CHRISTMASS ni ya kina Pope Julius I au ni yetu sisi na Yesu wetu?

CHRISTMASS ni ya kina Pope Julius I au ni yetu sisi na Yesu wetu?

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2019
Posts
3,862
Reaction score
6,438
wasaalam, wakuu

Ninaandika haya huku , nikijua nitapingwa zaidi kuliko kuungwa mkono.

Naandika huku nikitaraji pia dhihaka na kashfa kuliko majadaliano yenye mapenzi mema

Naandika sio kwa vile naelewa athari za upagani katika dini na madhehebu yetu

Naandika kwa sababu naelewa ,maafa ya kibinaadamu ambayo wapagani na nyingi zao mila na desturi ambazo zimeacha nyuma katika madhehebu yetu na dini zetu.

Naandika kwasababu pia mimi sio wa kwanza kuandika hapa na wala si wa mwisho kuandika haya.

Naandika kwasababu nilitamani kuandika hiki na nmeandika.

Tumezoea makala za namna hii kwingi tuendako katika majira haya ,lakini kila zama zinavyozidi kujongea taswira mpya inajengeka ndivyo navyo tunazidi kukumbushana kwa hekima njema

Basi

Kama utauliza popote duniani kuhusu 'christ mass' majawabu yake yatakuwa ni sikukuu ya kuzaliwa bwana yesu....lakini moja kwa moja hilo sio jibu la kweli la swali hilo ......kama ungeli ipata na ungelirejelea vitabu vya history ya kale na biblia kwa ujumla ungelipata sababu ya kupinga na kupangua kumbukizi hii ya mazazi ya kiongozi na mwokozi yesu kristo.
FB_IMG_16085315556034186.jpg

Katika injili zote haijapata kuwepo thibati, ya bwana YESU eti ya kwamba alizaliwa majira yapi?? na tarehe zipi.

Na mpaka ilipofikia mwaka 349 AD dunia haikuwahi kuwa na sikukuu ya kusherekea mazazi ya bwana yesu.

Kila ifikapo tarehe 25 Disemba watu husherekea kuzaliwa kwa bwana yesu na Wengi wetu kwa pumbao letu tulilo nalo tunaamini hiyo ni siku haswa bwana mwokozi alipoletwa duniani na mama yake, mama mwema , mtakatifu, mkarimu, mweupe wa moyo na nafsi alietakasika kabisa MARIAMU hata ALLAH (s.w) katika QUR'AN akamtaja na kuwa mwanamke pekee aliyetajwa katika maandishi hayo matukufu Sio kumtaja tu LaHashaa! ALLAH (s.w) akampa sura yake kabisa Mama wa Yesu (amani za mwenyezimungu ziendelee kuwa naye huko aliko)

Lakini ni kweli bwana YESU alizaliwa 25 disemba???
FB_IMG_16085291331392739.jpg

Ninajua kwamba bwana Yesu Hakuzaliwa mwishoni mwa mwaka,, kama ni hivyo sitakuwa na mashaka nikikuambia ya kwamba ninajua pia bwana yesu alizaliwa katikati ya mwaka wa 6 kuelekea wa 5 B.C.

Thibati hiyo ya Bwana Yesu kuzaliwa Katikati ya mwaka wa 6 kwenda wa 5 BC Pia imetambulika na Biblia ijulikanayo kwa jina la
Life Application Study Bible , katika ukurasa wa A20 .

Lakini hata maelezo yameeleza kwa ufupi kuzaliwa kwa bwana yesu na yanatosha kuonyesha 25 disemba sio sikukuu ya kuzaliwa bwana


Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, kwa msichana mmoja bikira aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. Malaika akamwendea, akamwambia, “Salamu, ewe uliyejaliwa neema na Mungu! Bwana yuko nawe!” Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: Maneno hayo yanamaanisha nini? Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yesu..... LUKA 1:26-31

Mafundisho hayo yanagongea msumari , kwamba habari za kupokea taarifa za mimba kwa Mariamu kulitokea mwezi wa sita ,na kama ujuavyo mwezi huo kwa jamii za kale nyingi hata zama za sasa ni mwezi wa katikati ya mwaka.....
wasomi wa histori wengi wamejaribu kuonyesha mwezi wa saba napo ndipo Mama mariamu alichukua mimba yake na akazaa kwa utimilifu pasi na kasoro yoyote.... kwa maana mtoto hakuwa na kasoro yoyote ya muda.

ikawa katika kukaa huko siku zake za kuzaa zikatimia ,akajifungua mtoto wake wa kwanza wa kiume, akamvika nguo za kitoto, akamlaza horini kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni. LUKA 2: 6-7

