Sina uhakika kama hao vijana wote hawajawahi kutumia mitandao ya jamii na hawajawahi kusikia kitu kinachoitwa Alliance in Motion Global.
Hizi habari zimetapakaa humu JF na mitandao mingine pamoja na ndugu zake Qnet(aliyeingia zamani), Forever living n.k
Kule Moshi tulisikia Alliance walipigwa marufuku na kuamriwa kuwalipa vijana waliowatapeli. Iweje huko Kahama habari hizo hazijawahi kufika?
Hata hivyo natambua ugumu wa kuchakarika na endapo ukielezwa namna ya kutusua haraka hapo lazima useme dodo chini ya mwembe hili hapa.
Kwa kuwaokoa, anza wewe kuwaelimisha wachache unaowajua ambao bado hawajatapeliwa kabla mamlaka za serikali hazijachukua hatua kuwasaidia.
Pia unadai wanatumia majengo ya serikali kuendeshea ushawishi wao, hapo wamewalipa hao hao viongozi unaowataka watoe msaada kuwanusuru. Ni ishu nyingine pia!