DOKEZO Chondechonde, Wakulima wa Namawala wamechoshwa na Askari Polisi Ifakara na familia ya kambenga

DOKEZO Chondechonde, Wakulima wa Namawala wamechoshwa na Askari Polisi Ifakara na familia ya kambenga

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

bababikko

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
2,696
Reaction score
4,352
Huu mgogoro unaoendelea ni miaka 17 hadi sasa Kambenga hana hati yoyote ya kumiliki ekari 1000 badala yake anatishia wanakijiji kwa hukumu za michongo.

Jana askari wawili pamoja na familia ya hiyo walienda mashambani na kunyang'anya mbegu wananchi wakitaka kupanda mashamba yao.

Tafrani ilitokea na wanakijiji wakajitokeza kwa wingi licha ya askari hao kupiga risasi ovyo wakazidiwa nguvu wakakimbia.

Sasa wananchi hao wamemwandikia barua waziri wa mambo ya ndani kuomba kibali cha kuwashtaki askari hao
 
Attachments

Dah! Hilo jina la Kambenga ni maarufu sana Ifakara. Tangu miaka ya 1990's nilipokuwa huko, nilikuwa nalisikia.

Poleni sana wananchi wa Namwawala. Ni vyema mkapambania haki yenu, mpaka kieleweke.

Long time kitambo!! Navikumbuka sana hivyo Vijiji vya Namwawala (Ruipa), Idete, Mofu, Kisegese, Mbingu, Mngeta, Ikule, Chita, Chisano, Mlimba, Mpanga, Tanganyika Masagati, Uchindile, nk. Kwa kilimo cha mpunga.
 
Kuna Mawaziri wa michongo ndiyo chanzo cha haya yote
 
Sijaelewa hapo...Police wana kinga gani ya kutoshitakiwa hadi kiombwe kibali kwa Waziri? Na je Waziri akikataa? Au kutokujibu?
 
Sasa Kama huyo kambenga Hana haki na hiyo ardhi na nyinyi ndio wenye haki si muende mahakamani,kwa nn mnataka huruma ishike nafasi na sio Sheria,?
 
Kero zenu zitasikilizwa na kutolea ahadi ya kuzitatua mwaka ujao wakati wa kampeni. Wananchi kuweni na subira.
 
Kama imeandikwa hukumu, hata umuandikie nani, Cha msingi nenda mahakamani katetee haki yako, Waziri hawezi kutengua hukumu.
 
Malalamiko ya wananchi ya walakini. Inaonesha eneo ni Halali kwa Kambenga ila kama kawaida ya tabia ya wananchi wa Bonde la Kilombero ni majungu na kulialia kutafuta huruma.

Washaurini waende mahakamani
 
Kama imeandikwa hukumu, hata umuandikie nani, Cha msingi nenda mahakamani katetee haki yako, Waziri hawezi kutengua hukumu.
hapa wakulima pia wanatoa tahadhari litakuja la kutokea hawa wamefumba macho
 
Kama imeandikwa hukumu, hata umuandikie nani, Cha msingi nenda mahakamani katetee haki yako, Waziri hawezi kutengua hukumu.
Wanakwambia ati "hukumu za mchongo" Sasa sijui Wana mahakama zao ambazo zinahukumu zisizo za mchongo?
 
Malalamiko ya wananchi ya walakini. Inaonesha eneo ni Halali kwa Kambenga ila kama kawaida ya tabia ya wananchi wa Bonde la Kilombero ni majungu na kulialia kutafuta huruma.

Washaurini waende mahakamani
Wanakwambia ati "hukumu za mchongo" Sasa sijui Wana mahakama zao ambazo zinahukumu zisizo za
 
Wanakwambia ati "hukumu za mchongo" Sasa sijui Wana mahakama zao ambazo zinahukumu zisizo za
Wanae ndio wanaendeleza mtiti

Hukumu za mchongo yaani hata mtoto anaelewa . kwa kifupi Kambenga Family Haina hati yoyote ya umiliki eneo Hilo Mali ya Wana kijiji

Sent from my Nokia C10 using JamiiForums mobile app
 
Sasa Kama huyo kambenga Hana haki na hiyo ardhi na nyinyi ndio wenye haki si muende mahakamani,kwa nn mnataka huruma ishike nafasi na sio Sheria,?
uamuzi uliishatolewa na mkuu wa mkoa Martin Shigela aliumaliza baada ya makaratasi ya kambenga kuonekana hayana mashiko akatulia sasa ameanza tena
 
Back
Top Bottom