kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Ni makosa na haikubaliki kufanyia utafiti jambo ambalo sababu/majibu yake tayari yapo na yanafahamika kwa watu. Mfano huhitaji kufanya utafiti wa kugundua kwanini unasinsia mchana darasani ili hali unajua kwamba jana ulikesha kwenye sherehe. Inajulikana tayari kuwa usipolala usiku utasinsia/lala mchana na usipolala mchana utasinsia/lala usiku. Sasa kama huo ndo ukweli kuhusu usingizi itashangaza kuona mtu ambaye hakulala usiku lakini pia hasinsii mchana, ama kalala usiku lakini anasinsia tena mchana, hii sasa ndio inayohitaji utafiti maana maana sio kawaida na tabia ya usingizi, tunahitaji kufahamu zaidi kama huyu mtu anakula milungi ndo maana halali, anatumia kinywaji gani, anaumwa, ana msongo wa mawazo, n.k.
Je, kwa mfano huo hapo juu swala la wanafunzi wa kidato cha nne kufeli measurably linahitaji utafiti ama kuundiwa tume gani? Kipi hakifahamiki kinachohitaji utafiti? Waziri mwenye dhamana ya elimu hakufanya nini kuzuia wanafunzi wasifeli mitihani yao?
Ili learning itokee (take place) ni baada ya muunganiko wa mambo/factors mbali mbali yakiwemo:
1.Mwanafunzi mwenyewe: (akili, juhudi, tabia)
2. Walimu: (elimu, juhudi, uzoefu, motisha, tabia)
3. Wazazi: (mahitaji, matibabu, kufuatilia elimu ya mtoto, mazingira bora yanayowezesha kusoma, ada, kufundisha tabia
4. Serikali: (majengo, idadi ya walimu, idadi ya wanafunzi kwa darasa, mishahara ya walimu, vitabu, maabara, usafiri wa wanafunzi na walimu, ukaguzi, elimu za walimu, mitaala, chakula shuleni)
5.Baraza la Mitihani: (alama za wanafunzi kujiunga form I, usimamizi, utungaji na usahihishaji wa mitihani)
6. Jamii: (tabia za wanajamii dhidi ya wanafunzi, vilabu vya pombe kwenye makazi, ngoma na miziki kwenye makazi, usafiri wa daladala, vibanda vya video, ubakaji)
7. Utandawazi: (matumizi ya simu, internet, magazeti na majarida kwa wanafunzi)
Je, vitu hivi havipo Tanzania? Kama mambo sio shwari katika kila kipengele hapo juu hatuhitaji kufanya utafiti tena, ila ni swala la ki-management lisilohitaji utafiti (research) maana sababu za kufeli zinajulikana tayari ni kuchukua hatua tu za kiutendaji.
Je, katika mambo hayo saba niliyoyataja hapo juu Kawambwa kama Kawambwa kahusika na lipi linalomuhitaji yeye ajiuzuru kama Waziri? Hili ni swala la mfumo mzima kuanzia chama tawala, serikali, wananchi, na dunia kwa ujumla, hata ulaya na Marekani wanalalamikia matokeo mabaya kwa watoto wao, na sababu ni hizihizi.
Ukiaangalia shule zilizofanya vizuri kwenye matokeo haya utagundua kuwa walikuwa na wanafunzi bora waliojiunga form 1, wana vitendea kazi, wana wazazi wenye upeo, wana walimu wanaolipwa vizuri, n.k.
Swali la kufeli kwa wanafunzi haliwezi likaachwa juu ya mabega ya Mh. Kawambwa. Anayedai kawambwa ajiuzuri anaropoka na kupayukatu. Kwa hali ilivyo hata ukimtoa Kawambwa peke yake leo hali itabakia ileile. overhaul??!!!