Kundi la tatu la sampuli za majaribio ya sayansi ya anga za juu, ambalo lilirudishwa na chombo cha anga za juu cha Shenzhou 14 cha China, lilirejeshwa Beijing alfajiri ya tarehe 5. Sampuli zilizorejeshwa ni pamoja na vifurushi vitatu vya baridi vya sampuli za kibaiolojia na mfuko mmoja wa sampuli usio na kontena.
Miongoni mwao, sampuli tatu za vifurushi baridi vya sampuli za kibaolojia zilikuwa ni sampuli za majaribio za mpunga na Arabidopsis thaliana ambazo zimekua katika anga kwa siku 120, ni mara ya kwanza kwa mbegu za mpunga kupatikana katika obiti duniani. Kwa sasa, sehemu ya sampuli zilirejeshwa kwenye maabara ya Chuo cha Sayansi cha China ili kuendelea kulimwa.