Chuki inakudhuru wewe mwenyewe

Chuki inakudhuru wewe mwenyewe

Mzee siku zote Sifu anayekukimbiza pia ....

Bila Huyo kukuchukua usingekuwa na ubunifu na Akili ya kiupambanaji kukuijia mwilini mwako ...

Yule anayekuchukuia na yeye kuna watu wanamchukia na anapambana ....circle ina endelea hivo ...na Dunia ndio ilivo
😂😂 tumepata maoni yako chief
 
Nelson mandela anasema hivi

"Chuki ni sawa na kunywa sumu huku ukitegemea itamuua MTU mwingine"

Kuhusu kuwa na chuki na kuchakaa mwili hii ni fact

Ila kuhusu kuwa na chuki na kuwa mwembamba hii ni opinion.

Chuki hutokana zaidi na kuwa na migogoro ya nafsi inner conflicts.
Ambayo haipo solved.

Interpretation- kutafsiri mambo
Fixed mindset
Scarcity mindset

Hayo mambo juu yanaweza kukufanya uchukie serikali, MTU ,watu n.k

Resentment = CHUKI ni mental illness
 
Utamsikia mtu anasema "hakika namchukia mtu fulani yaani sitaki hata kumwona "

Huyu hajui kuwa anajidhuru yeye mwenyewe,,, kwanza anaishi na nguvu hasi ambazo zina mwangamiza na kumtafuna yeye binafsi.

Hivi umeshawi kuwaona watu ambao wana roho ya korosho au kwa maana nyingine roho mbaya, hawa mara nyingi huwa wamenyauka kutokana na roho mbaya,, si kila mtu mwembamba ana roho mbaya hapana, ila wembamba wa watu hawa huwa tofauti sana kwakuwa wanatafunwa na nguvu hasi nyingi hivyo hukosa hata nuru.

Wewe unayeendekeza chuki tambua unajidhuru wewe mwenyewe kwakuwa kila utapokutana na yule unaye mchukia basi chuki inadhidi na kuzalisha kemikali mwilini mwako ambazo zinakudhuru wewe mwenyewe, na istoshe unakosa raha na amani moyoni mwako.

Na kibaya zaidi huyo unayemchukia haathiriki kama wewe kwakuwa yeye amekubali kuwa unamchukia na anaendelea na maisha yake,,, unabaki wewe unajishughulisha kwa kutaka kumuona anaharibikiwa, anaanguka na kupata madhira mbali mbali na kuanguamia,,, usichojuwa baraka zinatoka kwa Mwenyezi Mungu na humbariki amtakaye bila hesabu

Jifunze kuishi bila chuki hata vitabu vya dini vinasisitiza sana kusameheana na kugawa love kwa binadamu wenzetu.

Kwani asiye msamehe mwanadamu mwenzake hata huyo aliye juu zaidi na ambaye ni mkuu hatokusame pia.

Upendo ni nuru, upendo ni amani, upendo ni furaha, kuwa huru kwa kuepukana na chuki,,, siku zote chagua tabasamu.

Ni hayo tu!
Amen amen amen amen amen amen amen
 
Wako na wilaya mbili. Same na Mwanga. Hapo Same ndio uchawi unlala hapo! Kama hujipendi hebu kamlipue MTU anayelima ule mmea ambao Ni halali Kenya lkn huku Ni madawa ya kulevya.
Kwa hio huko ndio kuna ROHO mbaya?
 
Utamsikia mtu anasema "hakika namchukia mtu fulani yaani sitaki hata kumwona "

Huyu hajui kuwa anajidhuru yeye mwenyewe,,, kwanza anaishi na nguvu hasi ambazo zina mwangamiza na kumtafuna yeye binafsi.

Hivi umeshawi kuwaona watu ambao wana roho ya korosho au kwa maana nyingine roho mbaya, hawa mara nyingi huwa wamenyauka kutokana na roho mbaya,, si kila mtu mwembamba ana roho mbaya hapana, ila wembamba wa watu hawa huwa tofauti sana kwakuwa wanatafunwa na nguvu hasi nyingi hivyo hukosa hata nuru.

Wewe unayeendekeza chuki tambua unajidhuru wewe mwenyewe kwakuwa kila utapokutana na yule unaye mchukia basi chuki inadhidi na kuzalisha kemikali mwilini mwako ambazo zinakudhuru wewe mwenyewe, na istoshe unakosa raha na amani moyoni mwako.

Na kibaya zaidi huyo unayemchukia haathiriki kama wewe kwakuwa yeye amekubali kuwa unamchukia na anaendelea na maisha yake,,, unabaki wewe unajishughulisha kwa kutaka kumuona anaharibikiwa, anaanguka na kupata madhira mbali mbali na kuanguamia,,, usichojuwa baraka zinatoka kwa Mwenyezi Mungu na humbariki amtakaye bila hesabu

Jifunze kuishi bila chuki hata vitabu vya dini vinasisitiza sana kusameheana na kugawa love kwa binadamu wenzetu.

Kwani asiye msamehe mwanadamu mwenzake hata huyo aliye juu zaidi na ambaye ni mkuu hatokusame pia.

Upendo ni nuru, upendo ni amani, upendo ni furaha, kuwa huru kwa kuepukana na chuki,,, siku zote chagua tabasamu.

Ni hayo tu!
Very well said
 
Back
Top Bottom