Christian Bella afanya show Ikulu iliyoandaliwa na Rais Magufuli kwa ajili ya Rais Kabila wa DRC

Christian Bella afanya show Ikulu iliyoandaliwa na Rais Magufuli kwa ajili ya Rais Kabila wa DRC

Haahaa, mzee kaona hali mtaani ngumu kaamua kuacha zile pary za sambusa moja moja mkiwa wima, kama kuna mtu aliifaidi ikulu ni Jakaya jamani loo acha aendelee kuzoa tuzo maana anajua kula na wengine.
Sambusa zenyewe ni zile za kabichi sio za nyama.
 
Nchi Ya VIWANDA
Safi Sana Jpm Kazi Na Dawa Burudani Muhimu
 
Hii inauma sana,wako waliozunguka mikoa yote wakati wa kampeni ila mpaka sasa hawajawai kuitwa pale ikulu.
Hongera Bella.
 
Alikuwa anamuimbia Magu, "Usiliiie". Sasa sijui alikuwa analilia nini?
 
Namkubali sana sana sana Christian Bella lakini haikuwa sahihi yeye kutumbuiza kwenye dhifa ya kitaifa, hapo tulitakiwa kumuona saida caroli akichambua kama karanga. Otherwise labda kama kuna wasanii wengine locals walioalikwa
 
Wageni kutoka nje ya Tanzania wakija huku inatakiwa tuwaonyeshe mila na utamaduni wetu ili wakifika kwao Watutangaze. Unafikiri Kabila atajifunza nini kwa Christian Bella wakati Congo kuna wanamuziki wa bolingo wazuri zaidi ya huyo Bella.. Ndio maana watalii wa kizungu wakija Tanzania tunawauzia vitu vya kitamaduni kama vinyago,shanga za kimasai, n.k ili wakifika kwao wakatangaze utamaduni wetu.....Huwezi kumuuzia mtalii TV au Simu wakati kwao zipo nzuri zaidi ya hizi huku kwetu.

Ngoma za asili zilikuwepo uwanja wa ndege wakati wa kumpokea.
 
Kifupi namkubali sana Bella " ndio msanii mwenye kipaji cha ukweli ukilinganisha na hawa waimbaji wetu wengi feki ambao wanabebwa na media "haijalishi kwao wapi'! Kwani anaimba kwa kiswahili fasaha/kinachoeleweka kuliko hawa wanaobana pua na kutoeleweka " kwa hili namuunga mkono JPM kwa kutambua hili.
 
Back
Top Bottom