Christian Bella afanya show Ikulu iliyoandaliwa na Rais Magufuli kwa ajili ya Rais Kabila wa DRC

Haahaa, mzee kaona hali mtaani ngumu kaamua kuacha zile pary za sambusa moja moja mkiwa wima, kama kuna mtu aliifaidi ikulu ni Jakaya jamani loo acha aendelee kuzoa tuzo maana anajua kula na wengine.
 
Haahaa, mzee kaona hali mtaani ngumu kaamua kuacha zile pary za sambusa moja moja mkiwa wima, kama kuna mtu aliifaidi ikulu ni Jakaya jamani loo acha aendelee kuzoa tuzo maana anajua kula na wengine.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] chukua sambusa moja tu
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] chukua sambusa moja tu
Mkuu alitisha sana haa, si kubana matumizi kule bali balaa, halafu anaepewa sambusa moja ni mwanajeshi haahaaa utani wa ngumi ule.
 
Uku sasa ni kukosa uzalendo kwa nini asingewaalika wasanii wa nyumbani? Ingekuwa Ikulu ya Congo kuna msanii wa Tanzania angealikwa kweli?
Kwa jicho pana, kwa kuwa hafla hiyo ilikua maalum kwa ajili ya rais wa Congo ilibidi sana msanii wa congo awepo maalum kwa kuwapa raha raia wa kongo.. Pia Magufuli anamkubali sana Bella mara nyingi hua anazunguka nae.. Yote kwa yote Bella nimekaa nae ni mtu mwenye roho ya CHUMA, na ana udhubutu wa kufanya chochote.. Pia tujifunze Wakongo ndio wataalam wa Muziki hapa africa (muziki halisi wa band/live) ndio maana dunia nzima kwenye club za usiku lazima uwakute wanapiga live band/muziki hali.. Pia Wakongo ni watu wenye kujiamini na wenye roho ngumu.. Jiulize leo wasanii laini kama yamoto band walivyo laini wanaweza kwenda wenyewe nchi za watu na kuishi huko na kuanza kutafuta maisha ya muziki.. JIBU ni hapana ..
 
Wageni kutoka nje ya Tanzania wakija huku inatakiwa tuwaonyeshe mila na utamaduni wetu ili wakifika kwao Watutangaze. Unafikiri Kabila atajifunza nini kwa Christian Bella wakati Congo kuna wanamuziki wa bolingo wazuri zaidi ya huyo Bella.. Ndio maana watalii wa kizungu wakija Tanzania tunawauzia vitu vya kitamaduni kama vinyago,shanga za kimasai, n.k ili wakifika kwao wakatangaze utamaduni wetu.....Huwezi kumuuzia mtalii TV au Simu wakati kwao zipo nzuri zaidi ya hizi huku kwetu.
 
Usipende kukariri maisha.. je unadhani kutangaza utamaduni ndio ilikua target ya Magufuli??? Je unajua kuna mambo ya msingi zaidi ya kutangaza utamaduni/muziki wetu pale??? Je unajua Christian bella kuwepo pale ni muhimu mara 100 zaidi ya kutangaza utamaduni wetu???? Ngoja nikupe somo kidogo, kuwepo kwa Bella pale ni trick kubwa aliyotumia Magufuli kuonyesha kwamba Wakongo wanadhaminiwa, na wanapewa nafasi, hawabaguliwi, hii itasaidia sana hata wageni wetu na watanzania waliopo kongo kupewa priorities kadhaa., as long as hapo nyuma kulikua na ogomvi kati ya tanzania na kongo, kongo walianza kudai tunawasaidia waasi.. Tukiacha burudani hii ilikua ni trick ya kuonyesha umoja, mshikamano, na amani baina ya Tanzania na Kongo
 
Ukiona mtu anamponda Bella kwa sauti yake, huyo ukimsachi huwezi kumkosa na matunguli, jamaa ni bonge la msanii. Nimefurahi kuona hata JPM anamkubali, hope next time ataalikwa akapige bonge moja la show huko Congo. Tunahitaji kina Diamond wengi ili vijana wengi wapate fursa. Hapo ndo manager wake anatakiwa aoneshe ubunifu katika kazi, kijana keshapata promo sasa amtafutie show za maana.
 
Yamoto band kesha wachoka?

muwe hata mnajifikilia yaani yamoto band wakaimbe mbele ya marais ....una ramboooooo nna muwaaaaaaa

Asilimia 90 ya nyimbo zao zimejaa mitusi ya kiswahilini

Anaye watungia nyimbo hawa watoto Mungu anamuona!!!
 
Nani amekwambia hiyo show ilikuwa kwaajili yakutaka kutangaza utamduni? Kwanini isiwe Kabila anapenda muziki wa kikongo ndio maana akachaguliwa Bella? Ndio maana hata Tz kuna migawaha ya wachina, ili wapate kitu wanachotaka wawapo ugenini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…