Pasi na shaka bwana yesu alizaliwa katika mda timilifu kabisa

Tutake nini tena??? tuombe tujue na tusijue


pia ukirejelea mwanzo na takwimu hizo, hata mwaka wa kwanza A.D bwana Yesu tayari alikuwa na umri wa miaka mitatu na Nusu,, Na hapo pia panakinzana na ile dhana inayosemwa na wengi kuwa Bwana Yesu alipozaliwa ndipo miaka ikaanza kuhesabiwa....(ni vyema ukaingia mtandaoni kupata taarifa kwa uyakinifu zaidi)

POPE JULIUS WA I

Hilo fundisho kuhusu Bwana Yesu kuzaliwa tarehe 25, ya mwezi wa Disemba ni POPE shupavu wa roman aitwae Julius I alitangaza rasmi kuwa tarehe 25 Disemba ndiyo itakuwa siku ya kusheherekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo.......Pia hii ilikuwa siku ambayo wapagani wa walikuwa wakisherehekea kuzaliwa kwa Mungu wao, mungu jua na mwanzo wa majira ya michepuo ya mimea basi JULIUS akaingiza siku hiyo kwa minajili ya mungu wao wapagani wa rumi ili afanyiwe matukuzo na kuwatia katika makufuru wana wa Adamu
Screenshot_20201220-140522.png

Katika majira hayo hayo pia kulikuwa na sikukuu ya wapagani wa Kirumi inajulikana sana kwa jina la “Roman Saturnalia” ambayo pia Waroma walikuwa wanampa heshima mungu wao SATURN, ambaye wao walikuwa wanamwabudu....Mungu huyu ni sayari ya SATANI
Waroma walikuwa wanasherekea sherehe hiyo kila tarehe 19 ya mwezi wa Disemba na ilikuwa inaadhimishwa kwa kufulululiza kwa siku saba hadi tarehe 25 ya mwezi huo wa Disemba ndipo maadhimisho ya siku kuu hiyo yalipohitimishwa.
Screenshot_20201220-142944.png

Pia ilipofika miaka ya elfu na miamoja (1100s )AD Warumi walitangaza kuwa sikukuu (christmass) hii ni ya kidini na wakaweka ulazima pasi na shuruti kwa mataifa yaliyo chini ya makoloni yake kuifata na kutenga fedha kwa ajili ya sikukuu hii....pasi hiari

Kuna kiongozi wa ukatoliki wakati huo mjanja mjanja mmoja bwana nicholas....alifanikiwa kuzishawishi nchi nyingi za ulaya kuipokea sikukuu hii kama ndiyo sikukuu ya kidini na kitaifa ,, umashuhuri wa christmass ukaongezeka na uliendelea kuwa mkubwa miaka ya 1500 AD.

Na hapo ndipo uliponza kujitokeza mgawanyiko mkubwa mno katika ukristo,,jambo lililopelekea kuanzishwa kwa madhehebu mengi ya kikristo ya kiprostentanti, mpaka sasa yanakadiriwa kufikia takribani 3000..

Lakini mgawanyiko huo wa madhehebu ulisaidia sana kufichua mambo mbalimbali na kutoa uhuru wa mafundisho mengi mengi na hapo wakristo wengi walipata mwanya wa kueleza namna na maana ya christmass ni UPAGANI tena ni sherehe ya kutungwa.

Haya mafundisho yalifanya UINGEREZA kuiondoa sikukuu hiyo mwaka 1600 AD, kama sikukuu yake ya kitaifa na kidini hata katika makoloni yake yote.
FB_IMG_16085290771590828.jpg

Hata hivyo tamaduni ya sherehe hizi zilirudi kwa sura ya pili ya kikristo.....ambapo mtindo wa kusherekea wa sasa uliambatana na kupambwa kwa miti ya krismass katika makanisa na kutumina kadi za salam zilizosheheni maandiko ya biblia takatifu na maadhimisho yakazidi kupamba moto kila mwaka hata sasa katika zama zetu za kina SANTA CLAUS
FB_IMG_16085290712658851.jpg


DA'VINCI XV
 
Sasa shida hapo iko wapi?? Kama warumi walikuwa wanaabudu na kusherehekea sikukuu ya Mungu jua tar. 25.. kisha Papa akaona huo ni upuuzi na ni afadhali hiyo siku tumsherehekee Mungu wa kweli, hapo ubaya upo wapi? Maana siku zote na tarehe ni vya Mungu... Inaonekana kinachokusumbua wewe ni siku hiyo ya tarehe 25... Ila elewa kuwa kwa wakristo suala kubwa sio tarehe wala siku bali ni kuzaliwa kwa mwokozi.. na hata pasaka ni hivyo hivyo ishu sio siku wala saa bali kufa na kufufuka.
 
