BongoTz
JF-Expert Member
- Nov 3, 2006
- 272
- 3
Ingawa tunajua kwamba nchi yetu bado ni changa kwa siasa za vyama vingi kutokana na ufinyu wa elimu ya uraia waliyonayo watanzania walio wengi hususani sehemu za vijijini, lakini pia, uroho wa madaraka wa baadhi ya viongozi wa vyama vya Mageuzi umechangia kwa kiwango kikubwa kwa chama tawala kuendelea kuviburuza vyama hivyo katika kila chaguzi zilizowahi kufanyika--ukianza na ule wa mwaka 1995, 2000 na 2005. Na wasiwasi wangu mkumbwa ni kwamba, matokeo ya mwaka huu yatafanana na yale ya miaka ya nyuma kama wanamageuzi watashindwa kuunganisha nguvu mwaka huu ili kuing'oa CCM.
Mtu yeyote mwenye akili timamu atakaa na kufikiri kuwa baada ya mageuzi kufanya vibaya katika chaguzi zote tatu zilizopita, upinzani ungekaa pamoja na kufikia uamuzi wa pamoja wa kuandaa mikakati kabambe ya kukabili uchaguzi wa 2010. Lakini badala yake, bado kila chama kinadhani kuwa kina ubavu wa kutosha kupambana na CCM ambayo imekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 49 (ukiunganisha na miaka ya TANU).
Watanzania walio wengi wangependa kuona vyama vya upinzani vikiungana au hata kushirikiana ili kukiondoa chama kinachotawala madarakani. Lakini kutokana na uroho wa madaraka wa baadhi ya viongozi wachache wa upinzani hilo linaweza lisitokee tena kwenye uchaguzi wa mwaka huu kwani kila dalili zinaashiria kuwa huenda tena vyama vya Mageuzi vitarudia makosa yaleyale (kwa Kila chama kuamua kuingia kivyakevyake) kwa matumaini bandia kuwa huenda pengine muujiza utatokea na hivyo kuwashindisha viti vingi vya ubunge na hata kuwaweka ikulu.
Umefikia wakati sasa kwa vyama vya Mageuzi nchini kuachana na ndoto za mchana na kutambua kuwa mfumo wowote ule wa vyama vingi unahuishwa na uimara na uthabiti wa vyama hivyo ambavyo vinakuwa tayari kuchukua fursa za kuongoza nchi kama chama tawala kikidorora. Wakishatambua hilo, basi waache kabisa kulalamika eti chama tawala kinatumia dola kuwatisha na kuwamaliza nguvu; na badala yake waunganishe nguvu kama wanataka kuwa na nafasi ya kukishinda chama tawala kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Sambamba na hilo, vyama vyote vya Mageuzi nchini vikae pamoja na kuandaa mbinu za kukabiliana na nadharia ambayo chama tawala kimefanikiwa kupandikiza vichwani mwa watanzania kwa muda mrefu sasa. Nadharia kuwa, "Mageuzi ni upinzani." Semina ziendeshwe nchini kote kuelimisha wananchi kuwa Mageuzi sio upinzani, bali Mageuzi ni mbadala wa chama fulani kuiongoza nchi pale chama kilichopo madarakani kinapokuwa kimedorora. Mabango yenye sera-mbadala yabandikwe sehemu zenye mikusanyiko ya watu wengi kuainisha mapungufu ya chama tawala na kutoa mbadala toka Mageuzi. Pia matangazo kwa njia ya Radio na Runinga yatumike kueneza kampeni ya kuzima nadharia kuwa "Mageuzi ni upinzani." Vyama vya mageuzi vina wasomi wengi, tunaamini kabisa hawawezi kushindwa kulielezea jambo hili kwa ufasaha zaidi.
Pia, vyama vya Mageuzi vitafute njia nzuri ya kuelimisha wafuasi wao kuhusu umuhimu wa kura hata kama ni kura moja. Ukweli ni kwamba: ufinyu wa elimu ya uraia kwa wanachama wengi wa vyama vya upinzani [Mageuzi] umechangia kwa kiwango fulani kuvikosesha vyama hivyo kura halali tena nyingi tu katika chaguzi nyingi zilizopita. Mfano, wadadisi wa mambo ya kisiasa wanadai kuwa wananchama wengi wa chama cha CUF waliongozwa na jazba zaidi kuliko hekima katika uchaguzi mkuu wa 2005 na badala ya kupiga kura ya "HAPANA" kwa mgombea wasiyemtaka, wengi wao waliishia kuandika matusi na maneno ya kejeli mbele ya picha za mgombea wa chama tawala. Matokeo yake: kura hizo zilihesabiwa kama zimeheharibika.
Kadhalika, badala ya kupoteza muda mwingi kutoa malalamishi mengi yasiyo na msingi dhidi ya chama tawala, vyama vya Mageuzi vinatakiwa kuweka sera za kueleweka mahala pake. Malalamiko tunayoyasikia kila siku toka upande wa Mageuzi kuwa: "oh, CCM ni wala rushwa..., CCM haijafanya lolote lile kwa kipindi chote chote ilipokuwa madarakani...blah blah blah..." hayawaingii wananchi maskioni kabisa endapo kama malalamishi hayo hayaambatanishwi na sera-mbadala zinazo onyesha kuwa ni nini tofauti ambacho Mageuzi wangefanya kama wao ndio wangekuwa madarakani. Kinachotakiwa sio kelele na lawama tu dhidi ya chama tawala, bali ni sera za kueleweka zenye makusudi ya kulichukua taifa letu kwenda hatua nyingine, hatua iliyo bora zaidi.
Kimsingi, ili vyama vya Mageuzi viwe na nafasi ya kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ni vema wahakikishe kuwa wanasimamisha mgombea mmoja (kiti cha urais) chini ya kivuli cha chama kimoja cha mageuzi chenye nguvu na mvuto mkubwa kwa wananchi. Kwasababu, hata kama mgombea watakayemsimamisha atakuwa hovyo, bado atabebwa na kuchachaguliwa kwa sababu tu ya nguvu na mvuto wa chama atakachowakilisha. Lakini kama Mageuzi watashindwa kufanya marekebisho haya mapema, basi wakae wakijua kuwa chama tawala kitaendelea kushinda na kuisabaratisha ngome ya Mageuzi tena na tena na tena...
P.S. Mimi si mwanachama wa chama chochote. Ila ningependa kuona ushindani wa kweli kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania!