Chris Brown: Nimechoka kuwa mwema, nitakuwa mwovu

Chris Brown: Nimechoka kuwa mwema, nitakuwa mwovu

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Muimbaji na mwanamuziki nguli nchini Marekani, Chris Brown, ameibua mjadala mzito duniani kote baada ya kutoa tamko kali mtandaoni akitangaza kuwa amechoka kuwa "mtu mwema" na sasa ataanza kuwa "muovu" kutokana na kile alichodai ni kufanyiwa vitendo visivyo vya haki katika tasnia ya muziki.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, msanii huyo wa R&B amefunguka kwa hisia kali dhidi ya wasanii wenzake na mfumo wa muziki akisema:

"Siwapendi hata mmoja wenu nyie watu maarufu. Mimi ni bora zaidi yenu bila ubishi, mimi ni mfalme. Hakuna msanii hata mmoja duniani anayeweza kunifikia na mnajua hilo. Nimechoka kuwa mtu mwema, nitakuwa yule muovu."

Ujumbe huo uliosambaa kwa kasi kubwa mtandaoni unachangiwa na kile kinachoonekana kama ghadhabu za muda mrefu za msanii huyo kuhusu namna anavyonyimwa heshima na tuzo anazostahili ikilinganishwa na uwezo wake mkubwa wa kuimba na kucheza.

Kauli hii imewagawanya mashabiki na wadau wa muziki mtandaoni; huku wapo wanaomuunga mkono kuwa ni mfalme asiye na mpinzani anayepigwa vita na tasnia, wengine wanajiuliza iwapo kauli hii ni hasira za kweli au ni mbinu ya kutangaza mradi wake mpya wa muziki unaofuata.
1790153823884.png
 
Back
Top Bottom