mcshonde
Member
- Jul 15, 2022
- 66
- 154
Elon Musk amedai kuwa ndani ya miezi sita ijayo Neuralink itakuwa tayari kuwekwa kwenye ubongo wa binadamu. Chip hii ambayo ni kama laini ya simu imeundwa ili iweze kuungana na utendaji kazi mzima wa ubongo kuanzia kumbukumbu n.k. Kupitia tukio aliloliita “show and tell” tajiri Musk ameongeza kuwa kwa miaka ijayo, chip hiyo itasaidia kurudisha uwezo wa kuona kwa vipofu.
Mwanzilishi msaidizi wa Neuralink, DJ Seo, amedai kuwa N1 chip ina chanel zaidi ya 1000 ambazo zina uwezo wa kurekodi na kucheza na kila kitu kinachoendelea kwenye ubongo wa mwanadamu.
Wanaopinga mpango huo ni pamoja na kamati ya pamoja ya dawa (PCRM) ambao wanadai kuwa chip hiyo imeonyesha kuwa ni hatari kwani hata nyani waliofanyiwa majaribio wapo waliozimia, waliopata maambukizi, kukosa nguvu, kushindwa kutembea n.k.
Zoezi la kutafuta watu watakaojitolea (volunteers) litaanza mapema baada ya mamlaka ya chakula na dawa (FDA) kuthibitisha kifaa hicho.