Black Butterfly
Senior Member
- Aug 31, 2022
- 130
- 368
Kwa takriban mwezi sasa Polisi bado wanahangaika na uchunguzi wa tukio la Binti aliyeonekana katika Video akifanyiwa vitendo vya Ukatili na Wanaume Watano na bado kumekuwa na kauli za kutia shaka kuhusu haki ya huyo binti. Baadhi ya Askari wamekuwa wakitoa kauli zinazoonesha wazi kumkandamiza huyo Binti.
Lakini kuchelewa kupelekwa Mahakamani kwa Jalada la Uchunguzi wa tukio hilo kunazidi kuibua sintofahamu wakati tangu Agosti 9, 2024 Polisi walisema uchunguzi umekamilika sasa nini kinachelewesha kufikishwa Mahakani watuhumiwa waliokamatwa?
Hili jambo hadi sasa linahitaji Uchunguzu wa Tume Huru itakayoundwa kutoka nje ya Jeshi la Polisi na Vyombo vingine ambavyo baadhi vimeonekana kulinda au kuwaficha wahusika. Ikumbukwe tayari inasemekana mmoja waliowatuma wabakaji ni Afande. Sasa hali hiyo tu inaingiza mgangano wa kumaslahi.
Kama wananchi wenye uchungu na haki zetu tunaomba Uchunguzi wa Vyombo huru katika suala hili ili tuwe na amani ya matokeo. Bila hivyo tutapata wasiwasi kwa kulinganisha na matukio mengine ambayo polisi wamekuwa wakichunguza laki ni hakuna matokeo ya kueleweka yanayokuja.