Hata huko pia unawekeza, pesa yako inakufanyia kazi bila wewe kuwepo..!!
2020 hisa moja ya Nmb ilikua 2300 sasa hivi iko 13,900.
Kama ulikuwa na hisa 10,000 ambazo ulinunua kwa 2300 jumla uliwekeza million 23
Sasa hizo hisa 10,000 zidisha kwa 13,900
10,000x13,900=139,000,000
Umeona hapo uwekezaji unavyolipa?
Sasa ukiacha hiyo kuna gawio ambalo linatolewa kama faida na kampuni kila mwaka.
Jana wametangaza gawio la mwaka huu 610.15 haya tuzidishe
Hisa 10,000x610.15=6,101,500
Hiyo unaweza kuifanyia chochote unachotaka hata kujipongeza kufurahia ushindi wa team letu 😹😹😹
Sasa fikiria kama una hisa laki moja muda huu hilo shangwe lake linakuwaje??