aliepita(Prof.Assad).

Itakuwa ni jambo jema Bunge kuunda kamati teule kuchunguza utata wa matumizi haya ya shilingi trilioni 1.5 ili umma ujue ukweli ni upi na si hizi kelele za MATAGA kutaka kutuaminisha kuwa ufisadi ulidhibitiwa enzi za Hayati Magufuli tofauti na awamu zilizopita.

Kama hamtaki kuchunguza tuhuma hizi, acheni kumlinganisha Magufuli na watangulizi wake, hasa Kikwete, ambae wakati wake Bunge liliweze kuunda kamati teule na kuchunguza tuhuma zinazoihusu serikali, na pia vyombo vya habari viliweza kuanika kashifa mbalimbali za serikali bila kusahau Whistleblowers (kina Tumbili) waliweza kuanika madudu yaliyokuwa yanaendelea serikalini tofauti kabisa na ilivyokuwa wakati wa Magufuli .
Hivi zile za saccos alizokomba mwenyekiti zilikuwa million ngapi mkuu?.
 
usisahau kwamba kuna 29 bil imepigwa nje ya bajeti ya uchaguzi
 
Wazee wenu wanahangaika kupata viinua mgongo vyao kutoka mifuko ya pensheni, hospitali hazina madawa, vijana wenu waliomaliza vyuo hawana ajira, deni la taifa limefikia Trillion 18 kwa kipindi cha miaka 5 tu!
Ni bora hii hasara lakini watoto wetu wanasoma bure, barabara zimejengwa, tuna umeme hadi vijijini, madaraja yamejengwa, kuliko kipindi kile cha mzee wa msoga
 
Nikikumbuka ile kauli mafisadi serikali yangu hawana nafasi, na nchi yetu imechezewa sana na watu kumbe mwenda zake ndo mchwa wa nchi yetu dah R.I.P HAYATI JPM maana umeacha kila kitu hujazikwa na pesa wala daraja
 
Wazee wenu wanahangaika kupata viinua mgongo vyao kutoka mifuko ya pensheni, hospitali hazina madawa, vijana wenu waliomaliza vyuo hawana ajira, deni la taifa limefikia Trillion 18 kwa kipindi cha miaka 5 tu!
Acha matani trillion 18 miaka 5 ? Mbona tuliambiwa tunajenga miradi kwa pesa zetu za ndani cash kumbe mikopo.

Qmmke nilisha sema usiamini mwana siasa,
 
Back
Top Bottom