Elections 2010 Chonde chonde Slaa/Chadema, unganeni na wanamageuzi wenzako

Mkuu BongoTz ukiondoa uzandiki kidooogo point zako zitakuwa na Mantiki sana.

Umeeleza namna Al Gore na Democrat walivyokataa kum accomodate Nader lakini unashindwa kuoanisha hoja yako kwa kushindwa kuonesha ni vipi CHADEMA imekataa kum accomate Lipumba, yaani unataka uaminishe watu kwamba Lipumba aliomba Shavu CHADEMA akatoswa
 
Bongo Tz,

Nadhani wewe ni mgeni kwenye siasa.

Sio vyama vyote "vya upinzani" ni vyama vya upinzani. Kuna baadhi ambavyo ni pandikizi. Vina viongozi ambao ni WANACHAMA HAI wa CCM. Chunguza kwa makini kauli zao. Wengi wao wanawaponda wanamapinduzi wenzao, kwenye majimbo ambayo wenzao wanakubalika, wao wanaweka wagombea kwenda kuvuruga kampeni na kuwapunguzia wenzao kura zao.

Baadhi ya vyama hivi ambavyo SI VYA UPINZANI ni TLP na NCCR-Mageuzi.

Marando hakuondoka NCCR-Mageuzi kuhamia CHADEMA bila kulitambua hili.

Orodha nyingine ya vyama pandikizi?

SAU, APPT-Maendeleo, UPDP, DP.... niendelee?

Unapowalaumu CHADEMA, kumbuka kwamba wao hawawezi kwenda kuvuruga mikakati yao ya KUIKOMBOA Tanzania kwa kushirikiana na MAMLUKI hawa! Waungane nao ili WAANGAMIE?

Tuambie kingine, SIO HIKI!

2010 HATUDANGANYIKI

-> Mwana wa Haki

P.S. Au na wewe ni MAMLUKI?
 

That's one good analysis there, Mzuvendi. I agree.
 


Unaota au ni matamanio yako kwamba CHADEMA isishinde?

Jaribu kwenda kuongea na hao maskini, kule Ileje, Mwanjelwa, Makete, Dongobesh na kwingineko... kama utafanikiwa! LOL
 

Totally agree with ya buddy! I think that's one of the big reasons behind this 'go alone' mentality. Ulaji, ruzuku, ruzuku, ulaji. Period.
 
tatizo la vyama vya Upinzani ni kwamba kila mmoja wao anataka kushika Usukani.. hakuna chama kinachokubali kwamba Dr.Slaa anaweza kushinda au kuwapa viti vya Ubunge hivyo ni bora kila chama kisimame peke yake kwa sababu ya Ruzuku...
Mkuu, nakubalina na wewe 100% kabisa. But it's kinda sad kwamba vyama vya mageuzi vimechagua kuweka ruzuku mbele badala ya maslahi ya taifa. Anyhoo, it is what it is, mkuu.

Well, lakini hii hofu itaendelea hadi lini...?
 

Mkuu, kuna mtu aliniuliza kuwa kwanini vyama ambavyo haviko strong visiungane na Chadema, na mimi nimetoa mfano wa Gore na Nader kuonyesha kuwa wakati mwingine chama kilicho strong ndicho chenye hatihati ya kupoteza zaidi (lose more). It was just an example. That's all.
 

Nimekusoma mkuu
So mimi ninawaomba Chadema waangalie watakachopoteza kwa kukataa kuungana na vyama vingine

Tuendelee kukata ishu
 
Mkuu, nakubalina na wewe 100% kabisa. But it's kinda sad kwamba vyama vya mageuzi vimechagua kuweka ruzuku mbele badala ya maslahi ya taifa. Anyhoo, it is what it is, mkuu.


Well, lakini hii hofu itaendelea hadi lini...?
Hofu hii itabakia ktk vyama lakini sisi wananchi tuna jukumu letu..Kumchagua kiongozi anayeweza kutuongoza. Binafsi siamini demokrasia inaweza kuwepo Afrika pasipo nchi zetu kupitia hatua zilizosababisha kuwepo kwa Demokrasia kwani upinzani wowote wa fikra hutokana itikadi na sio Utawala dhalimu ulokuwepo..tofauti na demokrasia ambayo hupinga itikadi inayotumika kuongoza sisi huanza na mtu au kundi la watu against Kiongozi au Utawala uliopo hadi upinzani huo kuwafikia wananchi kuzua Mapinduzi au madai ya changes za mtawala sii itikadi..

