Christmas Uchagani: Wachaga wako overrated!

Christmas Uchagani: Wachaga wako overrated!

Mwaka huu niliamua kufanya tour trip huko Kilimanjaro ili kujifunza na kujionea shamrashamra za Wachaga wakisheherekea sikukuu ya Christmas.

Mpaka sasa bado nipo Uchagani.

Nimefanikiwa kufika maeneo ya Rombo, Mwika, Marangu, Old Moshi, Kibosho na Machame. Sijafanikiwa kufika maeneo ya Kirua Vunjo na Uru. Kuna mambo mazuri sana na mabaya machache niliweza kuyaona, kwa mada hii leo hapa sitayazungumzia mabaya wala mazuri (nitakuja na mada yake baadaye nikikamilisha ziara yangu), bali nitazungumzia baadhi ya mambo yaliyokuzwa kuliko uhalisia wake.

1. Sio kweli kuwa karibu kila Mchaga hurejea kwao kipindi hiki cha Kristmas. Ukweli ni kwamba idadi ya Wachaga wanaorejea makwao kipindi hiki huenda haifiki hata robo katika Miji (namaanisha Boma la Ukoo lenye muunganiko wa familia kadhaa zenye kushare wazazi) niliyoweza kuipitia, zaidi ya 80% ya wauhusika hawakurudi kwao. Kuna maboma kadhaa yalikuwa yamefungwa kabisa, hakuna aliyerejea kabisa!

2. Sio kweli kuwa kila jamii ya Kichaga kipindi hiki huweza kusheherekea Christmass kwa shamrashamra. Nimeweza kukutana na familia za Wachaga Waislamu (hasa maeneo ya Machame na Kibosho), jamii zingine maskini sana na familia nyingi zisizoeleweka nk, hao hawana muda wowote na sherehe za Krismasi. Wako busy na maisha yao mengine.

3. Misafara mingi ya magari binafsi yaliyokuwa yakielekea uchagani yalikuwa ni magari ya familia chache zenye uwezo mkubwa kifedha au maisha ya mbwembwe. Kifupi sana, magari yale huenda yanaakisi 10% tu ya familia za Kichaga. Wengi wa wachaga wamekuja kula sikukuu kwa kutumia usafiri wa umma bila kujali kama wanamiliki magari mijini au hawana kabisa magari.

4. Sehemu kubwa ya miji (maboma) zimejengwa kwa nyumba za kawaida kabisa na nyingine ziko kizamani japokuwa zinaonekana kutunzwa vyema. Zaidi ya 90% sio nyumba za gharama kubwa au kisasa. Pia niliweza kukutana na nyumba duni au mapagala yanayoonekana kutelekezwa lakini nikakuta kuna watu wanakaa!
Kibosho ulikuwa maeneo gan chief
 
Karibu Machame

20201228_083930.jpg
20201228_083219.jpg
 
Kibosho ulikuwa maeneo gan chief
Maeneo kadhaa, mwenyeji wangu ameniambia yanaitwa Kindi, Umbwe, Kibosho secondary, shirikani (eneo la Kanisa Katoliki lenye hospitali, kanisa la kihistoria na chuo cha uuguzi) nk.
 
Hapo point namba 2. Wachaga waislamu. Na jamii nyingine. Hiv ww wachaga waislam washerekee christmass inawahusu?

Pili umetembea sehem ndogo ya moshi ambayo si sehem ya shambea shambra
.
mkuu mwakani uende hapo ndipo kuna wachaga hasa
 
mkuu mwakani uende hapo ndipo kuna wachaga hasa
Niende marangap? Haal machame ina mchanganyiko sana na makabila mengine. Wachaga og wako rombo, wako marangu, wako mwika,wako oldmoshi vijijini. Wako kibosho. Huko bado wana practise mila za kichaga
 
Maeneo kadhaa, mwenyeji wangu ameniambia yanaitwa Kindi, Umbwe, Kibosho secondary, shirikani (eneo la Kanisa Katoliki lenye hospitali, kanisa la kihistoria na chuo cha uuguzi) nk.
Huijui kibosho chief. We umepitishwa njian kumbe.
 
Niende marangap? Haal machame ina mchanganyiko sana na makabila mengine. Wachaga og wako rombo, wako marangu, wako mwika,wako oldmoshi vijijini. Wako kibosho. Huko bado wana practise mila za kichaga
Sasa wanataka tuache mila na tamaduni zetu? Ngoja nikaulizie kwanza mbuzi zangu nachinjiwa lini[emoji23][emoji23]
 
Huijui kibosho chief. We umepitishwa njian kumbe.
Kote kapitishwa road ndugu yangu. Nimempa offer nimtembeze kwetu na mbuzi tutamchinjia kabisa kama kumkaribisha mgeni. Halafu niambie mtu utaenjoy vipi sikukuu ambayo si Imani yako? Huyu mpemba sijui mngazija atafurahia vipi sikukuu ambayo si yake maana naamini ni muislamu?

Pili... kule watu wote wanajuana ndo maana wanaijua na kuifuragia hiyo sikukuu... yeye anapita barabarani huko hakuna anayejuana nae atasemaje sikukuu ikonove rated?

And actually mwaka huu majority hatujaenda. Hawajui kama sisi ni kabila la 2 kwa ukubwa Tz? Hatuwezi enda wote. Hatujaenda kwa kukosa nauli bali mambo yamekua mengi. Nafasi kwa ufinyu wake
 
Hapana, sijatembea Kilimanjaro yote bali baadhi ya maeneo ya wachaga katika wilaya za Rombo, Moshi vijijini na Hai. Na ziara yangu imeshachukua siku tatu sasa.

Sina takwimu kamili bali nimefanya observation (general overviews). MwanaJF mwingine anaweza kuja na utafiti mpana zaidi.
Acha upuuzi mtu aje na utafiti wa kijinga unatusaidia nini huku jf,
Wewe na husda za kipuuzi unataka kuwaambukiza wengine huo upuuzi wako
 
Niende marangap? Haal machame ina mchanganyiko sana na makabila mengine. Wachaga og wako rombo, wako marangu, wako mwika,wako oldmoshi vijijini. Wako kibosho. Huko bado wana practise mila za kichaga
Kwa hiyo huo mchanganyiko Una kasoro gani? Ok nikfahamishe,; kulikuwa na mashamba makubwa ya kahawa na katani. Kibo Estate, kikafu, kitifu, boloti, Kware, mbosho, Lbo, weruweru na nkwansira. Manamna Waliokuwa wanahudumia hayo mashamba walitoka Kigoma, tabora, Singida, usukumani na Warangi. Wakaja na Dini ya Kiislaam, wakajenga misikiti na kuoa Wachaga Wakristo wakasilimu. Wachaga waliachwa kuhudumia Vihamba vyao na si kuwa Manamna ya Wazungu.
 
Mbee.. ngikundi ngikuoliye wari. Watana mbe[emoji23][emoji23] dhekana na isembo loo.
 
Back
Top Bottom