Mkuu
Sikonge umetoa tahadhari muhimu sana kwa ajili ya usalama wa Mchungaji Msigwa pamoja na wazalendo wengine wa aina yake, pamoja na kuwa vijana wa lumumba project wanajitahidi kupotosha.
Ikumbukwe kuwa
Chris Lukosi alipata kuwa askari polisi wa jeshi la policcm, sasa inapotokea anamtishia kamanda Msigwa kwamba siku zake zinahesabika hilo si suala la lkupuuzia hata kidogo, na kwa kuzingatia kuwa mara kadhaa askari polisi, askari wa JWTZ/JKT na askari wa magereza wamekuwa wakikamatwa na wengine kutuhumiwa kujihusisha na matukio ya ujambazi, ujangili na unyang'anyi matukio ambayo yamekuwa yakiendana na mauaji ya watu.
Kwahiyo
Chris Lukosi anatakiwa ajitokeze hadharani atueleze ni kwanini amefikia hatua ya kumtishia maisha Mchungaji msigwa hasa baada ya kumtaja katibu mkuu wa ccm kuwa ni jangili wa tembo wetu? je ni kusema kinana ndiye kamtuma amuue Msigwa ili kupoteza ushahidi alionao dhidi ya biashara ya ujangili inayofanywa na katibu mkuu huyo wa ccm?
Tusiyachukulie haya mambo kirahsi rahsi halafu ikatokea Mchungaji Msigwa amepatwa namaswahibu ndipo tukaanza kujiuliza kulikoni. Ni muhimu sana kuchukua tahadhari zote za kuhakikisha kwamba watu wote wanaosimama mstari wa mbele katika kupigania maslahi ya nchi hii wanalindwa na kuhakikishiwa uslama wa maisha yao.