Bila shaka hili tumelizungumza siku nyingi sana hapa JF.. Kilichotakiwa ni Nyerere kukiua kwanza chama CCM na kuanzisha makundi ya vyama kutokana na Itikadi ndani ya CCM yenyewe.. Sasa maadam Nyerere hakufanya hivyo kama inatakiwa tuanzishe vyama kutokana na Itikadi lazima CCM ife kwanza jambo ambalo haliwezekani, lakini pia tutakuwa na muda mrefu sana kujifunza kuelewa tofauti ya itikadi pasipo kujua mazuri na madhara ya kila itikadi ktk maisha yetu.. Ndio maana husisitiza zaidi kufikiria kitu kinachotokana na WATU na MAZINGIRA ya wahusika.
Hao tunaowaiga wana Mtawala wa Kimalkia ambaye hahusiki kabisa na Siasa. Wenzetu wamepitia hatua za kupinga utawala wa mtu mmoja au kundi la watu hivyo kubuni falsafa pinzani ya udhia huo na kiongozi huja na vision yake wakati sisi Mtawala ndiye mwenye fikra pasipo vision hivyo kuwafanya watawala wenye ambition..
Hivyo bado tunaweza mchagua mtu, na pengine ktk hatua hizi na kupinga mtu tutakuja fikia upinzani wa kifikra kuliko kujaribu kutumia itikadi kama sababu ya Upinzani hali hakuna kitu kama hicho..