Rais wa TEC Askofu Nyaisonga amelinajisi Kanisa letu. Ameamua kuasi kiapo chake cha ukuhani cha kusimama katika haki kwaajili ya kulinda uswahiba binafsi na mtawala.
Kauli yake imelitia doa Kanisa Katoliki. Amemwumiza Kristo, ambaye fundisho lake kubwa ni UKWELI na UPENDO.
Tunaomba maaskofu wetu wote wa Kanisa Katoliki, kila jimbo, na wasaidizi wao (mapadre), watueleze waumini kama maneno ya Askofu Nyaisonga ndio msimamo wa Baraza la Maaskofu. Kama utakuwa ndiyo msimamo wa Kanisa, itatupatia nafasi waumini kutambua kuwa Ibilisi ameanza kutenda kazi yake kwa kupitia wenye mamlaka ndani ya Kanisa.
Siku zote katika vita, adui hujitahidi amteke Kamanda Mkuu maana ndiye mwenye siri za Jeshi zima.