Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Habari ya wakati huu ni matumaini yangu nyote mpo salama.
Moja kwa moja niende kwenye mada husika.
Najua binadamu tuko tofauti lakini ningependa kupata comments tofauti tofauti kujua nini hasa hupelekea. Chuki, visasi, roho za kutendeana ubaya, malipizi, na mengineyo yasiyopendeza huletwa na nini?
Je, ni kwakuwa hujui na unaonekana mzigo?
Je, unajua zaidi yao na unaonekana kama tishio?
Au ni basi tu mtu anaamua kukuchukia bila sababu ya msingi na kukuombea kila uchwao ukumbwe na baya?
Ninakaribisha maoni.
Shimba ya Buyenze , Mshana Jr Watu8 , Omerta, @Da’Vinc , na wapendwa wengine karibuni.
Umemaliza kila kitu hapa...Jambo la kwanza, roho mbaya mtu huzaliwa nayo, na huwa inasubiri majira, nyakati na mazingira sahihi ili iweze kuanza kufanya kazi...
Binafsi katika kumtumikia kote mkoloni sijawahi kukutana na watu wa namna hiyo, isipokuwa nimekuwa nikipata kusikia visa hivyo toka kwa watu wa karibu...
Sababu ambazo nimekuwa nikizisikia huwa ni tofauti tofauti, lakini zote ni matokeo ya mtu kuwa na roho mbaya 'roho nyeusi'...
1. Ubinafsi - Hawa ni wale watu wenye umimi, kwamba kila kizuri kiwe chao na vibaya viwe vya wengine
2. Ufukara - Kuna watu ambao maisha yao yamegubikwa na ufukara wa mali, hivyo hujawa na chuki pale wanapoona mtu fulani yupo kwenye nafasi ya kupokea mkate mnono zaidi yao, au hata maisha yake nyumbani ni ya juu kuwazidi katika mali alizonazo
3. Kukosa weledi - Kuna watu waliopata vyeo au nafasi kwa ngekewa tu na wala sio kwa uwezo wa kiakili au taaluma, sasa kule kutokujiamini kwamba mtu anaweza akapokwa nafasi yake hufanya ajenge chuki kama njia ya kujilinda
4. Ukabila - Kuna maofisi ambayo watu wa kabila fulani ni kama wamechanjiwa kuwa wao ni wa ofisi hiyo tu, ikitokea wewe mwenyeji wa mkoa mwingine umeajiriwa au kupangiwa hapo, cha moto utakuona
5. Tofauti za kimaumbile/hulka/ulimbwende na utanashati - Imezoeleka kusikika kuwa watu wafupi huwa wakorofi sana, dhana hii ipo pia makazini ambapo kuna watu hukosa kujiamini kutokana maumbile yao, hujiona sii warembo au watanashati au hujiona wana kasoro fulani za kimaumbile ambazo zinawafanya wamuone mtu fulani kawazidi
6. Tofauti za kiimani - Kama ilivyo tofauti za kimaumbile, hata imani nayo huwa ni chanzo cha chuki baina ya mtu na mtu. Kuna ofisi ambazo imani fulani ya dini ina nguvu kuliko nyinginezo.
Pia kuna watu ambao huwa ni washirikina, hupelekea kuwachukia wale walio wacha Mungu.
7. Kuwa sehemu isiyo sahihi wakati usio sahihi - Isijekuwa pia upo mahali pasipo sahihi kwako iwe ni idara, ofisi au kitengo kiasi kwamba unazuia 'deals' za watu kufanikiwa, mathalani umezungukwa na wapigaji wakati wewe si mpigaji n.k
8. Mwisho, muhimu zaidi jichunguze wewe mwenyewe huenda una tabia isiyoridhisha inayosababisha watu kuwa na chuki nawe. Huenda chanzo ni wewe mwenyewe na si wengine.
Pitia huu uzi, utakusaidia kama umekumbwa na kadhia hii kwa sasa...
Thread 'Saikolojia: Kushindana na wanaobeba Chuki' Saikolojia: Kushindana na wanaobeba Chuki
Makazini kuna mitandao ya ukwapuaji pesa, sasa ukijifanya hutaki au ikiletwa mtumishi mpya wanajua unakuja kukanyaga dili zao za ulaji lazima ule wa chuyaHabari ya wakati huu ni matumaini yangu nyote mpo salama.
Moja kwa moja niende kwenye mada husika.
Najua binadamu tuko tofauti lakini ningependa kupata comments tofauti tofauti kujua nini hasa hupelekea. Chuki, visasi, roho za kutendeana ubaya, malipizi, na mengineyo yasiyopendeza huletwa na nini?
Je, ni kwakuwa hujui na unaonekana mzigo?
Je, unajua zaidi yao na unaonekana kama tishio?
