Chuki na uhasama ndani ya CCM tusipochukua hatua watatuletea vita ya wenyewe kwa wenyewe

Chuki na uhasama ndani ya CCM tusipochukua hatua watatuletea vita ya wenyewe kwa wenyewe

Bush Dokta

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2023
Posts
24,831
Reaction score
45,154
Aisee hali ni tete ndani ya kile chama kilichotamba kwa miaka mingi kuwa ni chama chenye umoja, mshikamano, chenye kuheshimu utu na watu.

Sasa ni mambo ya kuviziana tu. Imefika mahali mwanachama huyu anataka mwanachama mwenzake afe.

Hii si jambo la kuhendekeza hata kidogo. Chuki na uhasama vimepamba moto.

Ni CCM vs. CCM. Wanachogombania ni kile kile:

a/ Mgawanyo wa madaraka usiolinganifu, hawa wanapewa sana kuliko sisi.

b/ Upendeleo katika kutoa fursa sawa za kiuchumi. Kundi moja linadhani linafaidi uchumi wa nchi kuliko lingine.

c/ Ndani ya chama, upendeleo umezidi kiasi mmoja anaona anamdhalilisha mwingine. Inafika hatua sasa hata wajumbe wenye mashina yao wanaowafahamu wagombea wao vizuri hawapewi nafasi ya kupendekeza mgombea sahihi badala yake mgombea anachaguliwa kutoka juu (hili tulionya sasa matunda yake yamekomaa). Mtalinywa.

Matukio yaliyotokea hivi karibuni yameibua hisia za ajabu sana. Kwetu sisi watazamaji tunaona jambo hili sio sawa.

Wote ni wa chama kimoja lakini wanasagiana kunguni kama hawajuani. Kila mmoja anamuona mwenzake ni shetani.

Matukio ya Kufariki Hayati Dr. Magufuli, Kufungwa Sabaya, Kushtakiwa Musiba, na Kifo cha Membe nadhani Deep state mnaona kinachoendelea na mnajua suluhisho ni nini. Msijifanye hamuoni. Taifa litatumbukia.

Sasa imefika kuna kundi linaona halina cha kupoteza lolote na liwe ilimradi litaumiza mahasimu bila kujali taifa litaathirika.

Mheshimiwa Rais, kama maridhiano basi yaanze ndani ya chama chako hali ni mbaya. Kuanzia viongozi wa juu hadi wanachama wa kawaida.

Nimepitia mitandao ya kijamii naona wanavyosagiana kunguni najiuliza hawa wote si wa chama kimoja?

Kama wanafanyiana hivi, je, itakuwaje kwa mtu mwenye itikadi tofauti nao?

Je, shida ni maslahi? Ni umaskini? Ni maisha magumu au ni ujinga?

Au kuna mtu anapandikiza haya?
 
Inakata roho which is good,sasa hivi ukiwaona wanagombana ni kwamba wanagombania fedha zetu za kodi tozo na mikopo ili waitafune.
Pesa zenyewe hamna hazina haina kitu. Wanagombana bure tu.
 
Back
Top Bottom