Naanzia hapa,suala la budget waesema lini au umejiaje kama budget ni kubwa ? Umbali wa kwenda Mars na Mwezini unatofautiana vipi na changamoto ni zipi ? Bajeti hiyo ni kiasi gani wanayo
Kuna swali nilikuuliza wewe unahihikisha vipi ya kuwa kweli wameenda Mwezini au Mars ? Marejeo yako wewe ni yapi ? Hili swali hujalijibu. Kwamba je kwa kuona picha au kusikia habari ?
Hapa naona unawachoresha Wanasayansi na kuwafanya tuwaone wamebweteka. Kisayansi walitakiwa mpaka sasa hivi wawe wameshaenda zaidi ya mara kumi sababu ni zaidi ya miongo mitatu tangu tuambiwe Nail alikwenda mwezini. Maana yake walitakiwa wawe wameshabuni vifaa vyenyw ufanisi mkubwa na kwa gharama nafuu. Labda watuambie ya kuwa gharama imekuwa kubwa zaidi ya kuandaa movie kama hiyo, au wameshajua ya kuwa watu wameshawaona wao mazwazwa kwa kuigiza tukio hilo pale Area 51.
Lakini suala la uzandiki juu ya tukio la mwezini mbona limeshabatilishwa tangu zamani na husemwa pia sababu ya kifo cha John F. Kenedy ni kufichua siri au kutaka kufichua mbinu hiyo. Kihistoria husemwa ya kuwa hiyo ilikuwa ni vita baina ya USSR na Marekani katika kuonyeshana umwamba maendeleo ya kisayansi.
Mimi siyo kwamba nadhani bali nina uhakika kabisa.
Watuambie kwanza umbali wa kutoka katika uso wa dunia mpaka mwezini ni kiasi gani ? Bila kuweka Assumtions yoyote ile, wakiweka tu Assumptions wameharibu.
Pili, walitumia vigezo gani kutengeneza kifaa ambacho walijua fika kitawapeleka na kuwafikisha mwezini ? Hapa inabidi watuambie. Maana yake kabla inabidi ufanya ufanue utafiti, na utembelee sehemu husika. Tafiti hii ilifanyika wapi na kwa kutumia nini ?
Sasa unapohoji haya mambo ndipo unapoona ya kuwa hili ni igizo na wengine walithibitisha hilo.
Tatu, kiimani jambo hili hali wezekani, sababu hakuna anaejua ya kuwa Mwezi uko umbali gani toka mbingu ya kwanza ila kwa macho ukiangalia vizuri unaona ya kuwa mwezi uko karibu sana na mbingu ya kwanza kuliko ardhini, yaani duniani. Tunaambiwa umbali wa mbingu ya kwanza na dunia na mbingu na mbingu ni mwendo wa miaka 500. Hii ni kwa mwendo kasi wa juu zaidi (Rejea jaya katika kitabu kiitwacho "Qamus al Bida'ah" ). Maana chini ya muda huo hizo zinabaki kuwa stori tu na kufurahisha nafsi.
Tatu, zipo sababu za kisayansi zinazo pinga igizo hilo. Unaweza kuzifatilia Google ukazipata. Ukisearch "Did we land on the moon". Utaona mambo mengi wapo wanao thibitisha ya kuwa tukio hilo ni kweli na wale wanao kadhibisha tukio hilo, ukipima katika mzani utaona ya luwa hawa wapili wana hoja zenye nguvu mno kuliko wengin, na hao wa kwanza wameanza kuja kuandika hayo hivi karibuni.
Narudi kuendelea hapa nilipoishia...