Chris Watts - Mwanaume aliyeua watoto wake wawili na mke wake mjamzito kisa penzi la mchepuko

Chris Watts - Mwanaume aliyeua watoto wake wawili na mke wake mjamzito kisa penzi la mchepuko

Nafaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
12,154
Reaction score
31,246
"Behind every murder, there is a motive"
chris.jpg

Wanawake wengi wa Kitanzania kama siyo wa Afrika utasikia, mimi ningetamani kuolewa na mzungu. Kwanza ni waaminifu na wana mapenzi ya kweli! Muda mwingine nawatazama nacheka kicheko cha mwenyekiti cha Hiiii! Wanaume wa kizungu wakichepuka wakata kuoa wanaogopa kugawana mali na malezi ya waoto. Kuna visa kadhaa vya wanaume kuwaua wake zao ili wapate kuishi au kuoa tena bila tatizo. Na hiki ndicho alicho kifanya Chris Watts huyo mnayemuona kwenye picha akiwa na mkewe na waoto wao wakionekana wenye furaha.

Tarehe 13, mwezi wa 8 wmaka 2018, karatasi zilikuwa zimetapakaa kila mahali zikimuonyesha mwanamke mjamzito aliyejulikana kama Shanann Watts pamoja na watoto wake wa kike wawili wka majini ya Bella aliyekuwa na umri wa miaka 4, na Cleste aliyekuwa na umri wa miaka 3. Karatasi hizi ziliandikwa kuwa watu hawa wanatafutwa hawajilikani walipo baada ya kupotea ghafla kutoka wenye makazi yao huko Frederick, Colorado.

Mwanzoni, Chris Watts ambaye ndiye Mme wa Shanann na baba wa watoto waliopotea, alikubali kufanya mahojiano na vituo vya habari. Katika mahojiano hayo ambayo yalikuwa yakirushwa Mubashara, Watts alionekana akiwa kama akachanganyikiwa akiwaomba watu wamsaidie kupata familia yake. Watu walijitoa kumsaidia na wengi waliumia sana wakumuonea huruma. Lakini kwenye macho ya makachero, wao walikuwa wakiona kitu toauti.

Siku mbili baadae, Watts alikamatwa kwa kosa la kuhusika na katika mauaji ya familia yake.

Chanzo cha mauaji hayo

katika mitandao ya kijamii, Watts na mke wake walionekana kama wako kwenye ndoa yenye furaha. Lakini ukweli ni kwamba Watts alikuwa ana mahusiano ya kimapenzi na mfanyakazi mwenzie, akimdanganya kuwa yeye na mke wake walikuwa katika hatua za kupeana taraka.

Wakati wa majira ya joto, Shannan aligundua kuwa Watts alikuwa hayuko karibu naye tena. Shanann baada ya kuhisi tatizo hili alianza kujaribu kutatua tatizo ili kuokoa ndoa yake.

Watts alisafiri kwenye shughuli za kibiashara, na tarehe 13 mwezi 8, 2018, alirejea. Siku hiyo ulitokea ugomvi mkubwa baina yake na mkewe na ugomvi huo ulimpelekea Watts kumnyonga mkewe aliyekuwa na ujauzito wa wiki 15.

Pia watts aliwaua watoto wake, jambo ambalo linashangaza kwasababu watu wanajua kuwa alikuwa akiwapenda watoto wake sana.

Mtiririko wa Matukio mpaka kutekeleza mauaji
shab.jpg

Tarehe 11, mwezi 6 mwaka 2018, Shannan alireodi video ambapo alionekana kumsuprise mmewe kwa kumambia ana ujauzito ambao ungepelekea wao kupata mtoto wao wa tatu.

katika video hiyo, Watts naonekana kufurahi kupitaa kiasi. Anaonekana akimwambia hii ni bomba sana, kisha anambusu na kumwambia, nadhani hutokea pale unapotaka itokee.

Tarehe 14, mwezi 6, 2018, Shannan alilikodi video na kuiweka kwenye mtandao ikimuonyesha Bella Akiimba wingo wenye ujumbe wa kuonyesha jiinsi gani anampenda baba yake.

chris2.jpg

Bella anaonekana akiimba "Baba yangu ni shujaa/hunisaidia nikue huku nikiwa mwenye nguvu/ Ananifanya niwe mwenye kujiamini pia/ Ananisomea vitabu/ Hufunga kamba za viatu vyangu/ We ni shujaa wa kila kitu/ baba, baba, nakupena."

Tarehe 14, mwezi 6,mwaka 2018, Watts anachukua namba ya simu ya Nichol Kessinger ambaye baadae anakuja kuwa mchepuko wake.

chris3.jpg

Nichol anadai walianza mahusiano rasmi mwishoni mwa mwezi wa sita mwaka 2018.

