Chonde chonde wanasiasa msiigeuze mechi ya Taifa Stars vs Uganda kuwa uwanja wa kupromoti sera zenu

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Nimelazimika kutoa chonde chonde hii baada ya kuwasikia kwa masikio yangu baadhi ya wanasiasa wakihamasishana kuvaa sare za chama siku ya mechi.

Ni vema kama sote tukavaa kitaifa zaidi kwani kama tunaweza kuuweka pembeni usimba na uyanga wetu kinatushinda nini kuweka itikadi za vyama pembeni?

Wafuasi wale wa ACT wazalendo waliokuwa wanahamasishana naamini watanisoma na kuachana na mpango wao.

Maendeleo hayana vyama!
 
Taifa Stars Ni Timu Ya Wananchi Na Wazalendo Kama Ilivyo Yanga . Simba Ni Timu Ya Wafanyabiashara Wa Kihindi Na Kiarabu .
 
Mbona ccm huwa wanavaa kila kwenye shughuli ya kiserikali na hakuna anayewakemea? Na hiyo siku ya mechi utawaona.

Kwanza hiyo ni kuonesha kila chama kinaunga mkono timu ya taifa. Mimi nashauri vyama vyote vivae sare zao hiyo itakuwa sawa na kuvikusanya vyote pamoja na kuonesha umoja wa kitaifa.

Maendeleo hayana chama.
 
Nimelazimika kutoa chonde chonde hii baada ya kuwasikia kwa masikio yangu baadhi ya wanasiasa wakihamasishana kuvaa sare za chama siku ya mechi.

Ni vema kama sote tukavaa kitaifa zaidi kwani kama tunaweza kuuweka pembeni usimba na uyanga wetu kinatushinda nini kuweka itikadi za vyama pembeni?

Wafuasi wale wa ACT wazalendo waliokuwa wanahamasishana naamini watanisoma na kuachana na mpango wao.

Maendeleo hayana vyama!
Usizungukezunguke. Walioiteka hii mechi na kuanza kuhamasisha kiramli Ni makada wa chama chako wakiongozwa na DAB. Go to the point. Acha unafiki wa kitoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaa....... Iringa siyo kinondoni!
Tatizo la CCM Iringa badala ya kujenga chama chao wao wako bize kushindana na Msingwa. Msigwa hajichaguwi bali huwa anachaguliwa na wana Iringa.

Wao wanadhani eti kushindwa kwao kunatokana na wao kutokuungana, siyo kweli. Iringa wana CCM kwani wako wangapi hadi kuungana kwao ndiyo wawe na ushindi? Hawana wagombea bora na mbaya zaidi walipotoshwa kununua Madiwani wa CHADEMA ambao ushindi wao kwa asilimia kubwa ulichangiwa na Msingwa mwenyewe.

Hakuna hata diwani mmoja aliyekwenda CCM toka CHADEMA ambaye alishinda kwa ushawishi wake mwenyewe bila ya kuchangiwa na ushawishi wa Msingwa.
 
Nakubaliana na wewe kuwa kushindwa kwa CCM kunatokana na wao kukosa wagombea bora tena wazawa.

Nakumbuka hata mwaka 1995 wakati mwalimu Kibassa anashinda ubunge dhidi ya Dr Kitine, wazee wa Iringa walimwambia Nyerere alipokuja kumkampenia Mkapa kuwa Rais tutakuchagulia lakini mbunge tunachagua wenyewe hatupangiwi.

Historia hiyo wadogo zangu Kasesela na Hapi hawaijui!
 
Nakubaliana na wewe kuwa kushindwa kwa CCM kunatokana na wao kukosa wagombea bora tena wazawa.

Nakumbuka hata mwaka 1995 wakati mwalimu Kibassa anashinda ubunge dhidi ya Dr Kitine, wazee wa Iringa walimwambia Nyerere alipokuja kumkampenia Mkapa kuwa Rais tutakuchagulia lakini mbunge tunachagua wenyewe hatupangiwi.
Kwenye kikao kile kabla ya Mwalimu kuondoka nilikuwemo. Iringa wanajua wamtakae halafu wao CCM wagombea wao hutoka Dar es salaam pale kwenye vikao vyao vya pale Makumbusho.
 
Hahahaa...... Hata siku ya kutangaza matokea nilikuona pale mnara wa saa na mawe yako mkonono....hahahaa nyie wadimi mlikuwa wakorofi sana!
 
Back
Top Bottom