CHRISTMASS ni ya kina Pope Julius I au ni yetu sisi na Yesu wetu?

Biblia haituelekezi kusherehekea birthday ya Yesu, lakini Yesu mwenyewe alituagiza kukumbuka kifo chake yaani kusherehekea Pasaka, kwani hili ndilo tendo lililoleta ukombozi wa mwanadamu, kwa hiyo wanadamu wana ukaidi fulani wa kufanya mambo ambayo hawakuagizwa na kuacha yale waliyoagizwa, cha muhimu ni kufuata maagizo ya neno la Mungu tusifanye mambo kwa mkumbo kwa sababu siku ya mwisho kila mtu atajitetea mwenyewe, yaani mbele za Mungu huwezi kumsingizia kiongozi wako wa dini utaulizwa ulijua kusoma na kuandika utajibu ndio, ulisoma maandiko yanasemaje? basi.
 
sahihi .... hapa ndio inakuja ile concept ya kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe
 
Mtoa mada unaweza ukawa sahihi kwa upande mmoja lakini ukishindwa kuelewa maana ya maneno yaliyoandikwa kwenye Biblia itakusumbua kwa kushika kamstari kamoja tu na unenda nako utafiki fimbo ya kuulia nyoka. Katika kitabu cha Luka mlango wa kwanza kuanzia mstari wa 24 inaeleza mpaka hapo uliposhikilia wewe kinachoelezwa ni umri au muda wa mimba ya Elizabeti mke wa Zakaria siyo miezi ya Januari, Juni kama unavyotaka wewe. Naomba kunukuu.
24. Hata baada ya siku zile mkewe Elisabeti alichukua mimba akatawa miezi mitano, akisema
25. Hivi ndivyo alivyonitendea Bwana katika siku zile alizoniangalia ili kuniondolea aibu yangu mbele ya watu
26. Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti
;
;
;
36. Tena tazama, jamaa yako Elisabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa;

Ni kweli kwamba tarehe rasmi ya kuzaliwa kwa Yesu haijaandikwa popote kwenye Biblia lakini si kwamba mimba yake ilitungwa mwezi wa sita (Juni) bali mwezi wa sita ya mimba ya Elisabeti (Mama wa Yohana Mbatizaji).
 
We utabadirishaje siku yako ya kuzaliwa mfano umezaliwa tarehe 23 mwez wa 5 halafu usherekee siku ya kuzaliwa tarehe 8 mwez wa 6 hiyo ni akili kweli au ukili huoni hapo kwamba unakua unasherekea wrong date
 
C H R I S T M A S S"

Je! ni halali kusherehekea sikukuu ya christmass kwa mujibu wa maandiko? sasa sikia hii, kwanza kabisa hakuna neno krismas kwenye biblia, lakini je ni kweli Yesu Kristo alizaliwa tarehe 25 mwezi wa 12? jibu ni hapana, bali siku hiyo alikua anaachiliwa mfungwa toka gerezani. soma yeremia 52;31. Je! kuna mtakatifu yoyote aliyesherehekea sikukuu ya kuzaliwa? Jibu ni hapana, bali waliosherehekea sikukuu ya kuzaliwa ni wapagani, na katika kusherehekea kwao walitoa kafara za watu. Mtu wa kwanza ni farao, ambae katika kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa, aliua kwa kumtundika mkuu wa waokaji. Soma mwanzo 40;20-22. Mtu wa pili ni herode, ambae nae katika kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa aliuwa kwa kumchinja yohana mbatizaji, soma mathayo 14;6 na 10. Kupitia hayo hakika kabisa krismas sio tu sikukuu ya kipagani bali ni sikukuu ya kishetani. Mwenye sikio na asikie neno hili.

#MARANATHA
 
We utabadirishaje siku yako ya kuzaliwa mfano umezaliwa tarehe 23 mwez wa 5 halafu usherekee siku ya kuzaliwa tarehe 8 mwez wa 6 hiyo ni akili kweli au ukili huoni hapo kwamba unakua unasherekea wrong date
[emoji3][emoji3]ukisoma hiyo injili ya luka utaona kuwa huo mwezi wa sita unaozungumziwa ni umri wa mimba ya elisabety.. wala sio Mimba ya Maria...soma toka mwanzo utaona vema.. usikariri mstari mmoja pekee...
 
kwani hizi tarehe ama siku zina athari gani kiroho ???....

Au zinanifanya nivunje sheria gani ya Mungu au kwa maneno mepesi inanifanya nitende dhambi ya aina gani ??...

Je, nikiamua kutenga siku hata ya birthday yangu kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu (Kukumbuka mwanzo wasafari ya ukombozi) au Kifo cha kristu. Nitakuwa nimefanya Kosa gani yaani mnamaanisha Mungu ataangalia zaidi siku kuliko sincerety na kumkiri kwangu ???...
 
Shida ni background ya hii tarehe ya kumbukumbu..nadhani hapa ndipo hoja kuu iliposimamia..

#MaendeleoHayanaChama
 
Je ni maagizo kwa mujibu wa maaandiko? Au ni matakwa yako binafs..?

#MaendeleoHayanaChama
 
Umesema ukweli [emoji28][emoji28][emoji120]

Sent from my ACCESS55 Pro using JamiiForums mobile app
 
Christmas is not a Biblical festival. Hii ni sikukuu kama siku nyingine za kihuni duniani, Ni kama siku ya kuwakumbuka ma kayaman wote
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji28]
 
Ujuaji mwingi mbele kiza. Samahani sana ndugu yangu.
 
Jitafakari mkuu,,

Dini sio ushabiki..jamaa ameleta hoja fikirishi sana..

Bado hujachelewa,

Chukuwa hatua.
 
Hoja ya msingi ya mleta uzi ni hii tarehe kuingiliana na tarehe ya kusherehekea MUNGU wa jua,,na sio bwana aliye mbinguni.

Kama ni kumbukumbu kwann zisiwe mwezi wa 6..

Mwezi ule malaika alipomfata bikira maria?

Au kwanini usiwe miezi tisa baada ya bikira maria kupata minba ya Yesu.?

Wacha kujipa moyo kwenye kutetea uovu.
 
Christmas is not a Biblical festival. Hii ni sikukuu kama siku nyingine za kihuni duniani, Ni kama siku ya kuwakumbuka ma kayaman wote
Ni siku gani hiyo boss na ni kina nani hao ma kayaman
 
Hapa unaweza ukawa sahihi na unaweza ukawa wrong pia... maana wakristo wote wanategemea kalenda hiyo hiyo inayotambua JUNE kama mwezi wa sita!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…