Christina Shusho: Nilimuacha mume nitimize ndoto zangu

Christina Shusho: Nilimuacha mume nitimize ndoto zangu

Ndoa kama wakristo mnavyodai ni muunganiko wa mtu mume na mtu mke ili kuwa mwili mmoja. Hivyo huyo Shusho na mumewe walikuwa mwili mmoja na ndoto zake zilitakiwa ziwe ndio za huo mwili mmoja (ndoa).


Sasa kama ni mkristo anaetambua hilo basi kusema alimuacha mumewe kufukuzia ndoto zake ni utapeli wa hali ya juu huu.

Atupe sababu nyingine. Asitulaghai sisi wenye akili.
Alimkimbia Mzee shusho umli umekata
 
Kila mtu huitwa kivyake...

Sio lazima wawe pamoja...

Ikumbukwe Kila mtu hapa Duniani anakazi ambayo amepewa na Mungu kufanya.

Ndoa ni mambo ya Duniani tu.
Ndoa ilihasisiwa na Mungu, acha Ku promote udangaji! Ndoa ya, kikristo inavunjika mpaka mmoja afe,Ila kuolewa sio lazima, Ila, kwa, hawa dada zetu,kinachowavutia ni udangaji tu na tamaa, wakimuona Zuchu anavyofaidi kwenye ufuska,wanajiuliza kwanini wao wafungwe na ndoa
 
Hamna mtu anayeweza muelewa Christina kwakuwa ukiitwa na Mungu Kuna vitu unatakiwa uache ..

Hata wanafunzi wa Yesu waliacha hata kazi wakamfuata Yesu...

Mambo ya Rohoni na mwilini ni tofauti kabisa...
Hawakuacha wake au waume zao na wala Yesu hakuwaambia waache ili wamtumikie.
 
Hazipo kisheria ya kidini. Ni umalaya tu. Usipotoshe
Sawa, inawezekana hazipo kidini, lakini hao hao wanaoswalisha ndo hao hao wanafungisha ndoa hizo za mkeka, na hao hao ndo wanagawa talaka. Sasa kama mnakanana leo hilo lenu. Mbona mkisikia mtu kakojolea msaafu huwa mnaungana kumpiga au kuharibu mali za aliyefanya hivyo pamoja na jamii yake..!!?? Kwanini sasa msiungane hivyo hivyo kwa hao wanaofanya yasiyo ndani ya dini yenu? Au kwa vile waofanya hao ni wenzenu..!!??
 
Huyu anatumika na shetani, nilipomuona na Daimond tu nikajua tayari wamemdaka
Maneno mengine mtu ukiona yatakuchafua ni Bora ubaki nayo tu ndani kwa ndani sio lazima angesema chochote hata km ni kwa ajili ya kuwaaminisha wengine kua unaweza kuishi bila kukaa na Mwanaume Ila sio kwa statement ile
 
Maneno mengine mtu ukiona yatakuchafua ni Bora ubaki nayo tu ndani kwa ndani sio lazima angesema chochote hata km ni kwa ajili ya kuwaaminisha wengine kua unaweza kuishi bila kukaa na Mwanaume Ila sio kwa statement ile
Sijui hata kanisani kwake anawafundisha nini? Kwamba mkitaka kufanikiwa muachane na wanaume?
 
Kwa sasa Injili ni biashara nzuri,
sio rahisi kiongizi wa dini akanyanyuka na kukemea, naye ana mengi ya kukemewa.

Usisahau, Wasaliti wa Yesu Kristo ni wale wale walikua miongoni mwa wanafunzi wake. alio wachagua yeye
 
Hii ni kauli ya dada mwimbaji wa siku nyingi aitwae Christina Shusho, "Kusema ule ukweli mimi niliondoka kwa mume wangu ili nianzishe kanisa langu, nilijiongeza ili ndoto zangu ziweze kutimia maana kama ningeendelea kuungana na mume wangu sehemu moja ningeendelea kudidimia.

"Siku hizi hakuna mambo ya mke na mume ni mwili mmoja!! hiyo haipo utapotea ndugu yangu, wewe na mume wako au na mke wako hamuwezi kuwa sawa, hiyo haipo kila mtu ana njia zake.

Na mimi siogopi watu nasema ukweli, haya ninayoyasema ndiyo yapo kichwani kwangu, huyu ndio mimi, kwanini niendelee kudanganya watu. Kwanza mimi licha ya kuwa Mchungaji lakini sipendi watu waniite Mchungaji Christina Shusho, sipendi na sitaki"
Kwa kweli inasikitisha na kuhuzunisha sana.
 
Asirudi kuanza kulialia..!!
Unapoolewa au unapoowa, kuna mambo utayaacha. Sasa yeye alitaka aendelee na mambo yake kama bachela..!!?? Atoe ujinga wake..!!!

Katika vitu vinayowashinda wanawake, baadhi ni hivi;

1. Umaarufu
Wengi wa wanawake maarufu ndoa zao zina shida sana. Huwa wakishakuwa maarufu wanaona ndoa ni utumwa. Anataka awe popote muda wowote. Hii inakwenda hadi namna anavyowalea watoto wake.

2. Fedha
Mwanaume, anaweza akaishi na mwanamke asiye na kitu kwa maisha yao yote, lakini kwa wanawake walio wengi mwenye hela kuishi na mwanaume asiye na kitu, ikizidi sana wiki..!!

3. Cheo
Kuwa na cheo nako baadhi ya wanawake wameshindwa kujizuia kuwanyanya waume zao kwa vyeo vyao.

Huyu umaarufu tu unamsumbua..!!
UKO SAHIHI SANA,
NASIKIA NDOA ZA WALIO OA WABUNGE, NYINGI ZA MOTO SANA.
 
Angesema anapigwa bila sababu tungeelewa. Sio eti unaachana na mume kwa ajili ya mwito wa Mungu halafu hapo hapo unapingana na taratibu za ki Mungu.

Haiwezekani kuyasema yote hayo pale kwenye media sababu huenda ako anamstiri alokuwa mume wake.
Huwezi sema yote kinaga ubaga kwenye social media kama uko hekima hata kidogo.
 
kwa hiyo kaachana na mmewe akawe MCHUNGAJI? kwani mmewe amemzuia? ila ni MREMBO yule dada....jamaa sijui kaharibu nini pale.....au kakutana na muchungaji enzake.....??
Mrembo sana huyo
 
Back
Top Bottom