ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 25,030
- 61,298
Kuna kitu watu wengi huwa hatukikubali. Ukimweka mtu moyoni kwa chuki, hasira au maumivu aliyokutendea, mara nyingi si yeye anayeteseka bali ni wewe mwenyewe.
Fikiria mtu anayetaka kupanda mlima huku amebeba magunia mazito mgongoni. Atafika juu kweli, lakini kwa shida sana. Ndivyo ilivyo kwa mtu anayebeba majeraha ya zamani kila siku. Akikaa peke yake anawaza alivyotendwa, akilala anawaza, akiamka anawaza. Akiona mafanikio ya aliyemuumiza ndiyo maumivu yanaongezeka zaidi.
Cha kushangaza, mara nyingi wale waliokukosea wanaendelea na maisha yao kawaida. Wengine hata wameshasahau kabisa kilichotokea. Lakini wewe bado unarudia filamu ileile kichwani kila siku.
Watu wengi wanafikiri kusamehe ni zawadi kwa aliyekukosea. Hapana. Kusamehe ni zawadi unayojipa mwenyewe. Ni kuamua kushusha mzigo ili uweze kutembea kwa kasi zaidi kwenye maisha yako.
Tatizo ni kwamba kusamehe kuna gharama. Gharama yake ni kujaribu kujenga upya upendo au angalau kuondoa ule moto wa chuki ulioko ndani yako. Wakati mwingine unaweza kuanza kwa hatua ndogo sana; kupiga simu, kutuma salamu, kuulizia hali, au hata kutuma msaada mdogo kama uwezo unaruhusu. Sio kwa sababu wao wanastahili, bali kwa sababu moyo wako unahitaji kupona.
Kuna watu hawazungumzi na ndugu zao miaka 5, 10 au hata 20. Lakini ukiwachunguza kwa ndani, bado wanaumia kila wanapokumbuka yaliyotokea. Maumivu hayo yanakula furaha, yanakula amani na wakati mwingine hata yanaua hamasa ya kutafuta maendeleo.
Wakati mwingine tiba ya moyo ina gharama, lakini kutokujitibu kuna gharama kubwa zaidi