Au ni basi tu mtu anaamua kukuchukia bila sababu ya msingi na kukuombea kila uchwao ukumbwe na baya?
Ninakaribisha maoni.
Shimba ya Buyenze , Mshana Jr Watu8 , Omerta, @Da’Vinc , na wapendwa wengine karibuni.
Naunga mkono hoja.Jambo la kwanza, roho mbaya mtu huzaliwa nayo, na huwa inasubiri majira, nyakati na mazingira sahihi ili iweze kuanza kufanya kazi...
Binafsi katika kumtumikia kote mkoloni sijawahi kukutana na watu wa namna hiyo, isipokuwa nimekuwa nikipata kusikia visa hivyo toka kwa watu wa karibu...
Sababu ambazo nimekuwa nikizisikia huwa ni tofauti tofauti, lakini zote ni matokeo ya mtu kuwa na roho mbaya 'roho nyeusi'...
1. Ubinafsi - Hawa ni wale watu wenye umimi, kwamba kila kizuri kiwe chao na vibaya viwe vya wengine
2. Ufukara - Kuna watu ambao maisha yao yamegubikwa na ufukara wa mali, hivyo hujawa na chuki pale wanapoona mtu fulani yupo kwenye nafasi ya kupokea mkate mnono zaidi yao, au hata maisha yake nyumbani ni ya juu kuwazidi katika mali alizonazo
3. Kukosa weledi - Kuna watu waliopata vyeo au nafasi kwa ngekewa tu na wala sio kwa uwezo wa kiakili au taaluma, sasa kule kutokujiamini kwamba mtu anaweza akapokwa nafasi yake hufanya ajenge chuki kama njia ya kujilinda
4. Ukabila - Kuna maofisi ambayo watu wa kabila fulani ni kama wamechanjiwa kuwa wao ni wa ofisi hiyo tu, ikitokea wewe mwenyeji wa mkoa mwingine umeajiriwa au kupangiwa hapo, cha moto utakuona
5. Tofauti za kimaumbile/hulka/ulimbwende na utanashati - Imezoeleka kusikika kuwa watu wafupi huwa wakorofi sana, dhana hii ipo pia makazini ambapo kuna watu hukosa kujiamini kutokana maumbile yao, hujiona sii warembo au watanashati au hujiona wana kasoro fulani za kimaumbile ambazo zinawafanya wamuone mtu fulani kawazidi
6. Tofauti za kiimani - Kama ilivyo tofauti za kimaumbile, hata imani nayo huwa ni chanzo cha chuki baina ya mtu na mtu. Kuna ofisi ambazo imani fulani ya dini ina nguvu kuliko nyinginezo.
Pia kuna watu ambao huwa ni washirikina, hupelekea kuwachukia wale walio wacha Mungu.
7. Kuwa sehemu isiyo sahihi wakati usio sahihi - Isijekuwa pia upo mahali pasipo sahihi kwako iwe ni idara, ofisi au kitengo kiasi kwamba unazuia 'deals' za watu kufanikiwa, mathalani umezungukwa na wapigaji wakati wewe si mpigaji n.k
8. Mwisho, muhimu zaidi jichunguze wewe mwenyewe huenda una tabia isiyoridhisha inayosababisha watu kuwa na chuki nawe. Huenda chanzo ni wewe mwenyewe na si wengine.
Pitia huu uzi, utakusaidia kama umekumbwa na kadhia hii kwa sasa...
Thread 'Saikolojia: Kushindana na wanaobeba Chuki' Saikolojia: Kushindana na wanaobeba Chuki
Ni wivu tuHabari ya wakati huu ni matumaini yangu nyote mpo salama.
Moja kwa moja niende kwenye mada husika.
Najua binadamu tuko tofauti lakini ningependa kupata comments tofauti tofauti kujua nini hasa hupelekea. Chuki, visasi, roho za kutendeana ubaya, malipizi, na mengineyo yasiyopendeza huletwa na nini?
Je, ni kwakuwa hujui na unaonekana mzigo?
Je, unajua zaidi yao na unaonekana kama tishio?
Au ni basi tu mtu anaamua kukuchukia bila sababu ya msingi na kukuombea kila uchwao ukumbwe na baya?
Ninakaribisha maoni.
Shimba ya Buyenze , Mshana Jr Watu8 , Omerta, @Da’Vinc , na wapendwa wengine karibuni.
Wewe ndio umesema kiini cha tatizo kuu lilipo, mtu hawezi kukuchukia hivi hivi tu, eti ni hulka, umaskini, udini, au kutojiamini, hayo yote ni sawa kwa kiwango kidogo cha tabia za wasiojua kuishi bila ubaguzi.Makazini kuna mitandao ya ukwapuaji pesa, sasa ukijifanya hutaki au ikiletwa mtumishi mpya wanajua unakuja kukanyaga dili zao za ulaji lazima ule wa chuya