Hizi habari za kuanzisha Upinzani pasipo kupitia hatua za machungu na Upinzani wa itikadi fulani, ili mradi tu tumeingiza demokrasia ili kuwafurahisha IMF ni sawa na mtu kuzaliwa ktk dini na usifanye ibada ila kuwafurahisha wazazi. Uzawa huu hauwezi kuleta maana ya Upinzani zaidi ya vyama hivi kufikiria Ruzuku zaidi na kuuza sura.

Nchi zote za kiafrika mafanikio ya changes hazikuanza na vyama kuungana ama Itikadi bali Upinzani dhidi ya kiongozi aliye madarakani. Hizi ndio siasa za nchi za kiafrika only one leader can change everything tumeyaona haya toka enzi za Idd Amin, Samwel Doe, Kagame, Museveni na viongozi karibu wote nchi za Kiafrika umaarufu wao umetokana na upinzani dhidi ya kiongozi aliyetangulia au Ubaya wao umetokana na wao wenyewe na sii chama kwa ujumla..

Kwa hiyo wakati wao wanashindwa kuungana na hakuna dalili zozote watafikia kuungana kwa sababu Tanzania hatukupitia sababu zozote za kuunda Upinzani wa kifikra isipokuwa tuna Upinzani wa sura. Hivyo ni juu yetu sisi wananchi kumchagua mtu mwenye uwezo badala ya kuchagua sura, utamaduni tuloachiwa na Mwalimu.
Ndio maana mimi nimechamgua Dr.Slaa..
 


Mbona hutaki kuzungumzia tabia ya CCM kuiba kura? Hata wakiungana ndiyo kura sasa hazitachakachuliwa?

Mbona umetumia muda mwingi kuongea matope ndugu yangu?
 
Good point, mkuu!

Mkuu, if I may ask, ni hatua gani za machungu unazotaka Tanzania izipitie kwanza ndipo tujue kuwa mageuzi/upinzani wa kweli sasa umezaliwa nchini, officially? Hebu fafanua hiyo hoja kirefu...[do you mind to enlighten me here..., please...?]

Ish, mkuu!! You are know frightening the hell out of me! Hawa watu wote uliowataja hapo juu wameingia madarakani kwa kumwaga damu. Do you mean to tell me kwamba bila kumwaga damu, Tanzania itabakia kuwa kichwa cha mwendawazimu...? Ama unamaanisha nini kwa hilo...?

Ah, unadhani ni sababu zipi hizo...? Hebu tutajie...?
 
Mbona hutaki kuzungumzia tabia ya CCM kuiba kura? Hata wakiungana ndiyo kura sasa hazitachakachuliwa?

Mbona umetumia muda mwingi kuongea matope ndugu yangu?
Well, tatizo la wizi wa kura halipo Tanzania peke yake. Lipi hata nchi za dunia ya kwanza. Hapa wananchi na vyama vya mageuzi ndo wanatakiwa kuwa makini zaidi kuhakikisha kuwa wizi hautokei... na hata kama unatokea, basi uwe katika kiwango cha chini. Uchaguzi mdogo katika jimbo la Tarime mwaka 2008, ni mfano mzuri kabisa wa kutizamwa.
 

Mkandara;
Umekosea, ni uongo; hakuna kitu kama hicho. Kwa mujibu wa sheria, kila chama hujitafutia rasilimali zake kwa ajili ya kugharamia kampeni za uchaguzi. Na hii inabainishwa na sheria ya Gharama za Uchaguzi.
Sawasawa?
 
Mkuu wangu shukran sana kunipa nafasi ya kujieleza kwani kidogo naona kama hukunielewa..
Swala sio machungu gani na hatua gani tuzipitie, kwani machungu hayana hatua zakupitia.. ila machungu ndio kiamsho cha sababu ya mageuzi/Upinzani popote pale na ktk mifumo miwili tofauti ya kiutawala.

Mfumo wa kwanza ni ule wa Demokrasia ambao itikadi fulani inayotawala ndio imesababisha machungu wanayopata wananchi wake hivyo kuzua fikra mpya za mageuzi/Upinzani..Nikasema mfumo huu haupo ktk nchi za Kiafrika Upo Ulaya na hautakuwepo kwetu sisi kesho wala kesho kutwa kwa sababu sisi hatukupitia hatua za kuzaliwa kwa demokrasia yaani Upinzani wa Itikadi (Siasa) ila tumepitia Upinzani wa mfumo wa pili..