Sasa shida hapo iko wapi?? Kama warumi walikuwa wanaabudu na kusherehekea sikukuu ya Mungu jua tar. 25.. kisha Papa akaona huo ni upuuzi na ni afadhali hiyo siku tumsherehekee Mungu wa kweli, hapo ubaya upo wapi? Maana siku zote na tarehe ni vya Mungu... Inaonekana kinachokusumbua wewe ni siku hiyo ya tarehe 25... Ila elewa kuwa kwa wakristo suala kubwa sio tarehe wala siku bali ni kuzaliwa kwa mwokozi.. na hata pasaka ni hivyo hivyo ishu sio siku wala saa bali kufa na kufufuka.
Mwanzo nlipata ugumu ,kidogo ila nikakumbuka yawezekana utakuwa una simu janja ambayo inakuwezesha kupata taarifa mtandaoni , labda kwa kukusaidia ungeanza kumsoma kwanza julius I kwa undani,baada ya hapo malizia na costantine Augusto kama utapenda zaidi utawasoma na hao kina nicholas.

nasikitika kwanini??? sikumzungumzia POPE julius I kwa undani
 
Katika injili zote haijapata kuwepo thibati, ya bwana YESU eti ya kwamba alizaliwa majira yapi?? na tarehe zipi.

Kila ifikapo tarehe 25 Disemba watu husherekea kuzaliwa kwa bwana yesu na Wengi wetu kwa pumbao letu tulilo nalo tunaamini hiyo ni siku haswa bwana mwokozi alipoletwa duniani na mama yake,i
Hakuna hata kiongozi wa dini mmoja anayeshupalia tarehe halisi ya kuzaliwa Yesu Kristu, wote wana akili timamu na wanaiita kumbukumbu ya kuzaliwa Yesu Kristu. Mjadala huu ulishatolewa ufafanuzi sana ila kila inapokaribia sikukuu ya Noeli, hapakosekani jamaa atakayeanzisha uzi humu kuhoji tarehe halisi ya kuzaliwa Kristu. Ili kufupisha mjadala na kuufunga uzi, ni kwamba hata wanaosherehekea kuzaliwa Yesu Kristu wanatambua kwamba hiyo ni kumbukumbu, labda kama hoja yako iwe kwamba hawapaswi kusherehekea kabisa hata kumbukumbu.
 
sidhani hata kama umesoma paragraph zote
umeandika gazeti, nimeangalia utangulizi wako, jinsi ulivyoanza kwa kujihami, nikachagua paragraph inayozungumzia tarehe halisi, au kama ulivyoiita tarehe haswaa
 
basi tusubiri uo mchele ijumaa
Yeah, tusubiri tu. Sidhani hata wewe kama una uhakika na tarehe uliyoambiwa kwamba ndiyo tarehe yako ya kuzaliwa, maana nina uhakika wakati unatoka tumboni haukuwa na akili za kutambua tarehe. Lakini bila shaka unacho cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha mpiga kura na kitambulisho cha taifa, na vyote vimewekwa tarehe ya kuzaliwa kwako. Imebidi tu uendane nayo kama kumbukumbu halisi, ila hauna uhakika
 
LUKA 1:26-31
Mafundisho hayo yanagongea msumari , kwamba habari za kupokea taarifa za mimba kwa Mariamu kulitokea mwezi wa sita ,na kama ujuavyo mwezi huo kwa jamii za kale nyingi hata zama za sasa ni mwezi wa katikati ya mwaka.....
Mkuu, ili utafsiri biblia, unahitaji maarifa mengine pia, walau usome level fulani ya elimu. Biblia imeandika mwezi wa sita, kwa kiingereza sixth month, wala haijaandika mwezi Juni

26 And in the sixth month the angel Gabriel was sent from God unto a city of Galilee, named Nazareth,
 
Mkuu, ili utafsiri biblia, unahitaji maarifa mengine pia, walau usome level fulani ya elimu. Biblia imeandika mwezi wa sita, kwa kiingereza sixth month, wala haijaandika mwezi Juni

26 And in the sixth month the angel Gabriel was sent from God unto a city of Galilee, named Nazareth,
kwahyo Juni sio mwezi wa sita?? Unahisi hivo au unajua hivo?? Au unapalangana kutafuta sababu ya kutetea upagani wa papa?
 
Thibati hiyo ya Bwana Yesu kuzaliwa Katikati ya mwaka wa 6 kwenda wa 5 BC Pia imetambulika na Biblia ijulikanayo kwa jina la
Life Application Study Bible , katika ukurasa wa A20 .

Hicho ni kitabu gani unachokifanyia reference?
 
kingine nimegundua umeanza kusoma sasa....... keywords zote ziko hapo ni wewe na internet yako mkuu
Nilikwambia ni gazeti, wachache watamudu kusoma lote kwa mkupuo. Turudi kwenye swali, Hicho ni kitabu gani unachokifanyia reference?
 
Back
Top Bottom