Chuki makazini huletwa na nini?

Habari wote…nimebananika kidogo nipatapo muda napitia comments zetu…yawezekana nisipate muda wa kureply lakini ninazisoma na tunazifanyia kazi.

Kwa yeyote aliyecomment, natanguliza Shukrani za dhati🙏.
 
Kuna mwamba kasema hapo juu kuwa ni mtu kuwa na uwezo mdogo wa utendaji kwa hyo anajikomba kwa boss kwa kupeleka taarifa za uzandiki ili akubaliwe na boss...huyu nakubaliana nae kwa 100%...na kuprove hilo...kila msaidiz wa boss akibadilishwa...lazma aanze kuweka mazingira ya kuwa nae karibu ili amrushie taulo pale anapoboronga...hii ipo sanaa kweny private institutions
 


Mwenye CHUKI hana sababu.

Kukwaruzana kipo lakini kuchukiana ni Kwa watu wenye roho Mbaya
 
Kama ilivyo UPENDO usivyo na Sababu Maalumu ndivyo ilivyo Kwa CHUKI haina sababu maalum.

Mwenye chuki rohoni atakuchukia hata kama hujamfanyia chochote.
Mwenye Upendo atakupenda bila sababu yoyote yaani mpaka unashangaa.

Asije akakuambia mtu kuwa mtu Fulani anakuchukia Kwa sababu Fulani, Big No.
Kuna tofauti ya Kuchukia na kukasirika,
Kuna tofauti ya Kutamani na Kupenda.

Hasira huchochea Chuki
Na Wakati mwingine Tamaa huchochea Upendo
 
Umemaliza kila kitu hapa...
 
Sababu ni zile zile tu Mwanadamu asiyempenda Mungu wala jiran yake..

Wagalatia 5:19-21
....uasherati, uchafu, ufisadi,
[20]ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
[21]husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
 
Jamii zetu hasa sisi watanzania tunakuwa na chuki kazini sababu ya mambo yafuatayo

Wivu _hii uja endapo mnapokea mshahara sawa ila wanahisi kuna jambo unawazidi ambalo sio tu wanaweza litimiza kirahisi ila ni mpaka waingie mikopo .

Husuda _ hii huja baada ya wivu ni pale sasa wafanyakazi wenzio wanapoona hawakuwezi tena sasa ni husda tu ili wakufelishe

Background zetu _ ukikutana na wafanyakazi wenzio ambao wengi wametokea familia za kimasikini aisee ndugu tegemea kila rangi ya ajabu hapo kazini , hasa ukiwazidi baadhi ya vitu au wakigundua uko na background nzuri dhidi yao , watajipendekeza kwako ila ni unafiki sana maana wanakuchora.

Hivyo dawa ni kuwa wewe kama Wewe timiza majukumu yako , nenda kaendelee maisha na familia yako

TEKERI.
 
Makazini kuna mitandao ya ukwapuaji pesa, sasa ukijifanya hutaki au ikiletwa mtumishi mpya wanajua unakuja kukanyaga dili zao za ulaji lazima ule wa chuya
 
Naunga mkono hoja.
Nini kifanyike
1. Penda kutulia ofisini kwako usiwe mtu wa kushinda kwenye makorido/ofisi za watu
2. Tumia masaa yako 9 vizuri ili umalize au ufanye kwa ukubwa kazi yako
3. Masaa ya kazi yakiisha beba kilicho chako nenda nyumbani au kwenye mishe zako
3. Usipende kucheka cheka, tumia system ya kijerumani/kirusi. Unacheka ukiwa na sababu
4. Kama umebarikiwa kuwa na kalamu ya endorsement, fanya bila upendeleo
5. Usipende kufanyia kazi majungu yanayoletwa na X kutoka kwa Y, kuna muda pokea yapitie upande wa pili au kusanya XY uwaambie nk
6. Usiwe mwoga kwenye kufanya maamuzi na usipende kuwa chawa kwa aliye juu yako.
7. Usipende kushea mambo yako ya nyumbani ofisini.
NB: Sehemu kubwa ya hayo juu ukiyafanya si rahisi mtu kukuelewa nini kilichoko kichwani kwako na si rahisi kukuletea mazoea ya kijinga. Ni vigumu kumridhisha kila mtu, pia hata ufanye nini wanadamu hawataacha kufanya yao. Kikubwa zingatia weledi wako wa kazi
 
Ni wivu tu
Hasahasa ukiwazidi kwa jambo flani
 
Roho mbaya na hapo ukute umemzidi kitu ndiyo usiseme
 
Makazini kuna mitandao ya ukwapuaji pesa, sasa ukijifanya hutaki au ikiletwa mtumishi mpya wanajua unakuja kukanyaga dili zao za ulaji lazima ule wa chuya
Wewe ndio umesema kiini cha tatizo kuu lilipo, mtu hawezi kukuchukia hivi hivi tu, eti ni hulka, umaskini, udini, au kutojiamini, hayo yote ni sawa kwa kiwango kidogo cha tabia za wasiojua kuishi bila ubaguzi.

Ila

MASLAHI (PESA, Wealthy) NDIYO YALIYOKUPELEKA KAZINI WALA SIO (NAFASI) KAZI YENYEWE.

Mkono mtupu haulambwi

Kimtishacho Mfanyabiashara ni Mshindani wake na Mamlaka za Kodi tu.

Na kwa nini nchi na nchi huchukiana kiasi cha kupigana.





Sent from my TA-1004 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…