Mfumo wa pili ni ule wa mtawala kupitia chama kuongoza nchi na kuwaletea wananchi wake machungu, hivyo machungu yao hutokana na utawala dhalimu wa kiongozi au utawala uliopo madarakani. Hii ndio hali halisi ya nchi za Kiafrika na sisi Tanzania hatuna tofauti yeyote pamoja na kwamba tumeuziwa demokrasia kama chakula cha makopo tunachonunua supermarket kutokea Ulaya.

Ukweli utabakia kwamba sisi tunachopingana nacho ni mtawala au kundi la watu wanaotuongoza pasipo kutumia itikadi yoyote ila matakwa yao binafsi. Hakuna mtu anayeweza nambia JK anatumia itikadi gani wala mtu anayeweza kunambia Dr.Slaa anapingana na itikadi gani kwani sera zote na ahadi zao hazihusiani na itikadi zaidi ya kuzungumzia siasa za kanyaga twende..

Kwa hiyo machungu yetu yote yanatokana na Utawala bora, hivyo hatua za mageuzi zitatokana na kupinga utawala uliopo na sio kuzungumzia siasa ambazo ni pandikizi kwetu. Machungu yetu yote yanatokana na Uongozi mbaya sio siasa mbaya hata kidogo kwani hatuna siasa (itikadi)..
Kama tulivyopigania Uhuru hakika haikuwa kuondokana na Ubepari bali Kutwaliwa na Muingereza. halikuwa swala la kiitikadi sisi kudai Uhuru wetu bali kuondokana na utawala dhalimu wa mkoloni na ushindi wa TANU ulitokana na wananchi kuelewa kwamba machungu yanatokana na kutawaliwa hivyo wananchi walielekeza hatua zote za mageuzi/Upinzani kupingana na kutawaliwa (Colonialism) na ndipo tulipoweza kupata ushindi dhidi ya kutawaliwa.

Na ndio maana unaona watu wote hapa hasira zao ni Kikwete, hasira zao kwa CCM ni toka Mkapa hadi kundi zima la Mtandao ambao hawawakilishi itikadi yyoyote ila nafsi zao..Hawa ndio sababu na machungu yote ya wananchi kukosa maisha bora..Ni kutokana na machungu ya kukosa maisha bora ndio hatua tunazotakiwa dhidi ya ahadi zao Hapana mkuu wangu nilichofanya ni kuelezea Uzuri na Ubaya wa viongozi kuongoza mageuzi/Upinzani na sii siasa za chama chao kuwa sababu za machungu ya wananchi..Mapenzi au upinzani dhidi ya Idd Amin au Mseveni unatokana na Utawala wao sio siasa au itikadi.. Kwetu sisi CCM imekuwa ni kama mtu kiongozi ambaye kawaletea machungu wananchi na sii siasa (itikadi) za chama hicho.
Ah, udhanni ni sababu zipi hizo...? Hebu tutajie...?
Hakuna mtu anayepinga CCM kwa sababu ya itikadi zake walka hakuna mtu anayepinga Chadema kwa sababu ya itikadi zake ila tunapinga vyama vyote kutokana na viongozi wao waliosimamishwa. CCM na Chadema vimesimama kama WATU badala ya chama kuwakilisha Upinzani.
 
mobuto seseko alianzisha vyama vya upinzani 45 akavisajili na kuvilea, ili viwe vinampinga yeye katika chama tawala, teh! teh!
 
Mkandara;
Umekosea, ni uongo; hakuna kitu kama hicho. Kwa mujibu wa sheria, kila chama hujitafutia rasilimali zake kwa ajili ya kugharamia kampeni za uchaguzi. Na hii inabainishwa na sheria ya Gharama za Uchaguzi.
Sawasawa?
Mkuu mimi nime quote hii toka account ya JK ktk facebook. Kasema mwenyewe tembelea huko labda nambie nimekosea amount lakini hili kalizungumzia tena muda kitambo...
 
Mimi niliona kimoja kikipiga kampeni pale Buguruni siku kadhaa zilizopita....kwa keli sikuwalewa...hakuna aliyekuwa anasikiliza...nadhani wengine wanagombea basi tu...kupata ujiko kuwa waligombea kwa kuwa nina hakika wanajua hawawezi kushinda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…