CHRISTMASS ni ya kina Pope Julius I au ni yetu sisi na Yesu wetu?

Suala la kusherehekea Krismas ni suala la MAPOKEO; huu ndio mwanzo wake kwani hakuna, nasema tena, hakuna andiko lolote kwenye BIBLIA linalozungumzia hii sikukuu, tofauti na PASAKA ambayo Yesu Kristo, Aliye Hai ametuagiza tuikimbuke (hata kama ni kupitia kwa Wayahudi - kwenye Agano jipya!). Zaidi ya hapo, wajanja wakaifanya iwe na mtizamo na mwelekeo wa kibiashara zaidi na watu wengi, hata Wakristo, wakaingia mkenge huu. Twende na maandiko ili tusikumbwe na mafundisho ya UONGO na mwisho wake tuikose Mbingu jamani!
 
SIna uhakika tofauti ya Pasaka (kama kumbukumbu ya ufufuo wa Yesu) na Krismasi unapata wapi? Katika Biblia sijawahi kuona sikukuu ya Pasaka ya Kikristo (usichanganye na ile sherehe ya Pasaka ya Kiyahudi).
Zote mbili ziliundwa kwa hiari yao na waumini ili kukumbuka ukweli fulani wa imani nyao.
 
Tulia na urudi kwenye maandiko au ufanye consultation na viongozi wako wa dini/imani/dhehebu juu ya haya masuala mawili. Labda baadaye nikitulia naweza kukupa maandiko kutoka kwenye Biblia Takatifu juu ya PASAKA.
 
Tulia na urudi kwenye maandiko au ufanye consultation na viongozi wako wa dini/imani/dhehebu juu ya haya masuala mawili. Labda baadaye nikitulia naweza kukupa maandiko kutoka kwenye Biblia Takatifu juu ya PASAKA.
Karibu sana. Ila ukumbuke tunajadili sikukuu ya Wakristo siyo ile Pasaka ya Kiyahudi (=Pessackh). Maandiko kuhusu pasaka ni mengi. Hakuna kuhusu sikukuu ya Kikristo.
Hilyo ndilo swali tunalojadili.
 
fanyeni hivi kwa kunikumbuka.....-Jesus

Anyway.. kina babu chrismas na wale Sungura wa Pasaka waliingiaje kwenye ukristo?
 
Mzee, je wewe ni mzuri kiasi gani kwenye Bibilia? Bible imetaja Sikujua za kuzienzi
 
Kumbukumbu 16:1 “Utunze mwezi wa Abibu, ukamfanyie pasaka Bwana, Mungu wako, kwa kuwa ilikuwa ni mwezi wa Abibu alipokutoa Misri usiku Bwana; Mungu wako.

2 Nawe umchinjie pasaka Bwana, Mungu wako, katika kundi la kondoo na la ng’ombe, mahali atakapochagua Bwana apakalishe jina lake”.
 
fanyeni hivi kwa kunikumbuka.....-Jesus

Anyway.. kina babu chrismas na wale Sungura wa Pasaka waliingiaje kwenye ukristo?
"Fanyeni hivi kwa kunikumbuka" - hii si kuhusu sikukuu yoyote, ni kuhusu aina ya ibada ya ekaristia (chakula cha Bwana). Sungura wa Pasaka, mayai ya Pasaka ni desturi za baadaye ya kieneo zilizoanza Ulaya miaka 1500 baada ya Kristo.
krismasi ni sikukuu ambayo tuna habari zake mapema, baada ya mwaka 300 hivi.
 
Nilivyosema pale juu: Pasaka ya Kiyahudi (kufuatana na aya unyotaja; Kiingereza "Passover") ambayo ni kumbukumbu ya kutoka kwa Wanaisraeli katika utumwa nchini Misri ni jambo tofauti na ile Pasaka ya Kikristo inayokumbuka habari ya ufufuo wa Kristo.

Sababu ya kuwa na majina ya kufanana kwa Kiswahili (si kwa Kiingereza na lugha nyingine! - Passover as Jewish holiday -Easter as as Christian holiday, hakuna anayechanganya hizo) ni kwamba Yesu alikamatwa na kuhukumiwa baada ya kusheherekea sikukuu ya Kiyahudi.
 
Acheni ujinga kwa nini isitafutwe sherehe kwenye mwezi wa mimba au tuhesabu miezi 9 ndio itafutwe siku badala ya kupaka asali kitu kilichooza?
 
Tahere siyo issue, ila ukweli ni kwamba yesu alizaliwa na alivyozaliwa watu walisheherekea.

Mimi bibi yangu hajui tarehe ya kuzaliwa ila kila ikifika 01 january huwa tunasheherekea birthday yake.
 
Samahan Kwa kuchelewa,hv jina halis jamaa alilopewa na Maria Ni lipi Jesus Christ,Yesu,Masia au...........
 
Hata kalenda unayotumia ni kalenda ya Papa. Inaitwa Gregorian Calendar. Ya papa Gregorian

Sasa unaonaje ukaamua kuachana na matumizi ya kila kinachotoka kwa papa ikiwamo kalenda?
 
Hoja yako ni nini sasa? nimeandika kwamba kuhusu tarehe mwezi yawezekana ukawa sahihi lakini ulichokielewa kwenye Biblia ilikuwa ndiyo hoja yangu.
 
Kweli kabisa haiwezekani akazaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…