Choo cha kulipia Tegeta sokoni kimeniharibia siku

Choo cha kulipia Tegeta sokoni kimeniharibia siku

Mama Edina

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2022
Posts
850
Reaction score
2,019
Niende moja kwa moja.

Nimeingia sokoni, nikaona siwezi kufika kwangu na mizigo, acha leo nijisitiri vyoo vya kulipia Tegeta looh salaleee!

Ni Muda huu nahisi leo sitakula, nimekata tamaa kabisa. Ndani ya vyoo hivi unatoka na ugonjwa. Jamaniee sikushauri ukaangalie, panatia huruma. Nzi, kinyesi juu sijui, Jaman MTU kamaliza kupata huduma anashindwaje kusafisha.

Siku yangu imeharibika mapema Sana Kwa hali hii safari ni ndefu ndefu Sana ikiwa usafi wa choo uko vile.

Kinondoni mnapokea malipo ya huduma kwa vyoo vile, jiangalieni
 
🤣🤣🤣🤣 system za kukatia nyengo maeneo ya sokoni hazijawahi kuwa safi kabisaa sio hapo tu lakini maeneo mengi.

Hapo sehem ingekua salama n kwenye lodge ya karibu, sema.sasa nako n mtihani.

Mmama wa watu umetoka zako kushusha kimba na vimfuko vyako vya nyanya na njegere ile unatoka nje unakutana na yule jirani yako mmbeya. Ghafla mtaa mzima.unajua ulienda kukandamizwa asubuh na mapema gesti za sokoni.
 
Bado tupo kwenye round ya 2 ya ulimwengu ilihali wenzetu wapo round ya 10.

Ni rahisi kujua aina ya akili ya watu wetu kupitia vyoo na uchafu unaosambaa barabarani. Unapata majibu kamili tuna watu wa namna gani.
Mtu unamuwekea dustbin lakini anatupa uchafu pembeni kabisa ya dustbin hiyo hiyo.

Kama vile mtu anapoingia maliwatoni na kuamua kujisaidia pembeni, sio kwamba kabanwa sana ni kwa vile tu ni choo cha halaiki na hatosafisha yeye.
 
Nimetafakari ukianzisha biashara ya kuisambaza bidhaa majumbani in bulk italipa Kwa sie tusopenda kukutana na mambo haya.

Ukitungua ofsi maeneo ya sokoni. Magari ya kisambaza, nyanya,karoti,matunda nk italipa. And this is serious
 
Nimetafakari ukianzisha biashara ya kuisambaza bidhaa majumbani in bulk italipa Kwa sie tusopenda kukutana na mambo haya.

Ukitungua ofsi maeneo ya sokoni. Magari ya kisambaza, nyanya,karoti,matunda nk italipa. And this is serious
Mbona Kuna vijana wanafanya sana hizi delivers za vitu vya sokoni kwa pikipiki na magari huku maofisini/majumbani?
 
Back
Top Bottom