Tarehe 17, mwezi 6 mwaka 2018, ndipo Watts alimweleza ukweli Nichol kuwa ameoa na ana watoto ila yeye na mkewe wako katika mchakato wa kupeana taraka. Maelezo haya alikuja yatoa Nichol kwa polisi. Siku ya wababa duniani, Shanann anamwandikia ujumbe mzuri mumewe kwenye ukurasa wa Facebook uliosomeka
"Chris, tumejaliwa sana kuwa nawe katika maisha yetu! Unatuanyia mambo mengi kila siku na unatujali sana. Wewe ndiyo sababu nilikuwa na nguvu ya kukubali kubeba namba 3 (akimaanisha mimba)."

Tarehe 19, mwezi wa 6, Shanann anaweka picha ya picha ya kwanza ya Utra-sound ikuonyesha mtoto aliyeko tumboni, huku akiandika ujumbe "Baba bora hakuna baba bora zaidi kwa sisi jinsia ya kike kama huyu."

Tarehe 27, 2018, Shanann anawachukua Bella na Celeste anawapeleka na kusafiri nao kwenda North Carolina. Anakaa nao huko kwa wiki tano. Kipindi hicho Watts alikuwa kabaki nyumbani akifanya kazi.

Nitarudi baadae kidogo kumalizia nimepata mgeni. Kwa wengine Google jina tu utapata story nzima.
 
Tupo pamoja mkuu mie ndio ulevi wangu huo
 
Kuoa haraka haraka ipo Africa,ng'ambo kuoa ni big risk ni kujiletea umaskini mkiachana (divorce)
 
Hii niliifuatilia youtube iliniumiza sana..Chriss mchepuko ulimchanganya mpaka akafikia kutafuta namna amtoe mke wake mimba. Hakufanikiwa baadae akaona suluhisho ni kuwaua wote aanze upya na nicole.
Akiwa jela hajawahi kabisa kujutia kuiua familia yake ila anaumia sana kumuangusha mchepuko kwa kukamatwa wakati walikua wana mipango mizuri kwa mapenzi yao.
Familia yake yaan baba na mama yake wanamlaumu Mareham mkewe kwa kusababisha auwawe na hawamlaumu mtoto wao Chriss na wameshamsamehe.
 
Hatari sana.
 
Hatari sana.
Sana na inaonekana mchepuko ndo alimshawishi afanye hivyo japo Chris's anakataa kata kata.

Sababu walikuta kwenye google search history ya mchepuko amegoogle kuhusu magauni ya harusi, amegoogle majina ya watu waliowahi kuua wake wa mabwana zao so alikua ana husika kwa namna moja ama nyingine.
 
Kwa hiyo inaonekana jamaa aliamua afungwe peke yake na akaamua amlinde mchepuko asiwe hatiani? Hii story imenishangaza sana, jamaa sijui alipewa nini na huyo mwanamke.
 
Kwa hiyo inaonekana jamaa aliamua afungwe peke yake na akaamua amlinde mchepuko asiwe hatiani? Hii story imenishangaza sana, jamaa sijui alipewa nini na huyo mwanamke.
Exactly ndo inavyoonekana ameamua kumlinda. Inashangaza sababu hata muda wa mahusiano yao I mean tangu aanze kuchepuka mpka kuua ni miezi isiyozidi sita kabla alikua mume bora na baba bora kwa watoto wake. Mapenzi yao yalianza ghafla na kushamiri kwa haraka sana wakafikia mpaka kuanza kupanga kuoana na mchepuko akamuahidi kumzalia mtoto wa kiume. Chiss alikua na watoto wawili wakike na mke alikua njamzito mimba ya mtoto wa kiume.
Chris's alivyoahidiwa na mchepuko mtoto wa kiume akaona aitoe mimba ya mkewe ili aweze kuzaa na kipenzi chake mchepuko. Kama alichanganyikiwa hivi.
 
Jamaa alikuwa infatutaed, ule utamu wa penzi jipya ulimchanganya. It happens mkuu. Lakini nimemshangaa sana, bora hata angeomba divorce kuliko kukatisha uhai wa mke wake. Ama angejipa muda angekuja kumuona mchepuko wa kawaida tu kwa sababu angekumbuka hata ana mke na watoto ambao wanampenda na kumuamini sana, infact mke wake alikuwa anampenda sana and the woman believed in him too much, she ended up losing her mind and life for the man. Too sad. Itabidi niifuatilie hii story YouTube maana cases kama hizi huwa zinanipa shauku ya kupata lessons kutoka upande mwingine wa maisha.
 
Back
Top Bottom