Chips zina nguvu kuliko ugali

Chips zina nguvu kuliko ugali

Anayoyasema mtoa mada ni sahihi lakini ugali una faida moja kubwa ni kwamba ugali unameng'enywa taratibu katika tumbo la mwanadamu hivyo inapelekea huyo binadamu aliekula ugali kuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa muda mrefu maana tumboni kitu kinapungua taratibu

Lakini chips zinameng'enywa haraka na baada ya muda kidogo aliekula chips atahisi njaa

Ndo maana miaka ya zamani mpaka leo huwezi pata bondia kutoka kagera,kipindi tunasoma zamani vijana wa kagera tulikuwa tunawapiga makwenzi sana kwasababu walikuwa hawana nguvu kutokana na kula ndizi
 
kinachowafanya watu wasingizie chips sio chakula chenye nguvu ni umasikini tu uliotujaa, mtu anapiga hesabu chips za 1500 ni sawa na gharama ugali wa unga robo na dagaa pembeni akila lazima ashibe ila hizo chips za 1500 akimaliza kama hakijatokea kitu.... Sasa hapo ndo unapata majibu kwamba kumbe ni gharama za kununua chips za kushiba ndo kubwa..... Mtu anaekula chips za 3000 kavu pembeni akaweka mishkaki 10 na kinywaji pembeni we wa unga robo utamshinda nguvu kivipi? Tafuteni hela muache kusingizia vyakula ndo havina nguvu.... Wenzetu wanakula Buggers,Pizzas, Chips na Mikuku tena Broillers ila still ukifanya uchunguzi bado wanatuzidi kila kitu.
 
Ugali wa mahindi unadumaza akili za kupunguza uwezo wa kufikiri. Kama una watoto nyumbani ifanye ngano kuwa chanzo kikuu cha chakula cha kuongeza nguvu kwa watoto wako na siyo ugali wa mahindi.
 
huku kamachumu tunatumia kama mboga, ugali pembeni chipsi pembeni

ila hoja yako nzuri
 
Afya sio kula chakula kingi au kujaza tumbo tu,unatakiwe ule balanced diet,sasa hata ukijaza tumbo,mwili utachukua only required amount of nutrients,it's all about food suppliments.
 
Bhagoooosha!!chips ni mboga tu kama ilivo dagaa!!....ugali samaki(sato,sangara,kambale),au maziwa sio haya ya mang'ombe ya kisasa,....huenda mleta uzi hujawah kula ugal ila unakulaga uji...ugali baba lao
 
Anayoyasema mtoa mada ni sahihi lakini ugali una faida moja kubwa ni kwamba ugali unameng'enywa taratibu katika tumbo la mwanadamu hivyo inapelekea huyo binadamu aliekula ugali kuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa muda mrefu maana tumboni kitu kinapungua taratibu

Lakini chips zinameng'enywa haraka na baada ya muda kidogo aliekula chips atahisi njaa

Ndo maana miaka ya zamani mpaka leo huwezi pata bondia kutoka kagera,kipindi tunasoma zamani vijana wa kagera tulikuwa tunawapiga makwenzi sana kwasababu walikuwa hawana nguvu kutokana na kula ndizi
Kwani kinachotakiwa ni chakula kinachokaa tumboni muda mrefu au chakula chenye nguvu?
Na chakula kisipomeng'enywa mwili haupati nguvu
 
Back
Top Bottom