mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Ninaomba nieleweke. Ushauri wa kwanza kabisa wa kamati ya corona ni kwamba SERIKALI ITANGAZE UWEPO WA CORONA. Kwa maneno mengine serikali IKIRI (kwa kinywa chake) uwepo wa corona! Anayeshauri hivyo tayari amevaa barakoa! Hivi tukimwuliza ni kwa nini amevaa barakoa atasemaje?
Kwa nini inatakiwa serikali ikiri kwa kinywa cha RAIS au kwa TAMKO rasmi la serikali kutoka IKULU kuwa Tanzania kuna corona? Ni kwa sababu kinywa cha Rais ni mlango wa kufungulia vitu au kuvifungia vitu katika ulimwengu wa roho visiingie au visiingie katika Taifa lolote lile. Acha yeyote yule aseme (kama ambavyo wameshasema sana) kuhusu corona nchini kwetu lakini bado maadamu Rais aliyepita alishaKIRI hadharani kuwa Mungu ametuponya na corona, tangu wakati huo roho ya mauti nyuma ya corona haina NGUVU kabisa ya kulivamia Taifa letu. Hiyo ndiyo SIRI kwa nini kama Taifa tuko salama sana.
Shetani na mawakala wake wanajua hivyo na wanatafuta kwa nguvu zote mlango wa kuingia Tanzania. Chonde chonde Mama USITAMKE HILO wala kutoa WARAKA RASMI wa KUKIRI UWEPO wa corona Tanzania. Acha wengine wote waseme (kama ambavyo wamesema sana), lakini wewe ENDELEA KUKIRI UPONYAJI NA ULINZI WA MUNGU kwa Taifa letu bila kuyumbishwa na hali yoyote inavyoonekana wala kuyumbishwa na maneno ya yeyote yule ndani na nje ya nchi.
Kwa kufanya hivyo utaiokoa Tanzania uliyopewa na MUNGU uiongoze. Anayetaka kujilinda na corona na afanye hivyo kwa namna yoyote atakayoona ni vema. Kinywa cha RAIS kiendelee KUKIRI uponyaji na ulinzi wa Ki-Mungu dhidi ya corona. Hapo corona HAITAKUWA NA NGUVU nchini mwetu KABISA. Pendekezo la kwanza LISITEKELEZWE. Kwa sababu siku likitekelezwa, nguvu za giza nyuma ya corona zitaivamia nchi yetu na kuwasha moto wa corona ambao HAUWEZI KUZIMWA kwa LOCKDOWN, BARAKOA wala CHANJO.
Hizo nchi zinazoteseka kwa corona zimefanya hayo yote yanayopendekezwa kwetu na hayajawasaidia! INDIA wanatengeneza barakoa na chanjo na wameweka lockdown ya nguvu lakini corona bado inawatesa. Tofauti ya Tanzania na mataifa mengine yote ni kwamba sisi TULIMTANGULIZA MUNGU MBELE na tahadhali zingine zikafuata nyuma. Wao walitanguliza tahadhali na Mungu hakupewa nafasi ya kwanza! Tanzania tukifanya makosa tutakuwa wageni wa nani? BIBLIA inasema KIFO na MAUTI ziko katika uwezo wa ulimi.
Watanzania tumwombee SANA Rais wetu, VITA vyake ni vikubwa mno. Tusipomwombea, tusije tukamlaumu, maana bila Mungu kumsaidia hataweza. Walio wa rohoni wamenielewa vizuri sana. Tuendelee kuiombea nchi yetu na kumwombea Rais wetu kwa moyo wote.