Chonde chonde Mh. Faustine Ndugulile tunaomba uturudishe Misri tu,sio kwa kipigo hiki kwenye vifurushi

Sasa huyu Dr Faustine Ndugulile alivyokuwa anashupalia shingo kwamba makampuni ya simu yapunguze bei hadi sijui Tsh 9 ndio wamepunguza hapo? Ndio maana watu walisema serikali itapandisha bei kwa ajili ya watu wanatumia sana Whatsapp hivyo hawapigi simu za nje za kawaida na hivyo serkali inapoteza zaidi ya bilioni 20,haya ndio matokeo yake wameamua kuzirudisha kwa kuongeza gharama za MB.
 
Ndugulile nadhani alifanya hayo wakati wa awamu ya 5,naona anataka kusaidiwa na tisiara ei yake
 
Kibosho1 nimeona miss call ya mke wako amekupigia mara 2 lkn upokei
 
Na bado..

Hello, to continue providing you with quality services, we shall review our bundles on 02/04/2021. Continue enjoy exciting offers from Super Network. T&C Apply.
 
Screenshoot fanya ufute kuna namba ya shemeji hapo asije kusumbuliwa.
 
Mimi alichonishangaza ni kuweka bei elekezi ya chini wakati kwa mtazamo wangu hasa kwenye ushindani wa biashara Serikali ingestahili kuweka bei elekezi ya juu (Kikomo)
Ila Bei ya chini inayaachia mashirika yashindane...
Sasa kama yote yatakuwa na bei sawa na mtandao wa uhakika (simu na internet) ambapo ndio jukumu la msingi la mtoa huduma wa mawasiliano; kulikuwa na haja gani ya kusajili makampuni mengi ambayo hayashindani?
 
Makabwela bana. Yani iyo mnaona nyingiiiii. Ndo hivyo tena mlipangiwa kuwa na hali ngumu pindi tu mlipozaliwa.
 
Huko tunapo elekea serikali itaingilia mpaka mahusiano yetu ya mapenzi. Si kwa kiherehere hichi cha kujihusisha na kila kitu, na hayajifunzi haya majitu wala hayapati akili.

Yaliingilia korosho yakaharibu soko, yakaingilia dengu na kunde na kwenyewe yakaharibu soko. Sasa yameingia kwenye mitandao ya simu.
 
Kwani watanzania tumeikosea Nini hii serikali? Kura wanaomba kwetu Ila wakishachaguliwa wanaeafaidisha MABEBERU. Ndugulile, VodaCom ndio mjumbe aliye kuchagua au ndie kakupigia Kura?
Tutaonana 2025
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…