Chonde chonde Viongozi Simba msimtwishe Mgunda zigo zito, mtamuumiza

Chonde chonde Viongozi Simba msimtwishe Mgunda zigo zito, mtamuumiza

mnaona ujinga anaofanya kocha mzungu wa azam? hata msomali asingecheza juzi vile na kupanga kikosi kile, akija kocha mpya sasa hivi atakuja na yake ya kizunguzungu, naunga mgunda kupewa team
TENA APEWE MSHAHARA MKUBWA, GARI NA NYUMBA MASAKI KAMA WALE WAZUNGU
 
Ni kweli Mzawa anajua lakini hupotezi kitu kwa kuendelea kupata uzoefu kutoka kwa waliotutangulia kisoka.

Akipatikana Kocha mwenye CV zilizoshiba atakuwa Mentor mzuri tu kwa Mgunda na Matola, hasa kwa mustakabali wao huko mbeleni.
Uzoefu na CV ndio zinajengwa hivi ilivyo kwa Juma Mgunda sasa unataka apate CV ya kufanya makubwa Afrika kocha mzawa aitolee wapi ikiwa vilabu vikubwa vyenye uwekezaji mkubwa na ndio wanashiriki michuano hiyo hatuwaamini.
Alikuja kocha Sven Simba akiwa hana CV yoyote ya maana lakini kupitia mafanikio aliyopata Simba Sc alitengeneza CV yake nzuri na hakukaa sana akapandiwa dau akaondoka zake
Sasa kuna ubaya gani sisi kama Simba hiyo imani tuliyompa Sven tusimpe Kocha wetu Juma Mgunda ambaye so far mpaka sasa timu inacheza vizuri na matokeo anapata tena katika mazingira yote hadi ugenini

Qn;
Na kwanini unaamini chini ya Mgunda wachezaji wanashinda kwasababu ya Morali tu na Sio uwezo/mbinu za kocha Mgunda ila akija Mzungu ndio wataanza kushinda kwa uwezo wa Kocha mzungu??
 
Mgunda ni kocha mzuri. Hata akifungwa haimaanishi kuwa mbovu. Makocha wote wanafungwa.
Cha msingi Mgunda apewe huduma zote kama wanazopewa wazungu. Apewe makocha bora wa viungo, wa makipa, match analyst, usafiri mzuri, mshahara na posho nzuri, asikilizwe kama wanavyosikilizwa wazungu, na mengine tusiyoyajua. Naamini hata wachezaji wanamkubali.

Na yeye mgunda ajichunge, aache mambo ya uswahili. Kama kung'ang'ania kumchezesha Bocco aliyeisha n.k. Hivi ndivyo wabongo wanavyopoteza uaminifu.
 
Kutokana na kuwa Simba wanaendelea kupata matokeo mazuri kumekuwa na kelele kila kona kutoka kwa Mashabiki wakitaka Mgunda apewe timu kamili kama Kocha Mkuu.

Na Viongozi wa Simba ni kama vile wamekaa wakisubiri kama vile wanasikilizia. Nadhani hili litawagharimu Simba, huu mchezo wa kuwafuatisha Mashabiki sidhani kama utakuwa na mwisho mwema.

Ninashauri Simba waendelee na wakamilishe mchakato wa kumtafuta Kocha Mkuu na Mgunda na Matola wabaki kama Wasaidizi wakiendelea kupata uzoefu, walau kwa misimu miwili.

Shughuli iliyopo mbele bado ni mzigo mkubwa kwa Mgunda na Matola na inavyoonekana matokeo mazuri wanayoyapata Simba pamoja na maelekezo ya mwalimu ila ni kama pia kuna morali binafsi ya wachezaji, na hili halitachukua muda mrefu.

Namuheshimu sana Mgunda, lakini kutoka Coast mpaka Simba na kuridhika na matokeo yanayopatikana ni kucheza kamari tu.

Kama ni kweli kulikuwa na mpango wa kumfuatilia Kocha wa Asec basi mipango hiyo ifanyike ikiwezekana Kocha aje.

Mashabiki wenu hawa timu itakapoanza kukosa matokeo kama kawaida watabadilisha kiitikio(chorus) na hamtokuwa tayari kusikiliza nyimbo zao.
Tukimalizana Oktoba 23 hapo sasa hili nalo tutaliangalia...

Mmezoea kuwafunga makocha wa KIDHUNGU safari hii mna m-bongo mwenzenu anajua fitna zenu zote, shabaash.
 
Naona kama wameanza kumuogopa huyu Gwadiola mnene maana hata mechi ya trh 23 na utopwinyo tutawafunga tena nyingi tuuuu
Na ni fundi sana wa kuwakabili hao uto, msimu wa 20/21 aliwaharibia unbeaten yao pale mkwakwani, juzi tu hapa kawagongesha 3 wakawa wanahangaika kuzisawazisha kwenye fainal ya FA.

We subiri hiyo tarehe 23 uone.
 
Mimi sinq shaka kabisa trh 23 tunawafumua tena nyingi tuu
 
Naona kama wameanza kumuogopa huyu Gwadiola mnene maana hata mechi ya trh 23 na utopwinyo tutawafunga tena nyingi tuuuu
[emoji16][emoji3][emoji16][emoji119][emoji846][emoji442][emoji2969][emoji932] duh noma
 
Kutokana na kuwa Simba wanaendelea kupata matokeo mazuri kumekuwa na kelele kila kona kutoka kwa Mashabiki wakitaka Mgunda apewe timu kamili kama Kocha Mkuu.

Na Viongozi wa Simba ni kama vile wamekaa wakisubiri kama vile wanasikilizia. Nadhani hili litawagharimu Simba, huu mchezo wa kuwafuatisha Mashabiki sidhani kama utakuwa na mwisho mwema.

Ninashauri Simba waendelee na wakamilishe mchakato wa kumtafuta Kocha Mkuu na Mgunda na Matola wabaki kama Wasaidizi wakiendelea kupata uzoefu, walau kwa misimu miwili.

Shughuli iliyopo mbele bado ni mzigo mkubwa kwa Mgunda na Matola na inavyoonekana matokeo mazuri wanayoyapata Simba pamoja na maelekezo ya mwalimu ila ni kama pia kuna morali binafsi ya wachezaji, na hili halitachukua muda mrefu.

Namuheshimu sana Mgunda, lakini kutoka Coast mpaka Simba na kuridhika na matokeo yanayopatikana ni kucheza kamari tu.

Kama ni kweli kulikuwa na mpango wa kumfuatilia Kocha wa Asec basi mipango hiyo ifanyike ikiwezekana Kocha aje.

Mashabiki wenu hawa timu itakapoanza kukosa matokeo kama kawaida watabadilisha kiitikio(chorus) na hamtokuwa tayari kusikiliza nyimbo zao.
Ila nyie utopolo mbona mna gubu sana kuhusu Mgunda?

Mbona timu inafanya vizuri tu uwanjani kuliko hata wakiwepo hao wazungu mnaowataka?

Kufungwa mechi ya jana sio kosa la Mgunda bali ni usajili mbovu wa baadhi ya wachezaji wa kiwango cha kawaida sana.

Vipngozi acheni ubahili sajilini wakati wa dirisha dogo
 
Back
Top Bottom