Media ipe mtazamo uliochanganywa na akili zako mwenyewe, usimeze kila kitu. Hakuna media bora ila kuna zenye unafuu kuliko nyingine. Wewe fuatilia zote ila ujue kuchuja, kama ni habari inahusu China jiulize ni habari mbaya au nzuri kisha jiulize chombo kilichoitoa kina affiliation na China au hakina. China Daily, People's Daily, Global Times, CCTV4, CGNT, South China Morning Post, etc hivyo ni vyombo vya China haviwezi isemea vibaya. Ukisoma taarifa zake linganisha na taarifa za vyombo vingine ila zingatia nchi marafiki wa China na nchi adui wa China.
Mfano Urusi ni rafiki wa China ila usitarajie taarifa njema ya China kutengeneza jet engine yenye ubora zaidi itaifurahisha Urusi ambayo inategemewa na China kwenye hiyo teknolojia. So hapo chombo cha China kikisema engine iko vizuri, na vyombo vya Ulaya vikasema hata vya Urusi vikiponda ujue iko vizuri.
Hata kwa Urusi Sputnik, Zvezda, RT, RIA Novosti zikisema kitu chuja vilevile. Wakiisema vibaya Uingereza, na Aljazeera ikaisema vibaya, na Fox News hapo ni sawa. Ila sio Sputnik ishangilie Waziri Mkuu wa Uingereza kujiuzuru iseme alikuwa mbovu, na anayekuja itamchukia, na aliyetangulia, na atakayefuata tena ambaye bado hatumjui.
Aljazeera watakuwa neutral kuliko vyombo vingi vya Kiarabu ila juu ya Israel watapotosha na juu ya Saudi Arabia wanaponda sana na kukuza mambo. Waandishi wa habari wa Aljazeera kadhaa wameuwawa na Israel wakiwa na silaha na mjumuiko wa makundi ila utasikia Aljazeera inawaita waandishi wake. Sasa mwandishi aliyevaa kiraia na bunduki akiwa kwenye handaki wapi na wapi. Akiuwawa mwandishi amevaa PRESS, helmet na lile vazi la blue hapo ndio kosa.