Good point, mkuu!
Mkuu, if I may ask, ni hatua gani za machungu unazotaka Tanzania izipitie kwanza ndipo tujue kuwa mageuzi/upinzani wa kweli sasa umezaliwa nchini, officially? Hebu fafanua hiyo hoja kirefu...[do you mind to enlighten me here..., please...?]
Mkuu wangu shukran sana kunipa nafasi ya kujieleza kwani kidogo naona kama hukunielewa..
Swala sio machungu gani na hatua gani tuzipitie, kwani machungu hayana hatua zakupitia.. ila machungu ndio kiamsho cha sababu ya mageuzi/Upinzani popote pale na ktk mifumo miwili tofauti ya kiutawala.
Mfumo wa kwanza ni ule wa Demokrasia ambao itikadi fulani inayotawala ndio imesababisha machungu wanayopata wananchi wake hivyo kuzua fikra mpya za mageuzi/Upinzani..Nikasema mfumo huu haupo ktk nchi za Kiafrika Upo Ulaya na hautakuwepo kwetu sisi kesho wala kesho kutwa kwa sababu sisi hatukupitia hatua za kuzaliwa kwa demokrasia yaani Upinzani wa Itikadi (Siasa) ila tumepitia Upinzani wa mfumo wa pili..
Mfumo wa pili ni ule wa mtawala kupitia chama kuongoza nchi na kuwaletea wananchi wake machungu, hivyo machungu yao hutokana na utawala dhalimu wa kiongozi au utawala uliopo madarakani. Hii ndio hali halisi ya nchi za Kiafrika na sisi Tanzania hatuna tofauti yeyote pamoja na kwamba tumeuziwa demokrasia kama chakula cha makopo tunachonunua supermarket kutokea Ulaya.
Ukweli utabakia kwamba sisi tunachopingana nacho ni mtawala au kundi la watu wanaotuongoza pasipo kutumia itikadi yoyote ila matakwa yao binafsi. Hakuna mtu anayeweza nambia JK anatumia itikadi gani wala mtu anayeweza kunambia Dr.Slaa anapingana na itikadi gani kwani sera zote na ahadi zao hazihusiani na itikadi zaidi ya kuzungumzia siasa za kanyaga twende..
Kwa hiyo machungu yetu yote yanatokana na Utawala bora, hivyo hatua za mageuzi zitatokana na kupinga utawala uliopo na sio kuzungumzia siasa ambazo ni pandikizi kwetu. Machungu yetu yote yanatokana na Uongozi mbaya sio siasa mbaya hata kidogo kwani hatuna siasa (itikadi)..
Kama tulivyopigania Uhuru hakika haikuwa kuondokana na Ubepari bali Kutwaliwa na Muingereza. halikuwa swala la kiitikadi sisi kudai Uhuru wetu bali kuondokana na utawala dhalimu wa mkoloni na ushindi wa TANU ulitokana na wananchi kuelewa kwamba machungu yanatokana na kutawaliwa hivyo wananchi walielekeza hatua zote za mageuzi/Upinzani kupingana na kutawaliwa (Colonialism) na ndipo tulipoweza kupata ushindi dhidi ya kutawaliwa.
Na ndio maana unaona watu wote hapa hasira zao ni Kikwete, hasira zao kwa CCM ni toka Mkapa hadi kundi zima la Mtandao ambao hawawakilishi itikadi yyoyote ila nafsi zao..Hawa ndio sababu na machungu yote ya wananchi kukosa maisha bora..Ni kutokana na machungu ya kukosa maisha bora ndio hatua tunazotakiwa dhidi ya ahadi zao
Ish, mkuu!! You are know frightening the hell out of me! Hawa watu wote uliowataja hapo juu wameingia madarakani kwa kumwaga damu. Do you mean to tell me kwamba bila kumwaga damu, Tanzania itabakia kuwa kichwa cha mwendawazimu...? Ama unamaanisha nini kwa hilo...?
Hapana mkuu wangu nilichofanya ni kuelezea Uzuri na Ubaya wa viongozi kuongoza mageuzi/Upinzani na sii siasa za chama chao kuwa sababu za machungu ya wananchi..Mapenzi au upinzani dhidi ya Idd Amin au Mseveni unatokana na Utawala wao sio siasa au itikadi.. Kwetu sisi CCM imekuwa ni kama mtu kiongozi ambaye kawaletea machungu wananchi na sii siasa (itikadi) za chama hicho.
Ah, udhanni ni sababu zipi hizo...? Hebu tutajie...?
Hakuna mtu anayepinga CCM kwa sababu ya itikadi zake walka hakuna mtu anayepinga Chadema kwa sababu ya itikadi zake ila tunapinga vyama vyote kutokana na viongozi wao waliosimamishwa. CCM na Chadema vimesimama kama WATU badala ya chama kuwakilisha Upinzani.