Chochote kizuri nikimhusisha mama kinakufa

Kuna rafiki yangu nae ni hivyo hivyo nikamwambia mipango yangu tu lazima hiyo mipango ife, hata kama kesho yake ningekuwa na safari na tayari nshajiandaa halafu nikamwambia lazima hiyo safari ife,
Baada ya kugundua hilo Sahiv simwambii chochote

Hata mi nimegundua hivyo ukiwa na vitu usiwaambie watu kaa kimya tu
 

Unaweza simulia kidogo tukushauri usijekuwa unamsingizia
 
Somemtimes wazazi ukiwaonyesha mipango yako mizuri hawachelewi kwenda kuyatangaza kwa watu wengne eiza ndugu zak au mashoga zake ndo hapo wakati mwingine vipengele vinavyoanzia
Huu ndio ugomvi mkubwa na bi mkubwa wangu kila siku, wamama wa kiswahili ni shida sometimes, hawana vifua 😂
 
Siku umweleze kila kitu pengine kipo kitu kidogo cha kurekebisha.

Fanya akiwa hai akifa kabla hamjatengeneza itakuwa mbaya.

Mt 15:4

Kwa kuwa Mungu alisema, Mheshimu baba yako na mama yako, na Amtukanaye baba yake au mama yake kufa na afe.
 
Huyo mama ana nuksi.
Hayuko peke yake.
Kulikua na barmaid mmoja huku Kimara, aisee. Kila aliyemkula anapoteza kazi au biashara inakufa halafu alikua mzuri na kwa Ninyi mnao hisi uzuri wa mwanamke ni tako, nalo alikua nalo.
 
Unaweza simulia kidogo tukushauri usijekuwa unamsingizia
Yaani nimefuatilia tangu kipindi nasoma, siku nikimuambia tarehe ya mitihani huwa ananiambia ataniaombea, huo mtihani hata kama ni mrahisi lazima nifeli. Siku nisipomuambia nitafauli hata kama huo mtihani ni mgumu

Michongo mingi ya kitaa nikimshirikisha lazima iende tofauti.

Mwaka huu nimekuja kuhitimisha kwamba mawazo yangu ni sahihi baada ya kufanya jaribio hili; Nimemshirikisha kwamba nitaotesha alizeti ekari 2 kwenye shamba la nyumbani akaniunga mkono. Nikanunua mbegu ya alizeti inayotosha ekari 4 nikaotesha ekari mbili hapo nyumbani, then nikaotesha ekari 2 kwa siri kwenye shamba la kukodi hapo jirani na shamba letu. Cha ajabu ile ya shamba la nyumbani haikuota lakini ile niliyootesha kwa siri imeota yote na inaendeleanvizuri kabisa. Kumbuka haya mashamba yamekaribiana sana; jiografia ni moja na tabia ya nchi ni moja. Hapo ndipo ni kahakikisha kwamba mawazo yangu ya mda mrefu ni ya kweli.
 
Mhhhh,pamoja na hayo bado nakataa mama hana baya!Ebu uanze kusaliii sasa Mungu atakuonyesha ýote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…